NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, November 25, 2009

NAKUMBUKA SIKU NILIYOPANDA BOEING 747 KWA MARA YA KWANZA

 • Ukiniuliza swali ni uvumbuzi gani wa mwanadamu unaonivutia sana jibu langu la moja kwa moja litakuwa ni “jetliners”. Kila mara ninapoingia katika dege na halafu linaruka bila matatizo na kubakia angani kwa masaa zaidi ya 10 likiwa limejaza watu na mizigo huwa namvulia kofia binadamu kwa ugunduzi wake huu maridadi ajabu! Na mara yangu ya kwanza kusafiri na Boeing 747 nilishangaa mno (pengine kutokana na ushamba wa Kisukuma!)
 • Nilipoingia katika dege la Boeing 747 lililokuwa linamilikiwa na shirika la Alliance Airlines (Afrika Kusini) nilishangaa sana kwani dege lilikuwa limejaza wasafiri na mizigo tele mpaka nikakosa mahali pa kuweka begi langu nililokuwa nimeingia nalo.
 • Baada ya kuangalia umati ule wa watu nilikuwa na wasiwasi sana kama dege lile kweli lingeweza kuruka na kukaa angani masaa manane hadi tisa mpaka tufike London. Lakini kweli tena bila matatizo dege hilo lilijikongoja na muda si muda likawa limeruka na kweli baada ya masaa tisa angani tulifika London.
 • Kuanzia siku ile ndege imegeuka kuwa jambo linivutialo sana na nimeshasoma vitabu vingi na magazeti juu ya Historia ya juhudi za binadamu kujaribu kuruka, aina mbalimbali za ndege za kiraia, ajali kubwa za ndege, wagunduzi mashuhuri n.k. Wewe ni ugunduzi gani wa binadamu unaokuvutia zaidi?
 • Na mpaka leo kila mara ninapoingia katika dege daima huwa sikomi kushangazwa na teknolojia hii. Natumaini kwamba siku moja itawezekana kutengeneza madege ambayo hayatingishiki wala kusukwasukwa huku na huko hali ya hewa inapochafuka huko mawinguni. Huwa sipendi dege likianza kufanya hivi.

8 comments:

 1. Hata mimi midege mikubwa hunishangaza!

  ReplyDelete
 2. sijapanda hiyo midege, zamani nilishangazwa na basi zenye vyoo na AC baadaye nikaona ni za kawaida tu!

  sasa nashangazwa na ugunduzi wa tahajudi au meditation. unanisisimua na kunishangaza ni jinsi gali watu waligundua kitendo hiki muhimu

  ReplyDelete
 3. Ni kweli mtu huwezi kuamini kwangu yalikuwa ni maajabu kabisa. Na bado ni maajabu.

  ReplyDelete
 4. unapenda ndege?...dah sijui mara ya ngapi tokea nimepanda ndege ila mpaka nazeeka nitakuwa na "fear factor" fulani...ila it is a great invention...la sivyo tungetembea...or treni...or basi...n imagine how long will that take...

  ReplyDelete
 5. Kamala, safari yako ya Sweden lini? Madege hayaepukiki au utakwenda kwa meli?

  Nadhani siku moja utauona ugunduzi wa tahajudi au meditation kuwa ni wa kawaida pia!

  Candy - hata mimi naogopa sana ndege na wakati huo huo navutiwa na ugunduzi wenyewe. Ndiyo maana nikasema siku wakiweza kutengeneza midege ambayo haitingishiki itakuwa poa sana.

  Kuna kipindi tulikumbwa na "turbulence" katikati ya Atlantic Ocean basi mioyo ilitupapatika. Mdege ulikuwa unatikisika mpaka unazisikia injini zinatoa milio ya ajabu ajabu. Watu walianza kusali na nadhani sala zao zilisikiwa kwani baada ya muda hali ilikuwa shwari ingawa hakuna mtu aliyemsemesha mwenzake kwa muda.

  ReplyDelete
 6. Ahaa. Thanx Candy. That makes two of us. Actually 3 na kaka Matondo.
  Ndege kitu cha kushangaza saana na mara zote huwa nawauliza wanaozirusha kama huwa hazichoki. Japo naogopa lakini ndizo ziniwekazo mjini kwani ndio kazi ilipo kutengeneza spare parts zao.
  Mara yangu ya kwanza kutembea kuelekea kwenye ndege mwaka 1993(maana mara zote nilizopanda awali zilikuwa za kupelekwa) nilikuwa na fikra kinzani. Nilikuwa natamani kuweka rekodi ya kukumbuka kupanda ndege lakini sikujua inakuwaje huko juu.
  Tulifika DIA (sasa Mwl Nyerere Int'l Airport) kuelekea Mtwara na tukiwa uwanjani kulee juu kusubiri muda wetu, mara ndege la jeshi likagoma kuchomoa matairi, hivyo ilibidi walizungushe mpaka mafuta yaishe kisha waliangushe pembezoni mwa uwanja. CAN YOU IMAGINE UNA KALE KA-UOGA KA AWALI KISHA UNAONA HILO???
  Magari ya kubeba wagonjwa yakaja na kuwanusuru na muda mfupi baadae tunaambia "twiga mnyonge" (Air Tanzania) ameshapaki akitusubiri.
  Kama babangu asingekuwa mkali na kama asingeniangalia lile jicho lilioashiria "kitakachofuata ni kichapo" basi wasingeniona ndani ya ndege siku hiyo. Lakini nililipanda na sina ninalokumbuka. Najua kama ningekuwa nimefikisha umri wa kulewa ningechapa kilevi nisi-feel chochote mpaka nashuka.

  ILA japo si mpenzi wa ku-fly, bado nafuatilia saana mambo ya aviation hasa NASA na programs zao za SPACE SHUTTLE. Ziko veeery interesting na nazipenda saaana. Calculation za namna wanavyokwenda kwenye international space, kazi zao, kulivyo, wanavyo-recycle mikojo kupata maji na namna wanavyoishi kule kusiko na gravitational force (maana si mwajua lazima kuwe na watu kwenye space station)
  Tena Space shuttle itatua kesho nami naisubiri kuishuhudia.
  NAPENDA SAAANA MAMBO YA AVIATION LAKINI SIPENDI KUWA MMOJA WAO.
  Lol

  ReplyDelete
 7. Profesa Matondo, umenifurahisha kweli, lakini ndiyo maana ya kuwa na curious mind. Nami huwa najiuliza maswali kama ya kwako kila nipandapo KLM toka Amsterdam kwenda TZ wakati limesheheni mamia kadhaa ya watalii, kwakweli ninakosa jibu la namna binadamu alivyoanza kupata wazo la ketengeneza chombo kama hiki ambacho hudumu angani kwa masaa takribani 9 bila kusimama, . Nabakia kusema mzungu amejaliwa au kubarikiwa.........

  ReplyDelete
 8. Bonsoir dsl mais je n'arrive pas à te lire bonsoir

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU