NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, October 15, 2009

HUYU RUBANI VIPI?

Mimi huwa sipendi kusafiri wa ndege na huwa napanda ndege tu kwa kuwa hakuna njia nyingine ya kusafiri kwa haraka zaidi. Mwaka 2006 kindege cha Precision Air kilihangaika kweli kutua pale Ibadakuli Shinyanga na ingawa nilikuwa naendelea mpaka Mwanza niliomba nishukie hapo hapo kwani sikutaka tena kwenda kupata mateso katika kutua kule Mwanza. Jamaa walinikubalia kushuka kwa shingo upande. Ningekuwa kwenye ndege kama hii sijui ingekuwaje. Kuna mwingine anayeogopa kusafiri kwa ndege au niko peke yangu? Watu wa utambuzi mna suluhisho kuhusu tatizo hili?10 comments:

 1. Kama ulivvyosema ni usafiri rahisi lakini ni hatari. Lakini pia inawezekana ukasafiri na baiskeli na kudondoka na ikawa hatari, au kajikwaa na kuumia. Kwa hiyo hapa unaposafiri usiwe unafikiria sana.

  ReplyDelete
 2. Mungu wangu!! Mie ningezimia straight away....duh!!

  ReplyDelete
 3. Mh. Hii kasheshe yaliwahi kunipata hayo kwenye kidege cha LAM safari ya Beira niliiona chungu kwa mara ya kwanza nilisali kisukuma.

  ReplyDelete
 4. Mh makubwa! poleni sana nami yaliwahi kunikuta pale rubani wa precision alipozimia angani nikitokea Mza kwenda Kilimamnjaro tukarudishwa mza na air hostes (wa kiume)!!!

  Masangu, iko njia...Omwami Kamala na Kaluse watashuka na details bidae...lol

  ReplyDelete
 5. hivi kutoka tanzania mpaka marekani kwa meli siku ngapi na kiasi gani cha fedha?

  ReplyDelete
 6. yasinta katoa jibu zuri sana ukitaka kunywa asali usiichungunze chanzo chake,
  na wewe uliyesali kisukuma umenifurahisha sana hata mimi nikizidiwa huwa naita mayo badaae wazungu wananiuliza mayo ni nini ? nawaambia mama.

  ReplyDelete
 7. Actually usafiri wa ndege ni usafiri salama kupita mwingine. Problem ni ile idea ya kusafiri angani jambo ambalo some people wanaogopa kwani likitokea jambo that is it. Mimi pia sipendi dege linapoanza kuyumba. I don't like it!

  ReplyDelete
 8. hahahaa flight inna diffent stylee!!!! ndio maana napataga lagga wakati woooote nikiwa kunamohayo mapipa

  ReplyDelete
 9. Hebu msitutishe watu ambao tunatamani kupitia mawinguni jamani. Hebu jaribu kufikiria unasafiri na chombo ambacho hakigusi popote. La kutokea ni popote. Kwani ukiwa ndani ya lagga safari inabadilika? Na huyo mnywa asali awe makini maana asli hulambwa ama kuonjwa la sivyo ukinywa ukapaliwa hapatatosha

  ReplyDelete
 10. unajua kitendo cha kuruhusu vindege kama hivyo kuruka vikiwa na abiria,ni utovu wa nidhani na ni kutojari maisha ya abiria.vindege vya precision air mimi huwa sivielewi,nje vinaonekana vyenye rangi nzuri ya kuvutia,lakini ngoma nzito ukisha vipanda utaicheza ukiwa angani,utajiona kama umeisha kufa maana vinapiga kelele utadhani labda gari linapita kwenye barabara yenye mashimo!!!

  hivi serikali wanataka ndege zao zilete ajali kwa kuua makumi ya rai ndipo waje kuwa na mawazo ya kununua ndege mpya?au kukarabati ndege hizo kiufundi zaidi? mi nashindwa kujizuia kuwashangaa wahusika,!!! huu si uungwana,ndege ya rais aka!! haina matatizo yoyote,imeka njema kama ya EMERATES! lakini zile za wanyonge kama precision air utakuta hawana fikra ya kuzifanyia ukarabati ile ziwe kwenye standard! mimi hii inanisikitisha sana haswa la viongozi kutojali rai wao kwa kuwatengenezea njia nzuri za usafiri wa anga na nchi kavu na baharini ili nao raia wajisikie fresh katika kuendelea na shughuli zao za kimaisha!
  sasa mimi natoa wito kwa rais kikwete:
  PLIZ RAIS KIKWETE KAMA UNATAKA ILI TUKUCHAGUE TENA MWEZI WA KUMI ILI UTUONGOZE KWA KIPINDI CHA PILI ,TUNAKUOMBA UWAAGIZE WALE WOTE WAHUSIKA KATIKA SHIRIKA LA NDEGE,WAACHE TABIA YA KURUHUSU NDEGE MBOVU KUPAA ANGANI ZIKIWA NA RAI WAPENDWA,ILI ISIJE KULETE KILIO KWA TAIFA."UKIFANYA HIVYO NDUGU MUHESHIMIWA WATANZANIA WOTE TUTAKUPA KURA ZETU.
  SINA LA ZAIDI.
  WENU MWENYE KAJINA KADOGO "TZCHALIA"

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU