NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, October 24, 2009

NYIMBO ZA KISUKUMA/KINYAMWEZI HIZI HAPA25 comments:

 1. Nimezipenda hizi nyimbo za kisukuma ingawa nimeelewa nano moja moja. Safi sana kukumbuka nyumbani na kujali utamaduni wetu. J´pili njema kwa familia yako yote, pia kwa wtu wote.

  ReplyDelete
 2. Kaka Masangu matondo Nzuzulima naona umeweka picha mpya hapo safiii sana umependaza:-)

  ReplyDelete
 3. Picha ya zamani ya form IV hiyo enzi zileee!!! Kazi yako naimalizia na nitaileta wiki inayoanza kesho

  ReplyDelete
 4. Profesa, hivi Wasukuma na Wanyamwezi tofauti yao hasa ni nini?

  ReplyDelete
 5. Simon - hakuna tofauti kubwa. Lugha karibu ni ile ile na utamaduni ni ule ule. Tofauti ililetwa na wazungu wa mwanzo ambao katika uchambuzi wao wa lugha waliainisha kwamba Kinyamwezi na Kisukuma eti zilikuwa ni lugha tofauti (mf. Malcom Guthrie - 1971) na hivyo zinazungumzwa na makabila tofauti. Ukitoa huu ukungu ulioletwa na wazungu - Wasukuma na Wanyamwezi hawana tofauti yo yote ya msingi. Wote ni akina ngosha tu!

  ReplyDelete
 6. Asante kwa hili Profesa!

  Nimekuwa nikijiuliza kwa muda hiki kitu mpaka ikabidi niulizie hiki kitu kwa kuwa mie nilikuwa nashindwa kutofautisha .:-(

  ReplyDelete
 7. Kaka umenifikisha nyumbaniii!leo kazi ni moja tu kusikiliza hizi nyimbo,naona watu hapa wananishangaa lakini mimi nawaambia hawajui nini wanakikosa,hakuna kitu kizuri kama mtu kuwa na lugha,mila na utamaduni tofauti na wengine,likifika hilo la lugha na tamaduni, kweli huwa najivunia sana Tanzania.

  ReplyDelete
 8. Yaani najiona niko Shinyanga nikisigina zile karanga kwa ajili ya kupika mzubo. Matondo hivi unamfahamu Mzee Maiko Shilinde anatumia marimba ya mkono alikuwa anaimba sana redio Tanzania?

  ReplyDelete
 9. Ng'wanasayi - bado unakumbuka kusigina karanga eeh. Vizuri. Mzee Maiko Shilinde simfahamu lakini marimba ya mkono nazifahamu sana. Enzi zile kule vijijini ilikuwa ni marimba, zeze au filimbi. Utaalamu wangu mimi ulikuwa zeze na filimbi na mpaka leo bado nalicharaza zeze vizuri sana na ukinipa filimbi basi "nitakuimbia" nyimbo nyingi sana zikiwemo "maua mazuri yapendeza, ukiyatazama...", "Tanzania, Tanzania, ninakupenda kwa moyo wote", "Mungu ibariki Tanzania, wabariki viongozi wake...", "Bwana Mganga nipe mite ya gupela nubugota bogupanza, unichime nulushinge..." Kazi kweli kweli!

  ReplyDelete
 10. Bwana Matondo,
  Kwanza, napenda kutoa shukurani nyingi kwa kazi nzuri unayoifanya, mfano mzuri wa kuigwa na wote ili tudumishe utamaduni wetu wa ki- Africa.

  Bwana, SIMON KITURURU, aliuliza swali?

  ALIULIZA KAMA KUNA TOFAUTI KATI YA WASUKUMA NA WANYAMWEZI.


  Kabla sijajibu swali lako kwa kirefu napenda kutoa funguo mbali mbali za swali hili ili zisaidie kuelewa kiundani.

  Mpaka sasa jina la kabila hili kubwa halijulikani ni kabila gani, lakini kutokana na ufahamu wangu, labda tuliite (BANHU) au WABANTU, watu hawa wana ongea lugha moja, tofaouti yao ni matamshi na maneno machache sana ambayo yanatokana kupanuka kwa lugha na sababu zingine ambazo labda huenda sizijulikane.
  Neno “BA” au “BAA” ni sawa na neno “WA” kwa Kiswahili,
  SUKUMA, KIYA, NG’WELI, DAKAMA,


  Neno, SUKUMA
  maana yake kaskazini—haya ni maeneo za sehemu za mwanza na nyanda zake.
  Neno, KIYA
  maana yake mashariki --- haya ni maeneo za sehemu za magu,(ntuzu) na nyanda zake(Bana ntuzu)
  Neno, DAKAMA
  maana yake kusini- haya ni maeneo yaTabora, kahama, na nyanda zake(nyamwezi) wanyamwezi(unyamwezini.
  Neno, NG’WELI
  maana yake magharibii- haya ni maeneo ya nyanda za Geita na nyanda zake.

  Tukirudi kwa kilugha, au KIBANTU kama nilivyoeleza hapo juu, inaonyesha kwamba, (Bana- sukuma au Baa- sukuma) inaleta maana nyingine kabisa ambayo ni, watu wa kaskazini, Kwa sababu hii kunakuwa hakuna kabila la wasukuma, bali watu wa sukuma, (bana sukuma, au Baa sukuma, wa kaskazini, na ukiendelea, wadakama ambao ni wanyamwezi, wana julikana kwa jina (Bana dakama au Baa dakama) maana yake ni watu wa kusini na sio kabila
  (Bana kiya au baa kiya) ni watu wa mashariki na hakuna kabila la Kiya, na Bana ng’weli au Baa ngweli) hakuna kabila hilo pia.
  Kutokana na sababu hii kuna kuwa hakuna kabila la (kisukuma, kidakama, kina ng’weli na Kiya)
  Sababu nyingine ni inayofanya yaonekane kama ni makabila tofaouti ni kutokana na kutafasiri lugha hii ninayoiita (WABANTU) katika kiswahili, na mara inapoingia katika kiswahili inaleta tafasiri nyingine kabisa na kuleta maana ya kabila tofauti kabisa, mfano kabila la kisukuma.
  Swali langu ambalo nalifanyia utafiti bado mpaka sasa, hawa watu wa pande nne ambao nimezitaja hapo juu wanaongea kabila moja, ni kabila gani? Kwa sasa jina ambalo nalitumia wakati huu wa utafiti wangu ni BANHU, ni kiwa na maana wabantu.

  Rafudhi.
  Kwa mfano, mimi mtu wa (sukuma),wa- kaskazini, nikikutana ma mtu wa Kiya mashariki, rafudhi zetu zinakuwa tofauti, katika kusalimiana hata kimaongezi, lakini tunaelewana pamoja na tofaouti ya rafudhi na matamushi.

  Salaam ni utamburisho
  salaam ni utamburisho, kwa watu wa sukuma kwa mfano,, muundo wa salaam ni utamburisho au kujitamburisha, ukisalimiana na mtu ni sawa na kujitamburisha, wewe ni nani, unatoka sehemu gani katika pande nne za za hili kabila au dunia na ukoo wako ni ukoo gani? ukimaliza kusalimiana, tayari utajua huyu ni wa ukoo gani na anatoka sehemu gani wa pande hizi nilizo zitaja, kama itakuchanganya kutomjua huyo unayesalimianaye, kwa watu wa sukuma ni kawaida kabsia kumuuliza mtu( wazenga he Bhaba au mayu?) ikiwa na maana unakoishi wapi Baba au mama, jibu kwa kawaida huufuata kama lifuatavyo, Nene baba nazenga (Ma-sukuma) mimi naishi au natokea sukuma, ikiwa na maana mimi naishi au natokea kaskazini

  Mfano.

  Mtu wa (sukuma) kaskazini akiongea, huwa anakazia sana maneno yake na kwa sauti ya juu, ukilinganisha na (wadakama) wanyamwezi, wa kusini, wao wanaongea kwa ulaini zaidi na sauti ya chini, na kama ukiwa mbali inasikika kama wimbo Fulani kwa mbali uimbwao kwa maringo na usanii.


  Jina langu naitwa: Ideka makolobeka.

  ReplyDelete
 11. samahani kwa wasomaji wote, jina langu naitwa, Ideka Makolobela na sio makolobeka, kidole nacho huteleza.
  Ni mimi:
  Ideka Makolobela

  ReplyDelete
 12. Sawa Bwana Ideka Makolobela. Tumekupata. Asante sana kwa uchambuzi wako wa kina kuhusu tofauti kati ya Kisukuma na Kinyamwezi na natumaini kwamba Bwana Kitururu na wasomaji wengine wanafaidika sana na uchambuzi wako makini. Tunakuomba tu USIJE UKAPOTEA na tunategemea kusoma maoni yako hapa na kwingineko mara kwa mara.

  Malcom Guthrie (1971) katika uchambuzi wake alizitenganisha lugha hizi mbili (Kisukuma ni F.21 na Kinyamwezi ni F.22) na wanaisimu wengi huzichukulia hivyo. Japo zina tofauti za hapa na pale (kama vile toni) na baadhi ya sauti kama ulivyogusia, kimsingi Mnyamwezi na Msukuma wanaweza kusikilizana bila wasiwasi. Kwa hivyo (kwa vile mimi ni Msukuma) tunaweza kusema kwamba Kinyamwezi ni lahaja ya "Dakama" ya Kisukuma, japo sitashangaa pia kama Wanyawezi watasema kwamba Kisukuma ni lahaja ya "Sukuma" ya Kinyamwezi. Lakini tukiangalia idadi ya wazungumzaji basi Wasukuma tunashinda!

  ReplyDelete
 13. Labda na mimi niseme(kidogo) ninayoyajua kuhusu tofauti kati ya Wanyamwezi na Wasukuma.Inaweza ikawa ni vizuri kusoma yaliyopo Bujola kuhusu historia ya Wasukuma-hapa wanasema Wasukuma walikuja kutokea sehemu za Magharibi/Kusini Magharibi ya Mwanza. Nilipokuwa kijana mdogo nilipata mmmm tuseme bahati/nafasi,ya kufundishwa/kuelezwa kuhusu historia ya Wasukuma na mambo kama hayo;Wasukuma(nilivyofundishwa) walitokana na familia moja iliyotoka Kusini mwa Shinyanga na kuliacha tuseme Kabila X,kabila X lilikuwa linajumlisha Wanyamwezi;na baadaye Wanyamwezi nao wakaenda kaskazini mwa Tabora,kwa maneno mengine Wasukuma walianza wakiwa wachache;kwa ujumla hii ndiyo tofauti yao,kama kuna tofauti,isipokuwa kimila kuna vitu vichache sana ambavyo unakuta mmoja anafanya mwingine hafanyi.Ni maajabu kukuta Makabila kama Wachaga wanajumlishwa pamoja,wakati Mrombo,Mmachame,Mmarangu,Mkibosho,n.k.,lugha zao
  zina-elekea kutofautiana.Nijuavyo Wasukuma na Wanyamwezi ni wamoja kihistoria,na kuna wakati baadhi ya Wasukuma wanaweza kuwaelewa Wanyamwezi kwa haraka zaidi kuliko Wasukuma wa pande nyingine;mfano muda kuna Wasukuma hawatenganishi kesho na jana wanaita 'IGOLO',na neno 'MAZULI' kwa wengine lina maanisha jana na kwa wengine ina maanisha juzi!

  ReplyDelete
 14. Nyimbo nzuri sana, vipi unaweza kuwa na nyimbo za ng'wanakanundo au wale waimbaji wa ntuzu.

  ReplyDelete
 15. NAJISIKIA KAMA NIPO SHIMIYU KABISA. NAKUMBUKA ENZI ZA UTOTONI WAKATI TIKICHUNGA NG'OMBE NA KUPATA UGALI WA SAA MBILI ASUMBUHI. MIMI PIA NILIKUWA MTAALAMU WA KUPIGA NDONO NA GETEGETE. MPAKA SASA BADO SIJASAHAU. NITAFURAHI SANA KAMA NITAPATA NYIMBO ZA ZAMANI ZA BUKOBOGA NA BWIGASHE.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Yuuu Bhebe Nang'ho,Safi sana kwa kutukumbusha nyimbo za nyumbani maana imekuwa muda kitambo tangu zipotee masikiioni mwangu mwaka 1992 kipindi hicho tulikuwa tunawaangalia bure tu wakina manju wa Bhukoboka na Gadete;mpaka sasa nazitafuta sana hizo nyimbo,haswa za waimbaji wa Ntuzu kwenye Ding'ha wakati wa sabasaba sikukuu yetu.

   Delete
 16. Obeja sana nkoi otula mimbo giswe akisukuma mtandao,baguugimba na bhazungu du;bhebhe nadula ukapandika mimbo a bhalengi ba Bariadi

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nasege Mkisukuma Hahahaha heee heee !!!!,maana yake Natogwa hangi a henaho,Mimi jina langu naitwa Cheyo John Gwanchele kutoka Kinang'weli Bariadi-Simiyu ila kwa sasa Nakaa Shinyanga Kimasomo,Yes yawezekana kuzipata ila ongea na wadau tu utazipata wala usikimbie,Wabeja sana bwana Matondo.

   Delete
 17. Bhing'wi bhagalu na bhagika!! Mlimhola!! Tukumana twiizukija!! Sawaka ng'wanagandila nisanya limakobha!! Umnamhuli aha-makobha wite nh'ani!! Nduhu u-kushoka nazumalagwa kamli nalindebha! Yu natosha henaho! Uligigi aliho mnhu okunambilija nalichola pya-mimbouwa ga bhalingya bhakale! Tagala, ng'wanagandila, ng'wanasele, ng'nashitobelo agose bhalibalingi bhamakanji!! Nambilijagi bhadugu bhane! Ilina lyane Na-li BHUJIKOU MALEIMI BHULOGO

  ReplyDelete
 18. Bhasukuma ng'wanizukiza bhadugubhane bhana geta, na mshinyanga bha madebe mwanajinasa, mwabheja sana bhadugubhane welelo amulindeeeeeeee

  ReplyDelete
 19. Vipi kijana! Ninajaribu kurejea ulingoni japo kwa kuchechemea. Naomba sana hizo za Kisukuma na Kinyamwezi. Nimezisikiliza na kunivutia sana. Chonde chonde fanya hivyo ndugu yangu.

  ReplyDelete
 20. Historia ya Wasukuma na wanyamwezi iko hivi. Kulikuwa na familia moja maeneo ya Cameroon ya kusini hao jamaa walikuwa wakulima na walikuwa wanafuga pia. Familia hiyo ilikuwa ya kuhamahama kutafuta maeneo kwa ajili ya shughuli zao, ndipo hapo walipoondoka maeneo hayo na kuelekea upande wa mashariki. Hao jamaa kabila lao halijajulikana kwa maadishi. Watu hao walikuwa hawapendi misitu minene walipendelea zaidi maeneo yenye misitu ya kadiri ndiyo maana katika kuhamahama kwao walielekea mashariki zaidi kuliko kusini kwa sababu kusini kulikuwa na misitu minene ya Congo, na upande wa kaskazini maeneo yalikuwa yanakaliwa na watu kama tunavyojua kupitia maandiko matakatifu kuwa watu walisambaa kutoka maeneo ya mashariki ya kati pamoja na Misri. Basi, miaka ilisonga na idadi yao iliongozeka sana na waliendelea kwanda mashariki hadi walipolikuta ziwa victoria (Nyanza) walipofika hapo walitawanyika wengine walipita upande wa kulia na wengine upande wa kushoto wa ziwa. Jamaa wale waliopita upande wa kushoto walinyoosha hadi Kenya huko wakiitwa Wakamba na wale waliopita kulia walifanya makazi yao ukanda wote wa kusini mwa ziwa Nyanza. Pia kwa wale walio pita kulia kuna wale ambao hawaku-settle kandokando mwa ziwa Nyanza walinyoosha kusini zaidi na kujikuta wakifanya makao maeneo ya Bukombe, Kahama, Tabora na maeneo mengine (Hao wakaitwa wanyamwezi) na wale waliobaki kandokando ya ziwa walijikuta wakibanana maeneo hayo na kuanza ku-move kuelekea kusini wakijitambulisha kuwa wao wanatoka kaskazini (sukuma) na jamii waliyoikuta huko ikawaita wa-sukuma, yaani watu wa kaskazini au Northern people kwa ile lugha ya akina white. Hapo ndipo wapopoteza jina la kabila lao ambalo nafikiri ni WAKAMBA. Ikumbukwe pia kuwa wasukuma wamekuwa wakiongezeka kwa njia nyingi ikiwemo kuzaa sana kutokana na shughuli wanazozifanya (yaani wanapenda kupata watoto wengi ili kuongeza manpower katika jamii yao). Njia nyingine kabila la wasukuma kuongezeka ni kabila ndogo ndogo kujikuta zikigeuka kuwa wasukuma kutokana na wasukuma kupenda kuongea lugha yao, kwa hiyo jamii zingine hujikuta zikiongea kisukuma ili kunufaika na upole na ukarimu wa msukuma. Familia za kinyiramba zilizogeuka kuwa wasukuma ni nyingi tu hasa katika maeneo yaliyo hamiwa na jamii za kisukuma vivyo hivyo kwa wasumbwa, wakerewe, wazinza, wasangu na kabila nyingine nyingi tu. Njia nyingine ni intermerriage, ambapo yeyote anayemuoa au kuolewa na wasukuma hubadilika na kuwa msukuma (hii ni kwa level ya vijijini. Mijini inaweza kuwa sivyo). Hayo ndiyo niyajuayo kuhusu kabila la wasukuma. Ongezeko la wasukuma kwa sasa ni kubwa mno tofauti na watu wengi wanavyoweza kufikiri. Wanyamwezi na Wasukuma ni jamii moja utofauti wa lafdhi ni kutokana na utofauti wa maeneo wanayoishi tu lakini LUGHA NI MOJA.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mimi ni mwandishi wa vitabu ambaye nimekuwa na interest na historia lakini kwa kudra yake mola ameweza kunifunulia yote yaliyofichika kuhusu watu wa Afrika hususani wa mashariki.

   Nilianza kuandika upuuzi kidogo lakini kitabu changu kimoja kilinikosanisha na wazee mpaka kufikia bapaya lakini nilisimama na Mungu wangu akaniepusha na balaa. sasa niko kiimani zaidi.

   Nikikua kiimani niliandika falsafa ya mwanamuziki mashuhuri
   kumbe niko safarini, bila kulewa Neno nikaitafuta imani zaidi! Na huko nikachota mengi kuhusu kumfahamu Mungu.

   Sasa hivi naandika kitabu mkakata cha kiimani asilia cha kurasa 250. nimejichunguza mwenyewe na kupitia watu wangu nimewafahamu wengine pia.

   Mimi ni msukuma (chotara wa kisukuma) baba atokea eneo la Sukuma, Mwanza pale ambapo walipoanzia kutawala wasukuma kabla ya kutwaa nchi ktk karne ya sita. Yeye ni wa ile monarch ya kwanza kati ya zile tano za mwanzo; hivyo mie ni prince-sharifu. mama yangu anatokea Usia, Shinyanga katika utemi wa Makwaiya, ktk ukoo wa ma-manju -huko mimi ni manju na hivi sasa nakamilisha albamu yangu yenye vitomeo vya kisukuma. pia nina mashiko ktk unyamwezi yote. pamoja na kuwa elimu ya juu katika uongozi na uhasibu bila kusomea historia, nawatambua watu hawa kwa ndani sana.

   zimepigwa porojo nyingi lakini kitabu changu kinachofuata kitawafungua kutoka ktk kongwa za utumwa wa kutofahamu mtokako.

   Mtawajua hao watu na hakuna atakayebabia tena, mtajua jina Mwanza asili yake, ziwa Victoria, mtaijua Bagamoyo, mtaijua Dsm, mtamjua Mzanaki, Zanzibar ya akina nani, Mtasafiri hadi Zimbabwe na kutokeza Liberia.

   wacha niseme kiswahili cha kikwetu-mtajua na kujuaga! Matondo ikalaga chonjo!

   Wasalaam,

   Delete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU