NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, November 27, 2009

"HASSAN, PLEASE DON'T KILL ME WITH FOOD"

 • Kilichonivutia katika tangazo hili, ambalo sikumbuki nililiona kwenye blogu ya nani (pengine Othman Michuzi), ni lugha iliyotumiwa. Vipi kama mjasiriamali huyu angeandika tangazo hili kwa Kiswahili. Kulikuwa kweli na ulazima wa kutumia Kiingereza? Au pengine tangazo limelengwa kwa wateja wanaojua Kiingereza mf. watalii. Hongera mjasiriamali Hassan lakini "please don't kill me with food!"

5 comments:

 1. kwa kuwa tangazo hili liko zanzibar, nadhani miongoni mwa walengwa ni watalii. na kwa kuwa ili tangazo likumbukwe/likumbukike linatakiwa liwe na kakituko fulani ama kionjo cha namna fulani basi huyu jamaa kapatia sana.

  hiyo sentensi 'hassan please don't kill me with food' hata ingeandikwa kwa kiswahili 'hassan tafadhali usiniue kwa chakula' bado ingekuwa kituko/kionjo tosha kumkumbusha msomaji. katika hali halisi tumezoea kuona matangazo yanayosifia chakula, sio yanayo jinadi kwa uwingi wa chakula.

  ReplyDelete
 2. Hapa ndipo unapokutana na mtalii akakwambia "LUGHA YENU INAFANANA SAANA NA KIINGEREZA" maana anaweza asidhani kuwa ni English
  Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  ReplyDelete
 3. natamani kumeza ngamia angali hai jamaiii..... yaani kiswahili hatujui na kiingereza hatujui mie simo

  ReplyDelete
 4. Ukiangalia kwa makini hilo Tangazo mwandishi ajokosea Kingereza kwa bahati Mbaya, Amedhamiria kufanya hivyo. Na hiyo ni mbinu katika kuvuta hisia za watu. Hizo ni katika mbinu za matangazo ya biashara. Nimeishi Zanzibar kwa karibia mwaka mmoja. Migawaha, hoteli na sehemu nyingi za vyakula ni za wawekezaji kutoka nje.(UKITOA FORODHANI NA SEHEMU KAMA HIZO) Kuna uwezekano mkubwa sana hiyo restaurant ni ya raia toka afrika kusini. Na sidhani kama kwao lugha ya kingereza ni tatizo. Biashara mara nyingine lazima uwe mbunifu. NIMEPENDA HILO TANGAZO

  ReplyDelete
 5. Godwin Habib Meghji - Asante kwa ufafanuzi. Wakati mwingine mtu ukiona picha tu bila kujua mazingira halisi ya picha hiyo ni vigumu kufahamu hasa motisha na hata "maana halisi" ya picha hiyo. Hata mimi nilifikiri kwamba tangazo hili pengine lilikuwa limelengwa kwa watalii. Kama ni hivi basi Hassan anastahili kupongezwa kwani ametumia ubunifu wa hali ya juu katika ili kuvutia wateja. Ni wazi kwamba ukiliona tangazo hili utalisoma mara mbili mbili - na kabla hujajua kinachoendelea si ajabu ukajikuta ukiomba msamaha "Hassan, please don't kill me with food!"

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU