NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, November 29, 2009

HONGERA MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

Mh. John Pombe Magufuli akitunukiwa shahada ya uzamifu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Balozi Fulgence M. Kazaura.

Mama yake alikuweko kumshangilia mwana aliyefanikiwa kukifikia kilele.
 • John Pombe Magufuli (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), ni mmojawapo kati ya mawaziri vijana, makini na wachapakazi sana katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Jana alitunukiwa shahada ya uzamifu (PhD) ya Kemia katika mahafali ya 39 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
 • Mh. Magufuli alitunukiwa shahada hiyo baada ya kufanya utafiti, kuandika na kuitetea tasnifu yake juu ya matumizi ya maganda ya korosho katika kuzuia kutu.
 • Sote tunajua jinsi shahada za uzamifu zilivyo ngumu na zinavyochukua muda mrefu. Pamoja na majukumu yake mengi ya kuongoza wizara muhimu ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, bado alipata muda wa kufanya utafiti, kuandika tasnifu yake na hatimaye kuitetea kwa mafanikio.

 • Kwa kutambua umuhimu wa elimu ya juu, na bila kuamua kupita njia za mkato kama wenzake hawa, tunapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Tunategemea kwamba Ph.D hii imemwongezea maarifa mapya na kwamba ataendelea kufanya kazi yake kwa ufanisi na umakinifu zaidi. Hongera Mh. Dkt. John Pombe Magufuli!

7 comments:

 1. Ni mfano wa kuigwa. Hongera Mheshimiwa!

  ReplyDelete
 2. hakika huyu baba ana sifa chanya nyingi. katika watu ambao hata kama ungetaja kwa kumwita dokta watu wasingejiuliza maswali mengi huyu ni mmojawapo. mbali na taaluma huyu baba ni mtanzania mwenye uchungu kuliko hayo majangili mengine

  ReplyDelete
 3. Mheshimiwa, daktari, Waziri, Baba n.k John P Magufuli hongera sana, sasa wabane zaidi wanaotumia nyavu ndogo na mabovu katika uvuvi. Pia kumbuka kuna Mpwapwa breed hamna wa kuiendeleza

  ReplyDelete
 4. Nami nampa pongezi nyingi sana baba huyu. Utafiti wake alioufanya nimeupenda, na hapo naweza sema elimu ya Kemia imepiga hatua kwani knowledge mpya kabisa ameleta Mh Waziri Dkt Magufuli.

  ReplyDelete
 5. Hongera Mheshimiwa Magufuli. Waache hao walionunua Phd FAKE wahangaike. Chapa kazi sasa

  ReplyDelete
 6. Hongera kwa kazi hiyo pevu. Lakini hana sifa hizo chanya. Waulize wanaomjua. Yeye ndiye kiini cha uuzwaji wa nyumba za serikali. Kuna ufisadi zaidi ya huu. Si msafi hata kidogo. Tafakari.

  ReplyDelete
 7. Hongera Dakta Magufuli, mwalimu wa siku nyingi na mwanasiasa makini.

  Binafsi nimeupenda utafiti alioufanya. Ni mfano wa kuigwa.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU