NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, November 12, 2009

LIBENEKE LA MASHINDANO YA UREMBO - WANAWAKE TIPWATIPWA WAJIBU MAPIGO!!!


 • Ni wazi kwamba hivi sasa mashindano ya urembo ni biashara kubwa sana ndiyo maana yametanda kila kona kuanzia taifa, mikoa, wilaya, tarafa, kata na pengine muda si mrefu yatafika ngazi ya vijiji na hata familia!. Japo mashindano haya yanajumuisha watu wa kila aina wakiwemo watoto wadogo (bofya hapa), kwa kiasi kikubwa vigezo vinavyotumika ni vile vya Kimagharibi ambako ili mwanamke awe "mrembo" ni lazima awe mwembamba hasa hata kama ni ule wembamba wa kiutapiamlo!
 • Kimsingi hii ni kinyume na dhana ya jumla ya uzuri tuliyokuwa nayo sisi Waafrika ambapo mwanamke wa kwelikweli aliyekuwa akisifika alikuwa ni yule tipwatipwa, mwenye umbo mkatiko (vijana wanaita umbo namba 8), matako makubwa na miguu minene iliyosanifiwa (wenyewe wakiita miguu ya bia a.k.a usafiri wa uhakika!).
 • Wembamba kwetu sisi ulikuwa ni dalili ya maradhi na ukosefu wa lishe bora (unamkumbuka Clementine katika diwani ya Wimbo wa Lawino?). Wakati huu tulikuwa bado hatujajiingiza sana katika maisha ya deko na kula vyakula vya "kisasa" vilivyokuzwa kisayansi na kushindiliwa makemikali na sumu za kila aina. Kwa hivyo kansa na magonjwa mengine tunayoambiwa sasa kwamba yanasababishwa na unene hayakuwa tatizo sana kwetu. Sasa mambo yamebadilika! Soma makala ya Profesa Mbele kuhusu suala hili hapa.
 • Inavyoonekana wanawake tipwatipwa, baada ya kuona kuwa wanapigwa dafrau, nao wameamka na kuanza kufanya mashindano yao ya "urembo" pamoja na kufungua vilabu vyao wenyewe (gonga hapa na hapa). Hapa chini ni picha chache za mashindano ya aina hii ambayo nimeambiwa kwamba yalifanyika kule California na kwamba baadhi ya washiriki walikuwa ni Watanzania! (Mdau aitwaye Kessy anayeishi Las Vegas alihudhuria onyesho hili na ndiye ameniletea picha hizi - Asante Bwana Kessy)
 • Tanzania mashindano kama haya yapo? Kama yapo yanatazamwaje na wanajamii? Kweli Vodacom watakubali kumwaga mamilioni yao kwa mashindano kama haya?

Mshereheshaji
Baadhi ya Washiriki

Mchuano wenyewe
  • Bwana Kessy ameleta link ya video hii ya youtube na kusema kwamba (nanukuu) "mwanamke true wa Kiafrika anapaswa kuwa hivi na siyo skiny kama hawa mamiss Tanzania" Kazi kwenu wadau. Mimi ni mjumbe tu na mjumbe daima huwa hauwawigwi ati!

  8 comments:

  1. Haya mashindano yakitia timu Rwanda, nafikiri majaji watashindwa kuamua, ha ha haa

   ReplyDelete
  2. Chib sema. Kwani Rwanda kuna nini mpaka majaji washindwe kuamua??? Just curious.

   ReplyDelete
  3. Chib is right. Rwandese women are the MOST beautiful women in the world, period! If you have a heart condition DON'T visit Rwanda. You will die!

   ReplyDelete
  4. I have seen some! oooh my God. sijui Chib anakaaje huko tena eti alone!

   ReplyDelete
  5. Acheni kasumba zenu hizo za kusifia wageni na kuzarau wa kwenu,nani kakuambia Tz hakuna warembo Chibi?hao wanyarwanda wenu mbona basi hawajawahi kuchukua miss world? hawajawahi hata kufikia hatua waliyofikia ma miss wetu Tz tuliwahi kuchukua miss Africa nani anabisha?Sifia chako kwanza,Inaelekea uliwahi kupata girl friend wa kinyarwanda wewe hahahaaaaa!!bisha?

   ReplyDelete
  6. Tanzania hakuna wanawake wazuri na hawafikii hata nusu ya Wanyarwanda. Nenda Kigali ukaone. Mara yangu ya kwanza kwenda Rwanda kidogo nipate mshtuko wa moyo. Kuna matako huko sijaona kwingineko Afrika except South Africa. Tofauti ya Wanyarwanda ni kwamba ni warefu na wamekatika kiunoni na wana miguu mizuri sana halafu weusi wao ni ule wa hariri. They are the most beautiful women in Africa without a doubt.

   Mdau Alex in Kigali!

   ReplyDelete
  7. Jamani, kwani uzuri ni nini?????

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU