NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 16, 2009

KAMWE USINYWE POMBE NA KWENDA KUIBA

Mtu na babake wametoa kali ya mwaka kule Alabama. Baba ana miaka 37, mtoto wake wa kiume ana miaka 19. Kwanza walianza wakazitwika bia mpaka wakawa njwii halafu wakaamua kwenda kuvunja nyumba ili kuiba usiku wa manane. Kweli wakafanikiwa na wakaiba funguo za gari, dola karibia 200 na vito vyenye thamani inayokaribia dola 100 wakati wenye nyumba wakiwa wamelala.

Wakati wanajaribu kuondoka soo likabumburuka. Wenye nyumba wakaamka. Kwa akili za haraka haraka jamaa wakajibanza sehemu na hatimaye wakajificha chini ya kitanda katika chumba cha kulala. Soo likapoa. Baadaye baba akafanikiwa kuchepuka na kumuacha mtoto mvunguni mwa kitanda. Kumbe mtoto akawa amezimika mle mvunguni kutokana na kilevi.

Basi wenyeji wakalala kama kawaida mpaka asubuhi. Ndipo mama mwenye nyumba akashtukia ishu. Kuchungulia mvunguni mwa kitanda akamkuta mtoto mwizi akiwa ameutandika usingizi bila wasiwasi. Akakimbia kwenda kumwita jirani. Jirani alipokuwa basi mambo yakachangamka zaidi kwani yule kijana mwizi aliyekuwa amezimika mvunguni ni mjukuu wake. Polisi wakaitwa. Mwizi kuamshwa akawa anamuulizia baba yake. Polisi wakaondoka naye kwenda kumchukua baba yake na wote haooo korokoroni. Tangu hapo pombe siyo supu ati!

Itazame hii ishu hapa.

8 comments:

 1. teh teh teh, kama kisa cha kutunga vile kumbe kweli, woooi, walevi wana taabu sana. Umeiona ile video pale kwenye blogu yangu mtu amelewa njwii saa nne na ushee asubuuhi? juzi tu hapa tarehe 6.

  ReplyDelete
 2. Subi, si kwamba "walevi wana taabu sana" bali ulevi ni taabu kweli kweli. Mimi ni mmoja wapo wa waliowahi kuadhibiwa na ulevi...lol

  ntatoa ushuhuda siku moja baada ya kupigwa neno la uzima na mtakavitu simon...lol

  ReplyDelete
 3. Mie mara nyingi nimefanikisha kulewa hivyo saa kumi na mbili asubuhi na kustukiwa mitaa ya saa moja asubuhi!Halafu wala haikuwa kwa taabu!:-(

  ReplyDelete
 4. Subi - huyo wa kwako ni kasheshe zaidi. Naona alikuwa anajaribu kununua kreti zima la bia wakati hata kusimama hawezi. Mtu ukifikia ulevi wa hivyo basi ni hatari na pengine ni wakati wa kutafuta msaada. Nimeona watu wengi sana wakiharibiwa na pombe na pombe si kitu cha kuchezea.

  ReplyDelete
 5. pombe! naipenda ingawaje huwa inaniadhibu mara moja moja hasa ya ofa ndio mbaya.kama jana.

  hao wajamaa hawakuwa serious na kazi yao.

  ReplyDelete
 6. Mwaipopo - acha hizo. Mbona juzi tulikuwa wote na ulikuwa fit tu. Hizo pombe za ofa ulizinywa saa ngapi? Pombe nzuri ukiinywa kistaarabu. Wezi wengi hunywa kidogo ili kutoa nishai. Hawa jamaa naona walizidisha

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU