NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, October 13, 2009

VIDEO MBALIMBALI ZA MWALIMU NYERERE HIZI HAPA

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 10 tangu Muasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere atutoke, hizi hapa video zake mbalimbali. Japo zina urefu tofauti tofauti na zingine hazizidi hata dakika moja, kwa pamoja zinaonyesha falsafa yake tetezi na misimamo isiyolegalega ya Mwalimu. Natoa shukrani kwa wadau mliojitolea kuzitundika video hizi katika Youtube na Google Video. Kwa hotuba zaidi za Mwalimu Nyerere tembelea http://nukta77.blogspot.com. Mungu ibariki TANZANIA!

ANAKIRI SERIKALI YAKE ILIFANYA MAKOSA


CHIMWAGA 1995 (Nukta 77)


MUUNGANO
RUSHWA


UBAGUZI WA RANGI


MAZINGIRA


WALIMU
KODI


LINALOWEZEKANA LEO LISINGOJE KESHO


MIKOPO NA MADENI


NCHI YETU HAINA DINI (UNAWEZA KUISHIA 1:25)


HOTUBA KATIKA KIINGEREZA


12 comments:

 1. Nahamu kweli na hotuba za RAIS MWINYI kwa kuwa kirahisi tu mtu unaweza kufikiri hotuba zake zote zilikuwa na neno moja tu''Ruksa!'' kwa kuwa Watanzania wengi UKIULIZA wakumbukacho kutoka kwa Rais Mwinyi ni kuwa alikuwa tu Mzee RUKSA!:-(

  ReplyDelete
 2. Hizi hotuba zimenifanya nijisikie mzalendo tena. Kama ile ya Chimwaga ingefuatwa kwa kituo mambo yangekuwa vingine hivi sasa - lakini mengi yamekwenda kinyume.
  Mungu amrehemu Mzee.

  ReplyDelete
 3. Hotuba za Mwinyi pengine zitapatika akifa. Mi naitaka laivu ile aliyozabwa kibao. Ni mtu aliyesahaulika kwa sasa

  ReplyDelete
 4. Tulikuwa na bahati kuwa na kiongozi kama huyu. Asante kwa video hizi na Mungu aibariki nchi yetu inayoliwa na walafi

  ReplyDelete
 5. Profesa hizi video hazijakuletea matatizo?Nimeona kwa Dada Subi anatishwa azitoe nahisi na vyombo vya dola kuhusu haki miliki!:-(

  ReplyDelete
 6. Haki miliki kwa video za Nyerere? Ni nani anazimiliki? Familia ya Nyerere au? Please. Mimi kama unavyoona nimezitoa mtandaoni na hasa Google. Kama wanataka wawaambie google wazitoe. Tanzania walahi hatumalizi vituko. Leo hii hotuba za maraisi wa hapa Marekani ambayo iko makini sana na haki miliki ziko wazi pale Library of Congress na kwenye maktaba mbalimbali za marais hao. Ni mali ya umma na kila mtu anaweza kuzisikiliza bure wakati wo wote. Sisi leo tunawekeana hati miliki. Kweli?

  Kuna watu maneno ya Mwalimu yanawauma, kuwachoma na kuwanyima amani kwani wamekuwa wasaliti; na sasa wanataka Watanzania wamsahau. Historia itawasuta!

  ReplyDelete
 7. Hata mimi hatimaye nimeombwa kuziondoa video hizi. Kwa vile video zote nimezitoa mtandaoni, nimewaambia watu hawa wawasiliane na Youtube na Google video waweze kuziondoa video hizi katika mitandao yao. Ni jambo la kusikitisha sana! Kwa nini kuwe na woga wa kusikiliza video zenye mawazo komavu kama hizi jamani? Tunaelekea wapi lakini sisi?

  ReplyDelete
 8. Poleni sana Matondo na Subi, mkumbuke haya ni matoke ya ubabe na ulevi wa madaraka. Ni mazoea ambayo yalikwisha jengeka kitambo.

  Ninachowaomba ni kwamba msiwe na wasiwasi hata kidogo,hizi si zama za kutishiana na kuoneshana ubabe. Hizi video kama ulivyosema Matondo ni kwamba zipo zimejaa tele kwenye youtube na google. Sasa sioni tatizo liko wapi!

  Kuhusu mojawapo ya hotuba za mwalimu, anaposema kiongozi bora lazima atoke CCM, jamani hili lina mantiki yeyote kweli, sijui lakini mimi kwa mawazo yangu binafsi sikubaliani na Marehemu baba wa taifa kwa msemo huu.

  ReplyDelete
 9. Bwana Malkiory - Asante. Hawa jamaa wapiga mikwara kuhusu video hizi mimi wala hawaninyimi usingizi. Kama nilivyosema wahangaike na Google video hizi ziondolewe mtandaoni na sijui hasa wanachojaribu kufanya ni nini.

  Nyerere kama mwanzilishi wa CCM ni wazi kwamba alikuwa anaipigia debe CCM aliposema hivyo. Kauli hii aliitoa katika mkutano mkuu wa CCM na si nadra kwa viongozi wa kisiasa kuchemsha wanapojaribu kuhamasisha wafuasi wao. Unakumbuka pia aliwahi kuwafananisha viongozi wa upinzani na mbwa na akasema hawezi kuiacha nchi yake ichukuliwe na mbwa. Pengine kwa viwango na itikadi yake aliamini kwamba hakukuwa na kiongozi nje ya CCM ambaye angeweza kuwa mwadilifu na mchapakazi ambaye angeweza kuiongoza Tanzania. Alifikiri Mkapa ndiye alikuwa bora kuliko wengine wote. Kwa uchapakazi nadhani alikuwa sahihi kwani Mkapa alifanya mambo mengi sana mazuri hasa katika nyanja ya kiuchumi. Katika uadilifu hapo sijui kwani Mkapa anaandamwa na kila aina ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kujilimbikizia mali. Ngoja tuone itakuwaje.

  Lakini pia hawa wapinzani wamekuwa "big dissapointment" na mtu ukikaa na kujiuliza kweli mtu kama Mrema au Mtikila (ambao walikuwa wanatamba sana hata kumwogopesha Mwalimu) angeweza kuwa rais mambo yangekuwaje? Naona Mwalimu hakuwaamini watu hawa na ndiyo maana alikuwa na mashaka sana na uwezo wa upinzani kuchukua madaraka. Unafikiri sasa wapinzani wanaweza kuongoza nchi vizuri na kweli kupambana na ufisadi au mambo yatakuwa yale yale?

  ReplyDelete
 10. Ndugu Matondo,

  Kusema ukweli umechanganua vizuri bila kuegemea upande mmoja nashukuru sana kwa hilo. Viongozi wengi wa upinzani wamekuwa wakifanya kazi kwa jazba na kwa kuropoka ovyo kwa muda mfupi tu, ndiyo maana hawawezi kufikia malengo yao ipasavyo. Siku hizi simsikii tena ndugu yangu Slaa akishupalia suala la ufisadi, sijui amenyamazishwa tayari!

  ReplyDelete
 11. Slaa - pengine anaogopa kukolimbwa. CCM hawachezi wakiamua. Unapewa onyo kufunga domo lako na ukiendelea kuropoka UNAKOLIMBWA! Kidumu Chama cha Mapinduzi! Halafu unaitikia huku misuli ya shingo imekusimama, povu la jazba linakutoka mdomoni huku macho yamekutoka kama chura aliyebanwa na mlango KIDUMU!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU