NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, November 5, 2009

KISWAHILI KIPYA - KUFULIA NI NINI?

Wakati mwingine sisi tulioko ughaibuni Kiswahili kipya kinatupiga chenga. Mnamaanisha nini siku hizi mnaposema eti Kanumba amefulia? Natumaini si tusi (la nguoni) au neno baya!

7 comments:

 1. Sijui kama tutajibiwa ama nasi tutaambiwa kuwa TUNAULIZA KWA KUWA TUMEFULIA?
  Hahahahaaaaaaaaaaa.
  Tusubiri

  ReplyDelete
 2. kufulia ni neno linalotumika kumaanisha, 'ukata' au 'kuishiwa' au 'kutokuwa na mshiko' au 'kuwa bila ndururu' au wakati mwingine ukizungumza na watu ukasema jambo lisiloendana na mada au lisilotela maana wala mantiki, utaambiwa, nyamaza na wewe 'umefulia' au kama 'umefulia' si ukae kimya? kwa maana ya kuwa off-point au kuongea kisichoeleweka. Kwa mfano, Yanga walifulia kwa Simba (walifungwa na kupoteza mechi) au Aliyekuwa raisi wa Marekani bwana Bush alifulia Iraki (alikosea kwa kuanzisha vita ile), au, doh, matokeo ya pepa nimefulia kichizi mwanangu (mtihani nimefeli sana rafiki yangu).

  ReplyDelete
 3. Mzee wa Changamoto - natumaini sisi wanablogu hatujafulia, au pengine tunafulia mara moja moja. Lugha ni kitu cha kushangaza kweli!

  Dada Subi - asante sana kwa ufafanuzi wa kina. Sasa sijui kama nimefulia ama la. Safi sana wanablogu wenzangu. Sisi sasa ni ndugu! Tuangalie tu tusije tukafulia!

  ReplyDelete
 4. nyongeza kwa subi. ni kweli maana ni kuishiwa. neno hili limepigiwa baragumu na kundi la futuhi (comedy) la 'orijino komedi' la tbc 1. (kwa wasiojua neno 'futuhi' ni kiswahili cha comedy. simaanishi kikundi cha star tv kinachotumia neno 'futuhi' kama jina lao).

  kufulia ni kuishiwa hasa kunakotokana na ujinga wa kutotumia rasilimali ulizofahamika kuwa nazo awali. neno lingine linalokaribiana kimaana tunawezasema ni 'kutapanya'. yaani ufukara unaokuja baada ya kutapanya ama kwa kukosa mbinu sahiha za ujasiamali. pia kutokana na ukimwaga (kiswahili cha zamani kidogo cha ukimwaga, au siyo?).

  Pengine watu hawa hapa chini wanaweza kupeleka maana yangu vema. hawa wamewahi 'kutangazwa' kufulia na kikundi cha futuhi cha 'orijino komedi'

  1. augustine mrema
  2. edibily lunyamila
  3. muumin mwinjuma (huyu alipinga kufulia)

  ReplyDelete
 5. Sawa kabisa walivyoeleza da' Subi na kaka Mwaipopo. kwa kuongezea tu ni kuwa neno hili hutumika kwa mtu ambaye alikuwa na hali fulani, madhalan kipato cha chuu au umaarufu halafu kwa sababu fulani hali hiyo ikatoweka ghafla. Kwa msemo mwingine tunasema "kupigika" au "choka mbaya" !

  ReplyDelete
 6. Prof: Unaogopa kufulia?

  ReplyDelete
 7. Nyote asanteni tena kwa ufafanuzi wenu mzuri wa hili neno kufulia. Mmelifafanua vizuri na sasa nimeliewe vyema. Hata wataalamu wa vipindi vile vya kufafanua maneno ya Kiswahili katika redio sidhani kama wangefafanua vizuri namna hii mbali na kufulia tu kwa kusema kwamba hiki ni Kiswahili cha mtaani kisicho na maana. Asanteni sana!

  Ananony. wa mwisho - kutokana na fafanuzi zilizotolewa hapa nadhani kila binadamu katika kipindi fulani cha maisha yake huwa anafulia. Kama ni hivi basi nadhani kufulia kumefungamanishwa na hali halisi ya maisha yetu tunayoishi - kuna kupanda na kushuka a.k.a kufulia. Itazame historia na itakupa msururu mrefu wa watu wa kila aina waliopanda mpaka kileleni kabisa na halafu wakafulia. Kwa hivyo siogopi kufulia (na sijui pengine nimefulia hata sasa hivi) kwani ni hali halisi na ya kutegemewa katika maisha yetu. Wewe unafikiri hutafulia/hujafulia?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU