NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, November 2, 2009

INGEKUWA TANZANIA HII TUNGESEMA NI USHIRIKINA!

=> Tazama vizuri mkono wa kushoto - kuna popo!
 • Jana hapa Marekani ilikuwa ni sikukuu ya Halloween- sikukuu ya kipagani iambatanayo na mambo ya kishetani shetani japo inasherehekewa pia na "Wakristo".
 • Basi jana katika mchezo wa mpira wa kikapu wa NBA kati ya San Antonio Spurs na Sacramento Kings kilitokea kisa cha kushangaza.
 • Mchezo ulipoanza, na bila kutegemea, alitokea popo ambaye alianza kukatiza uwanja kutokea goli hadi goli. Kidogo kulitokea mtafaruku huku wachezaji wakijaribu kumkwepa popo huyo. Mchezo ulisimamishwa kwa muda.
 • Popo huyo alipokuwa akijaribu kukatiza tena uwanjani, Manu Ginobili, mchezaji wa San Antonio Spurs kwa kasi ya kutisha alimtandika kwa kutumia mkono wake wa kushoto.
 • Popo alidondoka chini, Manu Ginobili akamwokota na kumpatia mfanyakazi aliyekuweko, akatia "sanitizer" mikononi na gemu likaendelea.
 • Matokeo: San Antonio Spurs 113, Sacramento Kings 94.
 • Ingekuwa nyumbani si ajabu hii ingesemwa kuwa ni kazi ya "kamati ya wazee" kumbe...
 • Tazama video hapa chini kumwona Ginobili akimfanyizia popo huyu mwenye bahati mbaya.
 • Baadaye alipata chanjo ya kuzuia vijidudu na aliwaonya watoto wasijaribu kuwaua popo kama alivyofanya kwani inaweza kuwa ni hatari.

3 comments:

 1. Sasa tunajuaje kwamba huu siyo ushirikina? Wewe unafikiri wazungu hawajui ushirikina. Kama hujui wazungu ndiyo wachawi namba wani na si ajabu hapa mkono wa mtu umetembea. Ndiyo maana they won. Acheni kuwaogopa whites. They are just like us!

  ReplyDelete
 2. duuh hiyo siku ikiadhimishwa bongo watu watalogana kwelikweli...

  ReplyDelete
 3. Ha ha haaa, ingekuwa gumzo la mwaka

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU