NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, October 29, 2009

KICHEKO NI TIBA - KUTOKA WAVUTI.COM

Matani kutoka Kenya kutoka tovuti mpya ya Wavuti.com (zamani nukta77.blogspot.com). Kama unavyoweza kuona kuna Ki-sheng hapa na pale; na sarufi na hasa upatanisho wa kisarufi na ngeli za majina zimeparaganyika (mf. ukikunywa maziwa inafika...). Nawapenda Wakenya kwa sababu wao hawatilii maanani sana mambo kama haya ya usanifu wa lugha kama tunavyofanya sisi Watanzania. Nimeandika makala yenye kurasa 25 inayoitwa "Kiswahili Sanifu au Kiswahili cha Tanzania?: Matatizo ya Usanifishaji katika Kiswahili Sanifu" Ikichapishwa nitawapa "link" hapa kwa wanaopenda haya mambo ya lugha. Watanzania - tunayo haki ya kudai kwamba Kiswahili chetu ndicho sanifu kabisa na kile cha Wakenya na hata kile cha Demokrasia ya Kongo (ambacho wenyewe wanadai kwamba ni sanifu pia) si sanifu?
*************************************************************************

1. Ati wee ni m-black mpaka ukiingia kwa dinga (gari), dirisha zinakuwa tinted!

2. Kwenu kuchafu mpaka mende zinatema mate, ati ‘THU’ hii hao (HOUSE) ni noma.

3. Vile wewe mfupi, ukipigwa picha ya passport inatokea full.

4. Kwenu nyi wakristu hata dogi zenu zikiona mwizi anaiba, zinawaambia “wee iba tu Mungu anakuona.”

5. Ati hao (house) yenu ina gate lakini hakuna fence.

6. We’ ni mshort mpaka ukikalia kwa pavement (sakafuni) miguu ina hang kwa hewa.

7. We mjinga mpaka uli-fail blood test.

8. Wewe ni mblack mpaka mosquito ikitaka kukuuma lazima itumie torch.

9. We ni mrefu mpaka ukikunywa maziwa inafika kwa tumbo ikiwa mala (MGANDO/MTINDI).

10. Wewe ni mweusi ukikanyanga makaa unawacha footprint za black kwa makaa.

11. Nyanyako (bibi yako) mzee mpaka chawa za nywele yake hutembea na bakora.

12. Ati nyinyi ni wengi nyumbani kwenu yaani buda (baba) yenu hajui majina mpaka huwaaddress kama wananchi. (KAMA RAISI ANAPOTOA HOTUBA)

13. TV yenyu ni Ndogo lazima ufunge jicho moja ndio uone picha.

14. Wewe mblack mpaka unasweat soot.

15. Wewe mnono mpaka ukivaa yellow watoto wanafikiria ni schoolbus.

16. Manzii (mpenzi) wako ni m ugly mpaka alikataliwa ku act horror (movie ya kutisha) Hollywood.

17. Nyumba yenyu ni ndogo mpaka lazima utoke nje kuchange mind.

18. Kwenyu nyinyi ni wengi mpaka kwa hao (house) kuna round-about.

19. Kwenyu nyinyi ni wadaft (WAJINGA) mpaka kupata driving license ilibidi mpelekwe boarding school.

20. Nywele za watoto wenyu ni ngumu mpaka mnazitumianga kama steel wool.

21. Mko wengi kwa hao (house) mpaka kuna rush hours na kukinyesha kunakuwa na jam.

22. Wewe ni mshort mpaka ukishuka kutoka kwa zile vitanda double decker lazima utumie parachute.

23. Ati TV yenu ni ndogo hadi wasee wa news huanza kwa kusema ...ati munatuona jamani?

24. Sistaako ni ugly mpaka monkey ikampatia ndizi.

25. We mblack mpaka ukikutana na mzungu afternoon anakushow good evening?

26. Ngombe yenu mzee mpaka inatoanga yogurt.

27. Kwenu kumekauka mpaka ngombe yenu hutoa milk powder.

28. Wee ni mzee mpaka ukiumwa na mosquito zinatema mate

29. Paka yenu noma mpaka iki shika panya inaitisha chumvi, fork na pilipili.

30. Kwenu nyinyi ni wengi mpaka mkipigwa family photo wengine wanatokea kama wame hang (ning’inia) kwa frame.

31. TV yenu ndogo mpaka wasee wa News (watangazaji wa habari) wamepiga magoti.

32. We mrefu mpaka ukianza kuvaa underwear mbichi by the time ifike kwa magoti imekauka.

33. Nyumba yenu ni chafu mpaka cockroach huvaa slippers (malapa).

34. Budako (baba yako) ni fala, alienda ku-buy ngombe akaona ikikojoa akasema, sitaki hiyo, imetoboka

2 comments:

 1. Asante Prof. Matondo.
  Kweli lugha na matumizi ya lugha huendana na jamii husika. Kila mmoja yupo sahihi kwa mtizamo wake na wachache hujikosoa baada ya kuwasikia wengine wakizungumza maneno yale yale ila kwa lafudhi na matamshi tofauti.
  Haya matani ya Kikenya yamenifurahisha sana!

  ReplyDelete
 2. wakenya ni noma. mtizamo wangu ni kuwa wakenya wanakipogoa kiswahili. unajua ukizaliwa dsm na ukiwa haujawahi kutoka zaidi ya kimara utauita mwinuko wa kuelekea UDSM mlima (thus mlimani). wakenya hawajawahi kukisikia kiswahili kilivyo fasana na utamu utokanao na ufasana na mtindo wake. ndio maana wanadhani cha kwao ni kiswahili sahii. si kweli. watanzania tulio wengi tunajitahidi kutumi kiswahili fasaha. hasa kwenye upatanisho wa kisarufi, jambo ambalo wakenya ama wanalipuuzia ama hawalijui kama mdarisalama asivyojua tofauri ya muinuko, kichuguu na mlima.

  ila utani wao nimeupenda. umeegamia zaidi katika rangi, utajiri na vimo vya wahusika. yawezekana hayo ni mambo yaliyotawala mazungumzo, tambo na majigambo ya mkenya wa 'uswahilini'.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU