NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, November 11, 2009

"MSWAHILI" ANAPOFURAHIA MKE WAKE KUPATA BWANA WA KIZUNGU!

 • Katuni hii imenikumbusha mambo mawili: Kwanza suala la unene. Kitamaduni unene ulikuwa ni jambo la kujivunia na sidhani kama ulikuwa na madhara makubwa kama tunavyoambiwa sasa. Kila mtu alikuwa na ndoto ya kunenepa na vitambi vilionekana kama ishara ya kufanikiwa kimaisha. Watu walikuwa wanafanya kazi sana na tulikuwa tunakula vyakula vya kiasili - siyo kama sasa ambapo utandawazi umetuvuruga kabisa. Soma hapa, hapa na hapa kuhusu hili suala.
 • Pili: tabia yetu ya kutukuza wazungu, uzungu na vitu vyao vyote. Japo utawala wao uliisha, kisaikolojia jamaa bado wametuminya kweli kweli! Niliwahi kulalamika kuhusu suala hili hapa. Natumaini hatutafikia hii hatua aliyofikia huyu "Mswahili" mwenzetu kwenye katuni.

3 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!November 12, 2009 at 3:12 PM

  Kaka Masangu, hapo ni ankara a.k.a ze vijisenti vinamzingua huyo...lol

  kuhusu unene siwezi sema kwani nami ni munono kama wasemavyo wakenya....lol

  ReplyDelete
 2. Huyu sio mzima hata kidogo, hata kama unatamaa na hela kiasi gani hii haiwezi tokea

  ReplyDelete
 3. Pesa zilimuua Yesu, kwa hiyo ina maana watu wanaolewa na mzungu kwa kufuata pesa. Basi hilo si penzi tena. Na pia watu wengi sana wanadanganyika au amini kuwa wazungu ni watu wenye uwezo sana. Lakini wangejua, wangapi wameolewa na yakawashinda. Mmmm sisemi sana.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU