NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, November 19, 2009

KWA UFISADI KAMA HUU AFRIKA TUTAENDELEA???

Jana (Novemba 17, 2009) kulikuwa na makala nzuri katika gazeti la New York Times juu ya ufisadi wa Teodoro Nguema Obiang ambaye ni mtoto wa raisi wa miaka mingi wa Equatorial Guinea - Teodoro Obiang Nguema Mbasogo. Inaaminika kwamba Teodoro Nguema Obiang ambaye pia ni waziri wa misitu na kilimo wa Equatoria Guinea ndiye anaandaliwa kuchukua madaraka ya uraisi baada ya baba yake kuachia madaraka. Mambo chomozi katika makala hiyo ni haya:


 • Equatorial Guinea inashika nafasi ya tatu katika utoaji wa mafuta barani Afrika ikitanguliwa na Naijeria na Angola. Mwaka 2007 pekee, Equatorial Guinea ilijipatia dola bilioni 4.8 kutokana na mauzo yake ya mafuta.

 • Paradoksi ni kwamba zaidi ya robo tatu ya wananchi wa Equatoria Guinea ni masikini hohehahe kabisa wanaoishi kwa pato la chini ya dola 1 kwa siku!

 • Wakati huo huo, mtoto huyu wa rais ambaye bado ana miaka 38 tu ni tajiri wa kutupwa na ni wazi kwamba utajiri huo ameupata kwa kupitia rushwa na ufisadi. Mfano mali zake za kifahari hapa Marekani – bila kutaja akaunti zake za Uswisi na utajiri wake mwingine ni kama ifuatavyo:

(1) Jumba la milioni 35 katika pwani ya Malibu California

(2) Ndege yake binafsi – dola 38,000,000

(3) Magari manne aina ya Ferrari – dola 1,000,000

(4) Rolls-Royce mbili – dola 700,000

(5) Maybachs mbili – dola 700,000

(6) Bentley Arnage moja – dola 240,000


(7) Huja kupumzika Marekani zaidi ya mara tatu kila mwaka na kila anapokuja huja na pesa taslimu zaidi ya dola 1,000,000 tena bila kuwajulisha watu wa uhamiaji. Hili ni kosa la jinai kwa sheria za Marekani lakni kwa vile Marekani ndiye mnunuzi mkuu wa mafuta ya Equatorial Guinea, maofisa wa uhamiaji humfumbia macho.


Kwa hivyo:


(8) Ukiwa na mafuta, Marekani itakuruhusu ufanye cho chote unachotaka – hata kama ni kuvunja sheria zake! Ukijifanya jeuri wanakuja kuchukua mafuta yako kwa nguvu (muulize Saddam Hussein atakwambia)

 • Kwa ufisadi huu kweli, Afrika tutaweza kuendelea? Kinachoumiza moyo ni kuona kwamba umma wa Afrika, pengine kutokana na ukosefu wa elimu ya kweli pamoja na umasikini bado umelala na unaruhusu raslimali na utajiri wake uliopindukia kimo kufaidiwa na akina Teodoro Nguema Obiang wachache. Inasikitisha sana! Tazama hii clip hapa chini juu ya “vichaa wa Afrika"


3 comments:

 1. ni maisha yale yale ya kujitafuta kwenye miili utadhani miili ina umuhimu kuliko sisi halis na utu wetu. tuazdi kufanya mambo ya ajabu na kuzalisha nguvu hasi nyingi zaidi (dhambi?) bila kujua. bora hawa wangejua juu ya Karma (law of action and reaction)

  sijui kwanini hatuoni faida ya kumpenda jirani yetu kama alivyoagiza yula mfa msalabani

  ReplyDelete
 2. Na hapo mmoja wa raia wa nchi hiyo akijaribu tu kuongea basi utasikia kawekwa kizuizini

  ReplyDelete
 3. Equatorial Guinea wanahitaji wananchi wenye moyo ili kufanya mapinduzi (REVOLUTION). Wakiendelea kukaa kimya kama MAKONDOO watendelea na umaskini mpaka karne ya 22.

  -Too bad that our continent is still producing "men without chests."

  -IS OUR SOCIETY IN DANGER OF COLLAPSE BECAUSE OF A "ROT FROM WITHIN"? By Clive S. Lewis.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU