NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, November 30, 2009

UBAGUZI TANZANIA - WATANZANIA WASHUSHWA NDEGE YA PRECISION AIR

 • Mbona Waafrika/Watanzania tunawapapatikia sana wazungu kiasi cha kufikia kubaguana sisi kwa sisi? Ni kwa sababu ya makovu ya utwana wa kisaikolojia ambayo tuliachiwa na wazungu wakati wa biashara ya utumwa, ukoloni, ukoloni mamboleo na sasa utandawazi?
 • Ukienda katika mahoteli makubwa yanayoitwa ya "kitalii" huduma utakazopata utajua tu kwamba mtu mweusi hutakiwi kuwa pale. Watumishi wote watakuwa wanakimbilia wazungu. Na wakati mwingine mtu mweusi - hata kama nawe una dola zako kama hao wazungu - utanyimwa huduma kabisa, na au kubezwa. Tazama hapa.
 • Sasa hata kwenye ndege ni mzungu kwanza! Isome habari hii kutoka gazeti la Tanzania Daima hapa ambapo Watanzania walishushwa katika ndege ya Precision Air iliyokuwa inatoka Arusha kwenda Dar es salaam na kupakia wazungu badala yake - pamoja na kwamba Watanzania hao walikuwa na "booking" ya muda mrefu! Inafurahisha kusikia kwamba abiria hawa Watanzania waligoma kushuka katika ndege hiyo. Inabidi tusimame kidete matukio kama haya ya kubaguliwa yanapotokea ingawa kusema kweli unahitajiwa mkakati wa kijamii kuweza kurekebisha hali hii - kama inarekebishika kwani utandawazi unazidi kuchochea moto huu wa Mwafrika kujidogosha yeye pamoja na utamaduni wake.
 • Huku katika nchi za wazungu watu weusi tunabaguliwa, na nyumbani nako tunabaguliwa? Tukimbilie wapi?

6 comments:

 1. Hii ni aibu kubwa sana kwa nchi yetu, je tukiamua kuachana/kususia ndege hizo na kuwaachia wapakie wazungu tu hili shirika si litakufa.
  Na serekali yetu hapa itakaa kimya kama haijui kitu

  ReplyDelete
 2. Wazungu wengi wanaokuja huku ni masikini sana huko nyumbani kwao na wanakuwa wamesave pesa kwa miaka mingi ili waende kuclimb mount Kilimanjaro. Sasa sisi tukiwaona ooh mzungu mzungu mzungu utafikiri tumeona Yesu Kristo. Very stupid aisee. Nilikwenda Italy nikaona real situation na nikashangaa. Watanzania tutusie Precision tuone kama hao wazungu watasawasaida

  ReplyDelete
 3. Mimi ni mshabiki wa mwandishi maarufu Ernest Hemingway, Mmarekani ambaye aliwahi kutembelea na kuishi Afrika Mashariki, miaka ya 1933-4 na pia 1953-54

  Baada ya utafiti wa miaka yapata sita, nikafikia hatua ya kuandaa kozi maalum, ya kuwapeleka wanafunzi Tanzania kutembelea sehemu alizotembelea mwandishi huyu, huku tukisoma maandishi aliyoandika kuhusu sehemu hizo, kama vile "The Snows of Kilimanjaro" na "Green Hills of Africa."

  Siku moja, tukiwa kwenye hoteli fulani ya kitalii katika mbuga za hifadhi Tanzania na hao wazungu watupu na Mswahili mimi, alikuja mhudumu mmoja Mtanzania akaniuliza kama mimi ndio dreva wa hao wazungu.

  Kazi tunayo.

  ReplyDelete
 4. Na kweli kazi tunayo. Ila kama tutayafanyia kazi yataisha tu japo si kwa usiku mmoja.

  ReplyDelete
 5. Profesa Mbele. Hata mimi nilishakumbana na tatizo hilo pale Kempsink. Niliulizwa kama nilikuwa nawasubiri wazungu fulani hivi waliokuwa pembeni wakivuta sigara! Profesa Ngonyani naye yaliwahi kumpata kule Ngorongoro alikokuwa amepeleka wanafunzi. Tazama maoni yake hapa chini.......

  Wananchi, suala hili linanifanya nikune kichwa mara nyingi. Tufanye nini? Niliwapeleka wanafunzi wangu wa Kimarekani kule Ngorongoro. Asubuhi wakati wa kujipatia lunch box, mhudumu akaniambia sitakiwi kupata chakula pale. Nilichanganyikiwa, nikahoji si pale ndipo watu wanachukua lunch box. Akasema ndiyo lakini wageni tu, madereva hawapatii pale. Nikaelewa kwamba mimi mweusi sina lolote jingine ila udereva tu, na kwamba udereva hauna hadhi. Kumbe ndiyo maana usiku uliotangulia sikupata majibu mazuri kuhusu chakula cha jioni, mpaka walipoona nimekaa na vijana wangu sehemu ya kusubiri tunapiga stori na wananiita mwalimu. Kwenye haya mahoteli tunakumbana na haya kila mara na hasa kama mtu unakimbia pamba katika joto la Dar.

  ReplyDelete
 6. mpaka tujitambue tu. huoni ilivyo neema kwa JK kuitwa na Bush/Obama? nasi tunaiiita heshima

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU