NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, October 7, 2009

"WHAT DO YOU CONSIDER TO BE THE MOST IMPORTANT HUMAN INVENTION?"

Hili ni swali ambalo waliulizwa washiriki wa shindano moja la urembo hapa Marekani. "Mrembo" mmoja aliwavunja mbavu watazamaji alipojibu bila kusita "remote control". Mimi pia nilicheka lakini baada ya kufikiri niliona kwamba pengine sikupaswa au sikuwa na haki ya kufanya hivyo. Pengine televisheni na remote control ni vitu vya muhimu sana katika maisha na utamaduni wa "mrembo" huyu. Sisi ni nani mpaka tumcheke?

Ati, swali hilo ungeulizwa wewe ungejibu nini? Mimi ningechukua jibu la mwalimu Mkude - mwalimu wangu wa Historia wa darasa la tano pale Sima Primary School (Bariadi mjini) aliyetufundisha kwamba MOTO pengine ndiyo ugunduzi muhimu kabisa kuliko mwingine wo wote ambao umeshafanywa na binadamu. Na nisingeshangaa pia kama ningechekwa kwa kutoa jibu kama hili!

9 comments:

 1. Yeyote aliyegundua 'lugha' lazima alikuwa na akili sana! Sijui ni Adamu na Hawa (kwa misingi ya imani) au nani, mi sijui, ila yeyote aliyegundua 'lugha' ambayo ilizaa njia kadhaa za mawasiliano ya habari (ishara, picha, maandishi ya herufi katika karatasi, taipu, elektroniki, elimu, sanaa nk) huyo nataka kumpa pongezi nyingi sana! Sipati taswira ingekuwa vipi bila lugha na mawasiliano.

  ReplyDelete
 2. Uvumbuzi wa maana sana kwangu ni mavazi. Vyovyote yawavyo, ngozi, nguo na kadhalika kwa hakika, kwangu huo ulikuwa ugunduzi wa maana sana.

  Bila ugunduzi huo, sijui hali ingekuwaje!

  ReplyDelete
 3. Bwaya unachekesha. Unaogopa kutembea uchi kwa nini??????? Mimi naona nguo zilituharibia raha bure tu. Haki ya mama tungekuwa tunatembea uchi ingekuwa raha sana. Hebu fikiria jimama linakata mtako uchi barabarani. Hayo ndiyo yangekuwa maisha bwana achana na haya ya kujifichaficha. Ugunduzi bora to me ni UMEME!

  ReplyDelete
 4. Mr. Matondo kwa mtazamo wangu, uvumbuzi wa maana na ambao umechangia maendeleo ya mwanadamu ni CHOO. Can you imagine the 21st century without toilets!!!. By the way, kwa mujibU wa makadirio ya UN, watu zaidi ya billion mbili na nusu hawana vyoo. Nearly half of the World's population.

  Hello PORINI!!!!

  http://www.monstersandcritics.com/news/health/news/article_1301401.php/More_than_2_billion_people_without_toilets_UN#

  ReplyDelete
 5. labda bi kondom, au ile ya wahaya Katerero. yaani mtu anafanya ngono kwenye karatasi au mnapigana katerero unalia lia kama mbwa vile, wewe

  Kamala atwambie

  ReplyDelete
 6. jamani kuna uvumbuzi na nature (asili) vitu kama lugha ama choo (kwa maana ya haja) sio uvumbuzi. lugha inatokana na Mwenyewe. we dont do anything to have it or not. Choo ni mbwembwe za privace tu vinginevyo choo (haja) anausika nayo Muumba. kuna watu 21st century hawana choo (nyumba) lakini wanakwenda choo (haja)

  uvumbuzi wangu unaotisha kwangu ni usafiri wa anga yaani ndege

  ReplyDelete
 7. Yaani hata choo nao ni uvumbuzi? Lugha nayo ni uvumbuzi? Kuna watu wengi tu wanaishi bila vyoo. Lugha ni asili yetu na kila mnyama ana lugha kwa hivyo lugha haikuvumbuliwa na mtu. IPO TU kwa nyuki, pundamilia, sisimizi n.k.

  Mavazi pia si ugunduzi wa maana kwani kutembea uchi kuna ubaya gani? Ndiyo maana kuna nude beaches na mi binafsi ningependa kama tungekuwa tunatembea uchi ingawa ingekuwa noma kwa wenye VIBAMIA. Hata umeme is not convincing kwa sababu kuna watu wengi tu wanaishi bila umeme. May be moto is reasonable answer. Mimi ningesema pengine ugunduzi wa magurudumu (wheels invention) kwani yalimrahisishia binadamu movement na kubeba vitu na karibu njia zetu zote za usafiri zinategemea magurudumu. Huyo wa kondomu na Katerero naye, duh!

  ReplyDelete
 8. Ugunduzi wa maana ni upi? Na usio wa maana unafananaje?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU