NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 23, 2009

WANASAIKOLOJIA: MASHOGA NA WASAGAJI HAWAWEZI KUBADILIKA AU KUBADILISHWA

Chama cha Wanasaikolojia wa Wamarakeni kimetoa tamko kikiwaonya wanasaikolojia na wafanyakazi wanaojishughulisha na afya ya akili kuacha mara moja kuwaambia wateja wao mashoga na wasagaji kwamba eti wanaweza kubadilika na kuachana kabisa na tabia hiyo. Wanasaikolojia hao wamepinga kwa kina “reparative therapy” – aina ya tiba ya kisaikolojia inayopendekezwa na kikundi kidogo cha wanasaikolojia (ambao wanaungwa mkono na wahafidhina wa Kikristo) ambao wanaamini kwamba mashoga na wasagaji wanaweza kubadilika/kubadilishwa. Kutokana na utafiti ambao wamefanya, wanasaikolojia hawa wanadai kwamba mashoga na wasagaji wakilazimishwa kubadilika wanaweza kutumbukia katika msongo wa mawazo na hata kuamua kujiua.


Dini imetajwa kuwa ndiyo chanzo kikuu cha mashoga na wasagaji kutaka kuachana na mtindo huo wa maisha ambao unapingwa sana na makanisa mengi ya kikristo. Badala ya kuwalazimisha kuachana kabisa na tabia hiyo wanasaikolojia wanapendekeza kwamba ni bora mashoga na wasagaji washauriwe kuishi maisha ya kutofanya mapenzi kabisa au kuhamia makanisa ambayo hayakatazi tabia hiyo.


Ushauri huu wa wanasaikolojia umepingwa vikali sana na Exodus International - mkusanyiko wa makanisa ya kilokole ambayo yanaamini kwamba nguvu za Yesu zinaweza kuvunja “minyororo” ya ushoga na usagaji. Raisi wa shirika hilo aitwaye Alan Chambers mwenyewe ni shahidi mzuri kwani nguvu za Yesu zilimfanya yeye mwenyewe azishinde tamaa zisizotakiwa za kufanya mapenzi ya jinsia moja alizokuwa nazo.


Tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba pamoja na athari za kimazingira, pengine ushoga na usagaji ni tabia ambayo mtu anazaliwa nayo hivyo haiwezi kubadilishwa kirahisi. Wengine wanakwenda mbali hadi kudai kwamba tabia hii itazamwe kama ugonjwa na ianze kutafutiwa tiba kama magonjwa mengine ya kawaida. Watu wa utambuzi mnasemaje kuhusu suala hili na ubadilishaji wa tabia kwa ujumla?


Kwa habari zaidi gonga hapa na unaweza kusoma maoni ya wasomaji. Ted Haggard anayerejerewa mara kwa mara na watoa maoni alikuwa ni mchungaji wa kilokole mashuhuri sana hapa Marekani na ndiye alikuwa kiongozi wa chama chao cha kitaifa kijulikanacho kama "National Association of Evangelicals". Alivuliwa madaraka yote Novemba 2006 baada ya kubainika kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na malaya mmoja wa kiume!

9 comments:

 1. Hawa watu wamelaani hawa na wataishia kuchomwa moto. Na hao wachungaji walokole wanaofanya ushoga kama huyo Haggard nao bure kabisa. Dunia imekwisha. Hawa watu inafaa wachomwe moto tu

  ReplyDelete
 2. Mimi sidhani ushoga na usagaji kama ni tabia mtu anayozaliwa nayo, isipokuwa anaharibiwa tabia akiwa bado mdogo

  ReplyDelete
 3. Hawa ni wagonjwa - wanahitaji matibabu. Tunaweza kuwahasi?

  ReplyDelete
 4. Ni chukizo kwa Bwana

  ReplyDelete
 5. We anony wa tatu. Wasagaji utawahasije? Watu wengine bwana duh! Mnakurupuka tu bila kufikiri

  ReplyDelete
 6. ACHA TUFAIDI, KWANI TUNAWAUDHI NINI?

  ReplyDelete
 7. Usagaji ni uhuru wa fikra, ni kuvunja minyororo ya fikra, usagaji hauna madhara kabisa.

  ReplyDelete
 8. Ni kweli kiasi fulani. Dini na imani pandikizi za kigeni zimeziweka jela fikra za waafrika ... zilikotoka hizo dini kuna ushoga na usagaji ... tusijifanye wakristo kuliko yesu!

  ReplyDelete
 9. Any one tusagane nitampa tamu za kimataifa plz ni tex 0776906295 any time from now asante

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU