NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, November 3, 2009

PROFESA/MKUU WA IDARA AACHIA NGAZI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAKE

 • Profesa mmoja mwanaume ambaye pia alikuwa mkuu wa idara mojawapo hapa chuoni ameachia ngazi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi wake.
 • Inasemekana kwamba alikuwa nao wengi kwa mpigo na mpaka sasa wasichana watatu wameandika barua kuelezea jinsi walivyolaghaiwa naye.
 • Alikuwa akiwatumia wanafunzi wake picha zake za uchi kwa kutumia simu yake ya mkononi.
 • Alikuwa akilipwa dola 106,000 kwa mwaka.
 • Wanafunzi wake wa zamani wamtetea na kusema kwamba ni mmojawapo wa maprofesa wazuri sana - ingawa alipenda mno kuongelea mambo yake binafsi pamoja na familia yake.
 • Swali: Vipi tungekuwa na kasheria kama haka kule nyumbani? Mnakumbuka yale mambo ya mabinti "kushikwa" na hata "kudisco" wakimzembea Profesa? (sijui sasa kama mambo haya bado yapo yanatendeka au pengine utandawazi umeyamaliza!)
 • Kwa habari zaidi kuhusu hii ishu soma hapa na hapa

7 comments:

 1. Hii maneno ingawaje bado ipoipo lakini nadhani umashuhuri/umaarufu wake umedidimia kiasi fulani. nadhani ni kwa sababu ya maradhi na kustaarabika.

  mahusiano ya kimahaba baina ya walimu na wanafunzi wa vyuo vikuu sio haramu ikiwa hayatumiki kutoa upendeleo ama uonevu wa aina yoyote. Namaanisha ikiwa mwalimu ana mpenzi wake ambaye ni mwanafunzi basi uhusiano huo usitumike kumpa mwanafunzi alama za bure/ziada. au pia ikiwa mwanafunzi hatapenda kuendelea ama kuanzisha uhusiano na mwalimu basi mwalimu asitumie nafasi yake kumkandamiza/kumtesa mwanafunzi. Je hatujaona mwalimu na mwanafunzi wakioana?

  ReplyDelete
 2. Hiyo kali lakini naipenda ije bongo

  ReplyDelete
 3. Kama mambo yangekuwa hivi pale mlimani hakuna profesa ambaye angebaki kwani hata viprofesa vizee kabisa vinavyopaswa kuwa vimestaafu au dead bado vinakanyaga mabinti wabichi kabisa wanaopaswa kuwa wajukuu. Mimi nadhani vinakula viagra au Mkuyati. Mimi niliwahi kukamatwa katika somo rahisi kabisa lakini ni kwa sababu tu nilikataa kulala na kiprofesa kibabu. Tunaonewa sana na siku haya mambo yakifika huku mimi nitakuwa wa kwanza to prosecute hawa wasomi wasiojiheshimu. VERY SHAMEFUL

  ReplyDelete
 4. Mwaipopo ungekuwa mwanamke usingesema hivyo! Tunaonewa sana!

  ReplyDelete
 5. Acheni kulalamika nyie mabinti msio na adabu. Hivyo viprofesa vizee kwani vinawabaka? KAama vinawabaka mbona hamwendi mahakamani? Kusoma hamtaki kazi kutafuta wanaume wawape pesa za kununulia simu za bei mbaya, TV na vipodozi even cars wakati washamba mmetoka vijijini. Wakati wa mitihani ukifika mnaanza kuhaha na mnavipanulia mapaja vibabu ili mfaulu. Navyo kwa vile damu bado inavichemka vinawabanjua, mnapata C na maisha yanaendelea. Sasa mnalalamika nini?

  Mngesoma kwa bidii na kuonyesha msimamo wenu viprofesa hivi vizee kamwe vizingewagusa. Shame on you na huu utandawazi. Ukimwi utawamaliza ninyi na hivyo viprofesa vyenu vizee!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU