NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, October 19, 2009

MAWAZIRI NA WABUNGE WENYE VYETI VYA KUGHUSHI

Wakati wengine wanasota miaka 6-10 (kwa hapa Marekani) kupata shahada za uzamivu (PhDs) inasemekana waheshimiwa hawa wao waliamua kupita njia za mkato, wakaudanganya umma na kujipatia madaraka tena makubwa sana (na nyeti). Watachukuliwa hatua yo yote au ni "siasa" tu mtindo mmoja?

MAWAZIRI

(1) Dk. Mary Nagu (Viwanda, Biashara na Masoko)

(2) Dk. Diodurus Kamala (Ushirikiano wa Afrika Mashariki)

(3) Dk. Makongoro Mahanga (Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana)

(4) Dk. David Mathayo David (Kilimo, Chakula na Ushirika)

(5) Dk. Emmanuel Nchimbi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa-JKT)


WABUNGE

(1) William Lukuvi (Ismani-CCM)

(2) Victor Mwambalaswa (Lupa-CCM)


(3) Dk. Raphael Chegeni (Busega-CCM)

Kwa habari kamili soma hapa

Halafu mwangalie huyu mwenzao hapa uone tofauti!

3 comments:

 1. Hivi what is in a name (Dr)? the spellings or the knowledge. what is the meaning of branding yourself a PhD while you are empty headed? Jamani/Bagwitu!

  mie nina cheti cha shule ya msingi nilichofoji. hakifai kuombea uwaziri wa blogu?

  ReplyDelete
 2. Inasikitisha! Ingekuwa kwingine hii ingekuwa ni skendo na watu hawa wangekuwa wameachia ngazi wenyewe bila kulazimishwa na mtu. Lakini kwetu sisi ndiyo kwanza jamaa wanatanua! Mtu unapewa wizara ukidai una PhD kumbe pumba tupu! Ni Watanzania wangapi ambao wameshaathirika na huu upuuzi?

  ReplyDelete
 3. Cha kufurahisha zaidi ukisoma hata profile ya Nhcimbi kwa mafano kwenye tovuti ya Bunge ati utaona alikuwa amesoa MBA Mzumbe na wakati huo huo alikuwa anafanya PhD na akavimaliza vyote kwa wakati mmoja, Now that is jiniasi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU