NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, October 29, 2009

RIPOTI YA USAWA WA KIJINSIA DUNIANI - TANZANIA TUNARUDI NYUMA?

Ripoti mpya inayoonyesha usawa wa kijinsia duniani imetoka na nchi za Skandinavia bado zinaongoza (#1-Iceland, #2-Finland, #3-Norway, #4-Sweden). Kwa Afrika, Afrika Kusini (nafasi ya 6) na Lesotho (nafasi ya 10) ndizo nchi pekee za Kiafrika zilizomo katika kumi bora. Kwa Afrika Mashariki Uganda ndiyo inaongoza (nafasi ya 40), Tanzania imeshika nafasi ya 73 wakati Kenya ni ya 98. Marekani - ambako wanawake bado "wanabaguliwa" hasa katika suala la usawa wa mishahara, ajira, pamoja na mambo mengine - imeshika nafasi ya 31. Nchi ya mwisho ni Yemen (#134) ikifuatiwa na Chad (#133) na Pakistan (#132).

Baadhi ya vigezo muhimu vilivyozingatiwa katika uandaaji wa ripoti hii ni pamoja na usawa katika ushiriki wa shughuli za kiuchumi, usawa katika upatikanaji wa elimu ya viwango vyote, usawa katika upatikanaji wa huduma za afya na usawa katika ushiriki wa masuala ya kisiasa. Unaweza kuisoma ripoti kamili hapa na orodha ya nchi zote inapatikana hapa. Tovuti ya World Economic Forum ambayo huchapisha ripoti hii inapatikana hapa.

Jambo la kushangaza ni kwamba ripoti hii inaonyesha kwamba Tanzania inarudi nyuma katika juhudi zake za kuleta usawa wa kijinsia. Mwaka 2006 ilichukua nafasi ya 24, mwaka 2007 (nafasi ya 34), mwaka 2008 (nafasi ya 38) na mwaka huu (nafasi ya 73). Hii ni kweli?

Hapa chini ni Saadia Zahidi - mmojawapo wa waandaji wa ripoti hii akielezea jinsi walivyoweza kuiandaa.Swali: Nchi za Skandinavia pia ndizo zinaongoza kwa kuwa na talaka nyingi duniani. Je, kuna uhusiano kati ya usawa wa kijinsia na kiwango cha talaka au pengine hii imetokea kibahati tu?

8 comments:

 1. Personally sipendi haya mambo ya gender equality kwani ni against karibu dini zote. The Bible is very clear on this issue; and so is the Koran. I don't want mwanamke kuniambia eti yuko sawa na mimi. God never intended for it to be that way and it should be that way. Women are there basically to serve men. Adam was kind of sad and lonely and that is why Mungu akampatia MSAIDIZI. Women are there KUMSAIDIA mwanaume. Period! So forget about this equality blah blah! I am actually happy for Tanzania to be retreating on this issue.

  ReplyDelete
 2. TUNATAKA JAJI MKUU AMBAYE HANA HISTORIA YA RUSHWA NA UBINAFSI, NASIO KUCHAGUA JC KWAKUANGALIA DINI NA URAFIKI NA PIA USALAMA WA TAIFA KUNA WATU WANANDUGU ZAO AMBAO WANAWASAIDIA KULOBBY, WATANZANIA TUMECHOKA NA VIONGOZI WENYE UPENDELEO NA WENYE KUCHAKACHUA PROMOTION ZA WATU KWA KU-LOBBY.HATUTAKI UDINI WALA USWAHIBA.RAIS KUWA MACHO KTK HILI, RAIS TENDA HAKI KTK HILI WATANZANIA TUNAKUANGALIA

  ReplyDelete
 3. WATANZANIA WAWE WANACHAGUA JAJI MKUU NA SPIKA NA SIO USALAMA WA TAIFA NA RAIS HAWATENDE HAKI, TZ TUMECHOKA

  ReplyDelete
 4. TUNATaka katiba MPYa watanzania. WANAKILA MTANZANIA ASHIRIKISHWE, PIA RAIS ASIRUHUSIWE KUCHAGUA WABUNGE WA VITI MAALUM MAANA ANAPENDELEA ANAWEKA MASWAHIBA WAKE. KWA MTINDO HUU CCM INGALIE SANA INAWEZA KUPOTEZA 2015 HAtuna imani nayo wanapendelea viongozi, waziri wa nishati ajiuzulu hawezi ameshindwa kazi.

  ReplyDelete
 5. je rais anatenda haki ktk kuchagua viongoizi wa nchi naomba watu wachangie hoja

  ReplyDelete
 6. je gazei la last sundaY LA CITIZEN WATANZANIA WAMELIPOKEAJE KUHUSU USALAMA WA TAIFA KUWA NA NDUGU NA KULOBBY KWENYE JUDICIARY, MI NASEMA HAYO NI MAPUNGUFU SANA KTK TZ NNDIO MAANA VIONGOZI WA JUDICIARY WANANCHI WASHIRIKISHWE WACHAGUE KUWE NA MJADALA WA WAZI NA SIO UPENDELEO, JE HAO MAJAJI WA TATU CHANDE, LUANDA NA BWANA? WATU WA COMMENT, JE NI VIZURI KULOBBY KWENYE SENSITIVE POST KAMA HIZO,

  ReplyDelete
 7. KAMA MPENDA HAKI NA MZEE WA SIKU NYINGI MTANZANIA NADHANI SENSITIVE POSITION KAMA HZ ZA JUDICIARY, SPIKA ETC HATUTAKI WATU WALOBBY WALA KUSAIDIWA NA NDUGU AU MASWAHIBA ZAO WA USALAMA WA TAIFA, WALA HATUTAKI UDINI NA URAFIKI WALA UBAGUZI WA JINSIA HICHO NI KIUNDO MUHIMU

  ReplyDelete
 8. HATUNA IMANI NA RAIS ANAUPENDELEO KTK MAAMUZI YAKE NA UDINI ANAO. PIA JAJI RAMADHANI ANAUPENDELEO NA UKABILA

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU