NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, November 25, 2009

POLISI AFUKUZWA KAZI KWA KUTOLIPIA VIJIKO VIWILI VYA "ICE CREAM"

 • Hawa jamaa kweli wako siriazi na mambo ya rushwa na upendeleo. Polisi mmoja hapa Florida amefukuzwa kazi kwa kupewa vijiko viwili vya "Ice Cream" na kundoka bila kuvilipia, jambo ambalo liliashiria utumiaji vibaya wa madaraka yake.
 • Polisi huyo alikuta duka linalouza ice cream limefungwa lakini alimshawishi muuzaji aliyekuwemo ampatie vijiko viwili. Baada ya kupata ice cream yake polisi huyo alitoka nje na kwenda kufaidi ice cream hiyo ya bure na mpenzi wake aliyekuweko nje ya duka.
 • Iligundulika baadaye kwamba polisi huyu huyu pia aliwahi kula na kuondoka bila kulipa katika hoteli moja. Katika mkasa huu, polisi mwenzake ilibidi amlipie. Mkasa huu unapatikana hapa.
 • Vipi tungekuwa na sheria na kanuni kali kama hizi dhidi ya rushwa, upendeleo, na matumizi mabaya ya madaraka; na tukazitekeleza?

3 comments:

 1. Nanukuu "Vipi tungekuwa na sheria na kanuni kali kama hizi dhidi ya rushwa, upendeleo, na matumizi mabaya ya madaraka; na tukazitekeleza?" Mwisho wa kunuuu, jibu lake ni kwamba tungekuwa /tungefika mahali pazuri sana.

  ReplyDelete
 2. Nyie, acha kuiga. tanzania tuna uhaba mkuuubwa wa mapolisi, sasa tukiwaiga hawa jamaa si tutabaki bila polisi?

  harafu kweu mishahara kiduchu na wanaishi vibandani hawa jamaa, sasa bila kuwa wajanja unafikiri wataishije. tusiige jamani

  ReplyDelete
 3. Rushwa sisi ipo ndani ya damu. Mbona hata mawaziri wenye kila kitu bado wanakula rushwa? Hivyo idea kwamba eti kuwapa mishahara mizuri ndiyo wataacha rushwa haitasaidia pengine ndiyo wataanza kushindana kama wanavyofanya mawaziri na watu wengine wenye uwezo tunaowaona. Bribe is our way of life whether poor or rich. So stop complaining!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU