NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, November 9, 2009

NJIA MBILI BORA ZA KUMSHINDA MPINZANI WAKO KATIKA UGOMVI WA NGUMI

(1) Usipigane - hii ndiyo njia bora kuliko zote!

(2) Kama ni lazima upigane, zingatia siri hii. Ukiona unazidiwa - mtegee mpinzani wako anaporusha ngumi na wewe rusha hapo hapo tena kwa haraka ya kufumba na kufumbua. Hii ina matokeo matatu: Kwanza ngumi yake inaweza kukupata kwanza na kukufletisha kabla ya kwako haijatua usoni mwake (epuka hili lisitokee). Pili - ngumi yako inaweza kumpata kwanza na kumfletisha kabla ya kwake haijatua kidevuni mwako (hakikisha hili linatokea). Tatu - ngumi yake na yako zinaweka kutua kwa wakati mmoja na wote mkafletishana (na hii siyo mbaya sana). Nilifundishwa siri hii zamani sana. Tazama video hapa chini (dakika 1:18).

4 comments:

 1. Safi sana mkuu hii nimeipenda. Nadhani hata hao wazungu wabaguzi ukikumbana nao chooni unawatandika tu. Manake kuna wakati inakubidi tu uwe mgomvi hata kama ulikuwa hutaki unajikuta tayari. Sheria zipo lakini ni kwa maslahi ya wachache.

  ReplyDelete
 2. Hii imenichekesha sana......

  ReplyDelete
 3. binadamu wengine bwana. na tuamini mna akili nyingi na labda ya kutosha kwa kutufundiha jinsi ya kutwangana.


  nimeyasoma na kuyaacha hapa hapa na kamwe sitafuata ushari hata mmoja. Matonodo ukiwa mkristo; hujui ya kuwa imeandikwa kuwa akupigaye kushoto mgeuzie kulia???
  iweje unatufundisha kulipiza? UTAENDA MOTONI USIPOTUBU nakwambia

  ReplyDelete
 4. Kamala - acha kunitisha na moto bwana. Moto wa nini na wewe huamini katika moto? Na hiyo kugeuza shavu jingine ukitandikwa lile jingine usiichukulie kisisisi. Biblia hiyo hiyo pia inatufundisha kujitetea tunapoonewa na kwa hivyo kumtaimu adui yako anaporusha ngumi yake na wewe ukaungurumisha ya kwako si kosa. Kumbuka pia kwamba njia bora kabisa ya kumshinda adui yako ni KUTOPIGANA naye!

  Post hii ni UCHESHI/UTANI tu! Nilipowaona hawa wapiganaji jinsi walivyofletishana nilikumbuka jinsi jamaa mmoja alivyokuwa akitwambia zamani sana wakati ule tukiwa tunapigana kugombea ng'ombe wa nani wanywe maji kwanza wakati tukichunga. Maisha!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU