NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, November 28, 2009

NIMEWAKUMBUKA SATO WA MWANZA

Picha hii kutoka kwa Mjengwa imenikumbusha sato wa Mwanza. Hapo unanunua wawili, kitunguu kimoja na nyanya nne tano hivi, unakipanda kilima cha Bugando kupitia pale shule ya Sekondari ya Mwanza halafu unajitengenezea kachumbari yako safi. Ukiongezea chumvi na pilipili kidogo pembeni basi mlima wa ugali unateketea bila wasiwasi. Safi sana!

5 comments:

 1. Mhu umenikumbusha mbali sana, leo lazima nitengeneze hii menu, ingawa sato ntakao kula ni toka phillipens, lakini wahenga walisema ukikosa la mama hata la ng'ombe lafaa

  ReplyDelete
 2. Mi mate yamenijaa mdomoni,sato wa Mwanza bwana watamu,basi acha na mimi nile ugali kwa ramani ya sato,maana sina ubavu wa kuwapata.

  ReplyDelete
 3. Sasa hivi wamepungua kidogo upatikanaji wake baada ya wavuvi haramu wanaotumia nyavu ndogo kubanwa, hongera Magufuli

  ReplyDelete
 4. kuleni tu wanaume. wale wachimba madini wa Geita na north mara wanamwaga sumu za cyanide, mercury na nyinginezo ziwani, harafu nyie mnabugia. kwa ufupi matondo umemiss SUMU, siyasemi kwa u-vegeterian bali ni uhalisia

  ReplyDelete
 5. Kamala - sikujua kama uchafuzi wa mazingira unaofanywa na hawa wawekezaji wa kigeni umefikia kiasi cha kuathiri samaki wa ziwa kubwa kama hilo.

  Hata wewe kuwa mwangalifu na hizo mboga mboga unazokula. Zinaweza pia kuwa zimeathiriwa na maji ya sumu na madawa mengineyo.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU