NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, October 13, 2009

KAMA SIKU ZAKO HAZIJAFIKA .....

Tarehe 15 Septemba, 2009 wanyongaji katika jimbo la Ohio kule Marekani walihangaika kwa zaidi ya masaa mawili wakijaribu kumnyonga muuaji, mbakaji na mteka nyara aitwaye Romell Broom (pichani) aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa mpaka kufa kwa njia ya sindano ya sumu. Kutokana na matumizi yake ya madawa ya kulevya kwa muda mrefu, wanyongaji walishindwa kupata mshipa wa damu katika mikono yake ili kupitisha sumu ambayo hudhoofisha kwanza mwili na baadaye mapafu na moyo na hatimaye kusababisha kifo. Pamoja na mnyongwaji kujaribu kuwasaidia wanyongaji wake kwa kulala ubavu ubavu katika meza ya kunyongea na kujaribu kukunja ngumi ili kutunisha mishipa ya damu, wanyongaji hao hawakufanikiwa na baada ya masaa mawili Gavana wa jimbo la Ohio Ted Strickland aliamru unyongaji huo usimamishwe.

Walitaka kumnyonga tena baada ya wiki moja lakini wanasheria wake wakawa tayari wameshakata rufaa na kesi hiyo bado inaunguruma mahakamani. Na Romell Broom bado yupo tu anadunda. Kweli kama siku zako hazijafika hapa duniani binadamu hata wafanyeje ni bure! Kwa habari zaidi soma hapa. Mwenyewe anaeleza hapa yaliyomsibu siku ya Septemba 15, 2009 alipokutana na kifo uso kwa uso.

5 comments:

 1. Habari yake nimeisoma, Hakuna njia mbadala ya hukumu yake, maana hapo naona wameshindwa.

  ReplyDelete
 2. kwani wakimchoma kama sindano nyingine ya matibabu yaani kwenye likalio limoja hafi? not that i wish him dead.

  ReplyDelete
 3. Bwana Mwaipopo - umenifurahisha. Pengine ataweza kufa lakini inabidi watafute mshipa mkubwa wa damu ili sumu ienee kwa haraka mwilini na mnyongwaji "AFE KWA RAHA". Tazama hapa kuona utaratibu unaopaswa kufuatwa. http://en.wikipedia.org/wiki/Lethal_injection

  ReplyDelete
 4. Vipi kumtandika risasi au ile style ya Saddam?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU