NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 16, 2009

KWA MLIOKUWEKO: MNAZIKUMBUKA IMANI NA AHADI ZA MWANATANU?


Kumbe bado hazijabadilika na bado nazikumbuka karibu zote kwa kichwa. Duh!


IMANI YA CCM


 • Binadamu wote ni Sawa
 • Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
 • Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru


AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI


(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja

(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

(3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.

(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

2 comments:

 1. Hizi amri wengine tuliziimba shuleni huko madarasani katika somo la Siasa, haswa amri hizo ulizokolezea wino.
  Sasa katika haya lipi lililokuwa baya hadi leo wayaone ya marehemu Mwalimu hayafai?
  Alijisemea mwenyewe, 'ajabu yenu, hata yale mazuri mnatia question mark?'... hakukosea, majitu yamekuwa mambumbumbu kabisa mizungu ya reli.

  ReplyDelete
 2. ''8.Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.''

  Hivi katika viongozi wetu [Nyerere included] kuna aliyefanikiwa kufuata hii?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU