NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, September 25, 2009

PESA ZAKO ZINANUKA - NA BEN R. MTOBWA

Pesa Zako Zinanuka ni Riwaya nzuri sana iliyoandikwa na Marehemu Ben R. Mtobwa na kuchapishwa na Heko Publishers mwaka 1984. Niliisoma nikiwa Mlimani lakini nilipoziona picha za hawa "waheshimiwa" nikaikumbuka riwaya hiyo. Itabidi niitafute niisome upya. Mwisho wa "waheshimiwa" hawa sijui utakuwaje. Ngoja tusubiri tuone lakini ni wazi kwamba mabilioni yao yananuka. What a legacy!8 comments:

 1. Twaweza kuwa twapigwa changa la macho hapo mkubwa. Si pesambili kakataa kutaja mashahidi wake kwa madai kuwa ni watu wazito sana ktk govt na kwamba akiwataja waweza kutishwa na wakubwa?

  ngoja tuone itakapotufikisha...yawezekana pesa zao hazinuki bali zanukia!!!!

  ReplyDelete
 2. hilo ni changa la macho (sina uhakika profesa nzuzulima unakielewe kiswahili hiki).

  kuhusu uandishi tanzania ilikuwa na vichwa zamani tuache utani. ben mtobwa na agoro anduru nawakubali sana. siku hizi ubongo wetu umeganda. ni tv na internet tu. lol! ha! ha! ha!

  ReplyDelete
 3. Bwana Mwaipopo, hicho Kiswahili nakimanya. Ni katika kupitia blogu mbalimbali ambapo nakutana na kujifunza viswahili vipya. Hata kama ni changa la macho lakini hawa 'waheshimiwa' wameshachemsha na wameshaingia katika Historia ya Tanzania kivyao vyao!

  Siku hizi vitabu vingi vya Kiswahili vinaandikwa na Wakenya na sijui Tanzania kumetokea nini. Na kwa vile sasa Kiswahili kimepigwa dafrau shule za msingi, ngoja tuone huko mbele itakuwaje.

  ReplyDelete
 4. usiwe kama msukuma matondo maana msukuma ana pingu mkononi lakini akiulizwa kuna nini anasema nduhu shida bwana, watanzania wataandika kiswahili saa ngapi na kila mtu anataka kuwa mwanasiasa aache kwenda kuwahonga watu wampigie kura atapata wapi muda wa kuandika kiswahili na kama ni ugonjwa hii ni hatari kweli juma nkamia

  ReplyDelete
 5. Bwana Juma Nkamia;

  Lakini wote kweli tutakuwa wanasiasa? Hilo kweli linawezekana? Nani atamwongoza nani? Kuna hatari sana siasa inapogeuzwa kuwa mradi wa mtu. Mimi nadhani Baba wa Taifa alikosea sana enzi zile aliposema eti mtu kuwa kiongozi ilibidi kwanza awe masikini. Ni binadamu gani masikini ambaye leo unamkabidhi shirika la umma au wizara halafu akae na umasikini wake eti analinda maadili? Kama huwezi kumpa simba au fisi (mwenye njaa) akulindie mbuzi wako, iweje tufanye hivyo kwa binadamu wakati naye ni mnyama tena hatari kwelikweli? Huku kwa wenzetu (mfano Marekani) ni lazima kwanza uwe milionea ndiyo uanze harakati za kugombea ubunge au kupewa vyeo vikubwa serikalini. Nadhani hii inasaidia kupunguza rushwa zisizo na sababu...

  Angalizo: Wewe ni mmoja wa watangazaji bora kabisa ambao nchi yetu imewahi kutoa. Wenyewe wanasema "pure talent"

  ReplyDelete
 6. Kila mtu ana haki ya kuwa mwanasiasa bila kujali kipato chake.Kudhani kuwa masikini hawapaswi kuwa wanasiasa ni wazo la kibaguzi na linalopuuza mchango wa watu masikini. Kuna watu sio matajiri lakini wana hekima ya hali ya juu.Nikukumbushe tu kuwa tajiri hajui maisha halisi ya masikini na hivyo hawezi kuwa na uchungu wa maisha ya masikini.Tangu lini jiwe lililo baharini likajua kiu ya mtende ulio jangwani?Kama utajiri ni dawa ya ufisadi ni wanasiasa wangaoi hapa Tanzania waliingia kwenye siasa wakiwa matajiri na bado wameendelea kuhodhi mali za umma? Nikukumbushe tu kuwa nyoka ni nyoka na kenge ni kenge. Marekani ni Marekani na Tanzania ni Tanzania.

  ReplyDelete
 7. Mdau hapo juu unazungumzia nini? Mbona unachokisema hakihusiani na kesi ya hawa jamaa? Kesi hiyo imefika wapi? Wangekuwa masikini ingekuwaje? Ni kweli pesa zao zinanuka, period. Ni vizuri kuelewa mada kwanza kabla ya kukurupuka kucomment !

  ReplyDelete
 8. Mzawa, hujasoma mlolongo wa hizi comment ukisoma utajua nilikuwa na maana gani.Usiwe mwepesi wa kujaji mambo kabla ya kufuatilia.cjui mimi na wewe nani amekurupuka hapo?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU