NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, October 12, 2009

KWA NINI WAAFRIKA "TUNAKATAZWA" KUABUDU MABABU ZETU WALIOTUTANGULIA?

Jana asubuhi katika viwanja vya St. Peter Square kule Vatican Papa Benedict XVI alimtangaza "Baba" Damien De Veuster (January 3, 1840–April 15, 1889) kuwa Mtakatifu. "Baba" Damien De Veuster anakuwa Mtakatifu wa kwanza kutoka jimbo la Hawaii. Nilitembelea Hawaii mwaka wa 2005 kwa wiki mbili na Molokai -mahali alipoishi kwa miaka mingi akiwahudumia wagonjwa wa ukoma mpaka alipofariki (kwa ukoma pia) - ni mojawapo ya vivutio vya utalii.

Kama tunavyojua, "watakatifu" hawa (ambao ni lazima wawe wameshakufa) katika kanisa la kikatoliki huombwa na kuabudiwa; na inasemekana wana uwezo wa kutenda miujiza. Ili kutangazwa mtakatifu inabidi angalau miujiza miwili ya kiuponyaji itokee na iambatishwe moja kwa moja na anayetaka kutakatifishwa. Huu ndiyo utaratibu ambao Mwalimu Nyerere itabidi afuate kama kweli kanisa la kikatoliki linataka kumfanya kuwa Mtakatifu.

Swali langu ni hili: Mbona Waafrika wakisali na kuomba kwa mababu zao waliowatangulia wanaambiwa kwamba wanaabudu mizimu na wakiwaabudu hawa watu "waliotakatifishwa" na kanisa ni sawa?

3 comments:

  1. Kila kitu ni imani. Nasubiri kwanza nione wengine watasema nini:

    ReplyDelete
  2. Imani kwa sisi Waafrika kukatazwa kuabudu wazee wetu eti ni dhambi? Ni ukoloni wa kiakili kwani tumetawaliwa sana kisaikolojia. Hakuna sababu yo yote eti huyu jamaa aliyekufa na ukoma aabudiwe na mimi nisiweze kuabudu katika kaburi la Babu kule Tukuyu eti kufanya hivyo nitafanya dhambi.

    ReplyDelete
  3. shida ni kuwa ukristo ulitekwa na wajanja - wazungu. it is europeanised Christianity. wazungu ndio waliotutawala ki mwili na kiakili. hakuna namna ya kunyofoka kutoka minyororo yao ya utumwa huu. Ila kwa nyerere nina kigugumizi hivi.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU