NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, October 3, 2009

ATI, AFRIKA ILIYOZOEA KUOMBAOMBA NA KUSAIDIWA, IMEPATA NINI KUTOKA KWA OBAMA?

Kuchaguliwa kwa Obama kuwa rais wa arobaini na nne wa Marekani kulipokelewa kwa vifijo na nderemo nyingi barani Afrika. Kulikuwa na matumaini makubwa kwamba Afrika sasa ilikuwa imepata "mkombozi" na mtetezi katika jukwaa la kiuchumi la dunia. Wengi waliamini kwamba kijana huyu machachari mwenye asili ya Kijaluo pengine alikuwa ndiye chanzo cha mwanzo wa kutatuliwa kwa matatizo mengi ya kiuchumi barani Afrika. Kama kawaida ya Waafrika, tulimwona Obama kama mtu wa kutusaidia na kutukomboa. "Mesiya" wetu alikuwa amefika. Oh, bahati iliyoje!

Safari ya kwanza ya Obama barani Afrika ilikuwa Ghana - taifa la kwanza barani Afrika kupata uhuru likiwa chini ya mmojawapo wa viongozi wa Kiafrika wanaoheshimika sana - Kwame Nkrumah. Naona viongozi wengi wa Afrika na Waafrika wengi walivunjika moyo Obama aliposhindwa kuahidi misaada kemkem kwa bara la Afrika. Akiwa Ghana Obama (kimsingi) aliwaambia Waafrika kwamba ukombozi ulikuwa mikononi mwao wenyewe na misaada ya Marekani (kama ipo) itaelekezwa kwa nchi zile ambazo zinajibidisha kujiendeleza zenyewe, nchi zinazoheshimu demokrasia, haki za binadamu kwa raia wake na zenye uongozi bora unaojitahidi kupambana na ufisadi. Kwa Waafrika waliozoea kuombaomba, rushwa na kupewa vya bure pamoja na kukopeshwa (wakisahau kwamba daima kukopa harusi lakini kulipa matanga), maneno haya ya Obama yalionekana kama msumari wa moto.

Obama ni raisi wa Marekani na daima ataweka maslahi ya nchi yake mbele. Kama alivyosema Mwalimu Nyerere wakati akiwahamasisha Watanzania kumtandika Idd Amin katika vita vya Kagera "nia tunayo...uwezo tunao" na tukiamua kutumia raslimali zetu vizuri tunaweza kutatua matatizo mengi tu yanayotukabili bila kutegemea misaada kutoka nje. Kwa hakika, jukumu la kujikomboa ni letu sisi wenyewe!

Sijui kama Waafrika tulimsikiliza vizuri na kumwelewa Obama, au tulivunjika moyo kwamba hakutupa misaada na mikopo (ambayo bila uongozi bora nayo huishia katika mifuko ya wachache). Waafrika wengi pengine wangali bado wanajiuliza...Obama ameitendea nini Afrika wakati tayari ameshaionyesha (au niseme ameshaikumbusha) njia ambayo kwayo inabidi kupitia ili hatimaye iweze kuifikia nchi yake ya ahadi. “Development depends upon good governance”

Hapa chini ni baadhi ya nukuu za Obama kutoka katika hotuba yake ya Ghana:

“Development depends upon good governance”

“It is easy to point fingers, and to pin the blame for these problems on others,”

“You have the power to hold your leaders accountable and to build institutions that serve the people.”

“America will not seek to impose any system of government on any other nation,” “What we will do is increase assistance for responsible individuals and institutions, with a focus on supporting good governance.”

“The purpose of foreign assistance must be creating the conditions where it is no longer needed. America can also do more to promote trade and investment. Wealthy nations must open their doors to goods and services from Africa in a meaningful way.”

1 comment:

  1. Obama ametukumbusha kwamba aliyekuw nacho ndie atakayeongezewa, ni sawa kabisa kuzisaidia zile nchi ambazo zina nia ya kujisaidia kwa maana nchi za kiAfrika zimejaa rushwa, ufisadi na uzembe mwingi tu

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU