NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, October 27, 2009

RUSHWA WAKATI WA UCHAGUZI: NI KOSA LA WAGOMBEA AU WAPIGA KURA?

Tumefika mahali sasa – pengine kutokana na umasikini uliokithiri na ukosefu wa elimu-elimishi – wapiga kura wengi sasa wanafikiri kwamba rushwa wakati wa uchaguzi ni HAKI YAO. Ni ukweli ulio wazi kwamba bila kutoa rushwa huwezi kuukwaa udiwani na hasa ubunge. Nilikuwa nyumbani wakati wa uchaguzi mkuu uliopita na kimsingi nilichokiona hakikuwa “demokrasia” bali mashindano ya kutoa rushwa – kuanzia magunia ya chumvi, sukari, mabati, kanga, vitenge, baisikeli na wajanja waliweza kupata mpaka pikipiki, mitaji ya kufanyia biashara na hata kujengewa nyumba kabisa. Mzee wa vijisenti alikujulikana kwa kufanya iliyokuwa inaitwa “kufuru”. Ni kwa sababu hii sikushangaa sana niliposikia kwamba alikuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali za ufisadi. Mabilioni ya shilingi aliyokuwa akiyamwaga wakati wa “kufuru” zake inabidi yalipwe kwani hakuna cha bure hapa duniani.


Basi kama hivi ndivyo, tumlaumu nani katika hili sakata la rushwa wakati wa uchaguzi? Tumlaumu mgombea ubunge ambaye anajua kwamba bila rushwa hatachaguliwa hata kama awe na sera nzuri namna gani, au mpiga kura ambaye hatoi kura yake bila kupewa sukari? Nini suluhisho la mduara huu usio na fundo? Hii kweli ni demokrasia?

7 comments:

 1. Maana ya haya uliyoyaeleza, ni kwamba wanasiasa ni zao la jamii. Hawawezi kuwa tofauti na jamii ilivyo. Wao wakiwa mafisadi, maana yake na sisi ni mafisadi hata kama kwa kawaida tunawaona wao zaidi. Wa kulaumiwa kimsingi ni wote kwa uzito tofauti.

  Kwa jinsi ufisadi ulivyoweza kutengeneza 'mfumo' imara katika jamii kwa maana ya mduara huo tunaouona hapo, tukitaka kuumaliza inabidi tuamue kuanza upya. Tubomoe kila kilichopo na tuanze ujenzi wa jamii mpya.

  Mbegu haiwezi kuota bila kufa. Nashawishika kuamini kuwa pasipo kwanza jamii iliyopo kufa, hakuna kitakachaoendelea.

  ReplyDelete
 2. Swala linachanganya hili na sijui tumlaumu nani. Mfumo mzima umeharibika. Elimu pengine itasaidia. Wananchi wakianza kupokea rushwa halafu wanapoenda kupiga kura wanachagua mtu ambaye wanadhani kwamba atawasaidia itabadilisha sana mambo.

  ReplyDelete
 3. Dr. Matondo hapa wa kulaumiwa ni mwananchi. Kwa sababu wananchi wanelewa kwamba hivyo vizawadi wanavyopewa (wanavyohongwa) na wagombea uchaguzi kama vile Kanga, Vitenge, Kofia, Sukari, na michele havilingani na thamani ya kura zao.

  Isitoshe miaka mitani ijayo mgombea atakuja tena kuwahadai na vijizawadi uchwara, na wananchi wanawachagua tena. Hili linatia uchungu. Nadhani Watanzania wanahitaji darasa la uraia (Civi nationalisn)ili waelewe power waliyonayo, haswa wakati wa uchaguzi.

  Hivi kweli mtu mwenye akili timamu unaweza kuthamanisha pea ya kanga mbele ya ujenzi wa madarasa, madawati shuleni, madawa hospitalini, utawala bora,na maendeleo ya miji yetu?

  Kwanini baada ya miaka mitano ya kwanza, ambayo pengine mgombea hakutimiza ahadi alizoatoa, wananchi wasimtie adabu na kuchagua mtu mwingine?

  La hasha, hili haliwezekani kwa sababu wetu wanazivalia njaa zao vibwebwe. Wanasau kwamba ni makosa yanayofanyika sasa ndiyo yanayoathiri kizazi kijacho.

  Natumaini kwamba mabadiliko mengi katika nchi yetu bado yapo mikononi mwa wananchi wenyewe. Tukiweza kutia adabu kidogo, na kuachana na tamaa tunaweza kuchagua viongozi ambao wataleta maendelo kwa wote, na sio kuchagua WACHUMIA TUMBO TU.

  Karumanzira

  ReplyDelete
 4. tusimlaumu mtu bali tujikague, tujibadili sisi kwanza ili tuubadili ulimwengu. wasomi na wanaoelewa mambo kama Matondo, warudi vijijini kwao na kuelimisha wananchi badala ya kuendelea kuhemea huko ughaibuni au kwenye miji mikubwa. warudi vijijini na kuishi na jamii zao ili wazielimishe

  ReplyDelete
 5. Wasomi na mnaoelewa mambo kama Matondo - mmesikia suluhisho la Kamala? Tujikagueni, tujitambueni na tujibadili sisi kwanza kisha tuache kuhemea huku ughaibuni na katika miji mikubwa. Turudini vijijini tukazielimishe na kuzipigania jamii zetu. Kamala naunga mkono suluhisho hili!

  ReplyDelete
 6. fnhz\nzngdzmzgdmz

  ReplyDelete
 7. Bwana Matondo,
  Kwanza, napenda kutoa shukurani nyingi kwa kazi nzuri unayoifanya, mfano mzuri wa kuigwa na wote ili tudumishe utamaduni wetu wa ki- Africa.

  Bwana, SIMON KITURURU, aliuliza swali?

  ALIULIZA KAMA KUNA TOFAUTI KATI YA WASUKUMA NA WANYAMWEZI.


  Kabla sijajibu swali lako kwa kirefu napenda kutoa funguo mbali mbali za swali hili ili zisaidie kuelewa kiundani.

  Mpaka sasa jina la kabila hili kubwa halijulikani ni kabila gani, lakini kutokana na ufahamu wangu, labda tuliite (BANHU) au WABANTU, watu hawa wana ongea lugha moja, tofaouti yao ni matamshi na maneno machache sana ambayo yanatokana kupanuka kwa lugha na sababu zingine ambazo labda huenda sizijulikane.
  Neno “BA” au “BAA” ni sawa na neno “WA” kwa Kiswahili,
  SUKUMA, KIYA, NG’WELI, DAKAMA,


  Neno, SUKUMA
  maana yake kaskazini—haya ni maeneo za sehemu za mwanza na nyanda zake.
  Neno, KIYA
  maana yake mashariki --- haya ni maeneo za sehemu za magu,(ntuzu) na nyanda zake(Bana ntuzu)
  Neno, DAKAMA
  maana yake kusini- haya ni maeneo yaTabora, kahama, na nyanda zake(nyamwezi) wanyamwezi(unyamwezini.
  Neno, NG’WELI
  maana yake magharibii- haya ni maeneo ya nyanda za Geita na nyanda zake.

  Tukirudi kwa kilugha, au KIBANTU kama nilivyoeleza hapo juu, inaonyesha kwamba, (Bana- sukuma au Baa- sukuma) inaleta maana nyingine kabisa ambayo ni, watu wa kaskazini, Kwa sababu hii kunakuwa hakuna kabila la wasukuma, bali watu wa sukuma, (bana sukuma, au Baa sukuma, wa kaskazini, na ukiendelea, wadakama ambao ni wanyamwezi, wana julikana kwa jina (Bana dakama au Baa dakama) maana yake ni watu wa kusini na sio kabila
  (Bana kiya au baa kiya) ni watu wa mashariki na hakuna kabila la Kiya, na Bana ng’weli au Baa ngweli) hakuna kabila hilo pia.
  Kutokana na sababu hii kuna kuwa hakuna kabila la (kisukuma, kidakama, kina ng’weli na Kiya)
  Sababu nyingine ni inayofanya yaonekane kama ni makabila tofaouti ni kutokana na kutafasiri lugha hii ninayoiita (WABANTU) katika kiswahili, na mara inapoingia katika kiswahili inaleta tafasiri nyingine kabisa na kuleta maana ya kabila tofauti kabisa, mfano kabila la kisukuma.
  Swali langu ambalo nalifanyia utafiti bado mpaka sasa, hawa watu wa pande nne ambao nimezitaja hapo juu wanaongea kabila moja, ni kabila gani? Kwa sasa jina ambalo nalitumia wakati huu wa utafiti wangu ni BANHU, ni kiwa na maana wabantu.

  Rafudhi.
  Kwa mfano, mimi mtu wa (sukuma),wa- kaskazini, nikikutana ma mtu wa Kiya mashariki, rafudhi zetu zinakuwa tofauti, katika kusalimiana hata kimaongezi, lakini tunaelewana pamoja na tofaouti ya rafudhi na matamushi.

  Salaam ni utamburisho
  salaam ni utamburisho, kwa watu wa sukuma kwa mfano,, muundo wa salaam ni utamburisho au kujitamburisha, ukisalimiana na mtu ni sawa na kujitamburisha, wewe ni nani, unatoka sehemu gani katika pande nne za za hili kabila au dunia na ukoo wako ni ukoo gani? ukimaliza kusalimiana, tayari utajua huyu ni wa ukoo gani na anatoka sehemu gani wa pande hizi nilizo zitaja, kama itakuchanganya kutomjua huyo unayesalimianaye, kwa watu wa sukuma ni kawaida kabsia kumuuliza mtu( wazenga he Bhaba au mayu?) ikiwa na maana unakoishi wapi Baba au mama, jibu kwa kawaida huufuata kama lifuatavyo, Nene baba nazenga (Ma-sukuma) mimi naishi au natokea sukuma, ikiwa na maana mimi naishi au natokea kaskazini

  Mfano.

  Mtu wa (sukuma) kaskazini akiongea, huwa anakazia sana maneno yake na kwa sauti ya juu, ukilinganisha na (wadakama) wanyamwezi, wa kusini, wao wanaongea kwa ulaini zaidi na sauti ya chini, na kama ukiwa mbali inasikika kama wimbo Fulani kwa mbali uimbwao kwa maringo na usanii.


  Jina langu naitwa: Ideka makolobeka.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU