NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, November 7, 2009

UTAFITI: UNENE UNASABABISHA AINA NYINGI ZA KANSA KULIKO ILIVYODHANIWA

 • Mbali na kuwa chanzo kikuu cha magonjwa ya moyo, watafiti sasa wanasema kwamba unene ukiwemo ule wa futufutu (obesity) ni kisababishi kikubwa cha aina mbalimbali za kansa. Kwa mfano, watafiti sasa wanasema kwamba:
 • Unene unasababisha asilimia 49 ya kansa za mfuko wa uzazi, ikifuatiwa na asilimia 35 ya kansa za matumbo. Unene pia unasababisha asilimia 28 ya kansa za kongosho (pancreatic cancer), asilimia 24 ya kansa za figo, asilimia 21 ya kansa za kibofu cha mkojo, asilimia 17 ya kansa za matiti na asilimia 9 ya kansa za utumbo mkubwa (colorectal cancer)
 • Mbaya zaidi - watu wanene wanaongoza kwa kufa na kansa kwa sababu mara nyingi wanapopata kansa, kansa zao huwa hazitibiki kwa urahisi kama za wenzao wembamba
 • Mimi nadhani kwamba utafiti huu haukuzingatia sababu zingine zinazosababisha kansa yakiwemo mazingira na mfumo wa maisha ya watu. Nyumbani tuna/tulikuwa na watu wanene lakini kutokana na tabia ya watu kufanya kazi sana pamoja na kula vyakula vya kiasili (ambavyo havijabadilishwa kisayansi ikiwemo kutiwa mahomoni ya bandia, mbolea kali na madawa mengine) hata Shirika la Afya Duniani linakiri kwamba Afrika lilikuwa ni bara lenye wagonjwa wachache kabisa wa kansa. Na halafu utandawazi mpya ukaja.
 • Leo hii tumebadilisha maisha yetu, tunakula vyakula vile vile tunavyoletewa kutoka nchi za Magharibi na mfumo wetu wa maisha umebadilika. Matokeo yake sasa kuna mripuko wa kansa za kila aina na unene - jambo ambalo miaka michache tu liliyopita ilikuwa jambo la kujivunia - sasa linaonekana kuwa ni jambo la hatari! (Tazama pia hapa na hapa)
 • Isome ripoti kamili hapa na tazama video fupi ya CNN kuhusu jambo hili muhimu hapa.

3 comments:

 1. Habari za muhimu hizi kama zitapewa attention. Utandawazi ni njia mojawapo ya hawa jamaa kutumaliza.

  ReplyDelete
 2. Posti elimishi na nzuri sana Prof. Matondo.

  ReplyDelete
 3. Dada Subi (na anony hapo juu) - asanteni. Lakini ni nani ambaye anasoma na kuzingatia?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU