NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 30, 2009

NINA WASIWASI NA SHULE ZA SEKONDARI ZA KATA

Lengo letu ni zuri sana. Kila kata iwe na shule yake ya sekondari. Lakini tumejiandaaje? Kuna walimu wa kutosha katika shule hizi? Kuna vitabu? Kuna maabara? Mazingira kwa ujumla yakoje? Watoto kweli wanapata elimu kama inavyotakiwa? Picha hii ya mama mpishi wa shule imenitatanisha!

5 comments:

 1. Nakubaliana nawe 100% hakuna aliyewaza kwa umbali zaidi.Ni mada nzuri sana .

  ReplyDelete
 2. Mi nataka kujua - hii shule ina wanafunzi wangapi? I am just curious!

  ReplyDelete
 3. hizi shule za kata nyie mlio ughaibuni mzisikie bombani tu. ni zaidi ya "bora shule". kwa mfano darasa la saba katika shule ya msingi mwaipopo lina wanafunzi 80 mwaka huu, mwakani wanafunzi 75 au wote 80 watakuwa fomu wani shule ya secondari nzuzulima, ambayo iko kilometa moja tu toka shule ya msingi mwaipopo. ha! ha! ha!

  ReplyDelete
 4. Shule za kata zina mapungufu mengi sana ukiacha
  ukosefu wa maabara na vitabu shule hizi hazina kabisa
  walimu maana hata kama utakuta shule yenye wanafunzi
  300 ina walimu wanne, walimu hao watakuwa wakijishughulish
  a na kazi zao binafsi na si kufundisha.

  Hivi sasa shule nyingi za kata zimekimbiwa na
  walimu ambao wengi wao wameenda vyuo vikuu kusoma na
  wengine wameenda vyuo vya diploma wale wenye leseni ya
  muda mfupi.

  Kuna tatizo la mahala pa kuishi pia,mwanafunzi
  anayetoka mbali kiasi cha km 30 hulazimika kupanga
  karibu na shule anayosomea na hivyo kwa watoto wa kike
  wengi sana wanajazwa mimba.Kutokana na matatizo hayo
  shule nyingi zinatoa matokeo mabaya sana katika mitihani
  ya taifa kwa mfano kuna shule moja huko Ukerewe mkoani
  Mwanza ambayo katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne
  hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepata daraja la kwanza,
  la pili au la tatu mwanafunzi wa kwanza katika shule
  hiyo alikuwa na daraja la nne alama ya 28 sasa tujiulize
  hao wanaoshindwa wataenda wapi au watafanya nini?
  Tumaini Munale-mkufunzi,chuo cha ualimu Bunda.

  ReplyDelete
 5. Kama nilivyosema hapo juu, wazo la kila kata kuwa na shule yake yenyewe lingekuwa wazo la kimapinduzi kweli kama lingeandaliwa na kutekelezwa vizuri. Nakumbuka mwaka ule nimechaguliwa/nimeshinda/nimefaulu kwenda kidato cha kwanza kule Bukoba nilikuwa peke yangu pale kijijini kwetu na nakumbuka mara ya kwanza niliporudi nyumbani majirani walikuja kunijulia hali. Sasa hivi kuna wanafunzi wengi sana ambao wako sekodnari na wengi wao wanasoma shule za kata. Kufaulu mtihani wa darasa la saba sasa hakutishi tena kama zamani na hii ni ahueni kubwa. Nilitembelea shule moja nilipokuwa nyumbani na niliona mazingira ambayo hayakunitia moyo wala matumaini - maabara hakuna Bunsen Burner hata moja na majengo hayakuweko. Kweli ni "bora shule". Hii pia ilinikumbusha mwaka nilioenda kidato cha tano kule Sengerema High School kusoma HGK. Kutokana na kuwa na first class nzuri sana nilitegemea kwamba pengine ningepelekwa shule inayojitosheleza. Haikuwa hivyo. HGK ndiyo ilikuwa imeanzishwa pale Sengerema na hakukuwa na vitabu wala walimu. Wanafunzi wenye wazazi wajanja walikimbilia Mzumbe na kwingineko tukabakia "vichwa ngumu" wachache pale Sengerema na kusema kweli tuliokolewa hasa na "notisi" kutoka huko huko Mzumbe. Inashangaza kwamba tuliweza hatimaye kufaulu mitihani ya kidato cha sita vizuri. Sijui kulikuwa na ulazima gani wa kufungua mkondo wa kidato cha tano wakati maandalizi yalikuwa bado hayajakamilika. Baada ya muda mchache tu mkondo huo ulifungwa na "combination" za sayansi zikatawala. Ni wazi hakukuwa na maandalizi ya maana. Na sasa tunataka kubadilisha lugha ya kufundishia katika shule za msingi kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Sijui kama tumejiandaa au tunakurupuka tu kama ilivyo kawaida yetu.

  Kwa vile shule nyingi za kata zipo vijijini walimu wengi wanakimbilia mijini ambako, mbali na mambo mengine, kuna twisheni na mazingira ya kufanyia kazi yana uafadhali kidogo. Elimu - ambayo ndiyo mkakatati-mama wa maendeleo katika jamii yo yote ile bado tunacheza nayo - halafu eti tunategemea kuendelea!

  Bwana Tumaini Munale naomba tuwasiliane. E-mail yangu ni profesamatondo@gmail.com. Asante

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU