NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, November 2, 2009

WANASIASA WA AFRIKA: IGENI MFANO WA JENERALI PERVEZ MUSHARRAF WA PAKISTAN

 • Imegundulika hivi karibuni kwamba kati ya dola bilioni 6.6 ambazo Marekani iliipatia Pakistan ili kuisaidia kupambana na magaidi wa Kitaliban na al-Qaida, ni dola 500 tu zilizotumika kwa lengo hilo.
 • Badala yake, rais aliyepita wa nchi hiyo, Jenerali Pervez Musharraf, alitumia kiasi kikubwa cha pesa hizo kujaribu kuinua uchumi wa nchi yake uliokuwa ukididimia. Pesa zingine zilitumika kuimarisha majeshi ya Pakistan (ambayo daima ipo katika hatihati ya vita dhidi ya jirani yake India).
 • Kilichonivutia katika ripoti hii ni kwamba hakuna panapotajwa kwamba Musharraf aliiba pesa hizi na kuzificha kwa manufaa yake binafsi - jambo ambalo pengine tungelitegemea kwa viongozi wengi wa Waafrika.
 • Badala yake, kiongozi huyu wa kijeshi, aliweka maslahi ya nchi yake mbele na kuamua kuzitumia pesa hizo kuinua uchumi wa nchi yake pamoja na kuimarisha majeshi yake ukiwemo ule mradi tata wa mabomu ya Nyuklia.
 • Ati, Afrika leo tungekuwa wapi kama viongozi wetu wangetumia pesa za misaada na mikopo (ambazo tumekuwa tukipewa/tukikopa tangu uhuru) kwa kuendeleza nchi zao badala ya kukimbilia kuzificha katika mabenki ya Uswizi?
 • Pamoja na matatizo yake yote, pamoja na udikteta wake wote - kwa hili namuunga mkono Jenerali Pervez Musharraf na huu ni mfano wa kuigwa na viongozi wa Afrika!

4 comments:

 1. Viongozi wa Afrika waache kuiba wachekwe??? Bila rushwa na ufisadi Afrika ingekuwa mbali sana. Kabisa kusingekuwa na haja ya watoto kusomea chini ya miti na wananchi kukosa maji ya kunywa. Watajibu siku moja mbinguni hawa mafisadi. Cha ajabu ni kwamba nao wanakufa na KUOZA

  ReplyDelete
 2. That is the way to go Gen. Musharraf. Acha hao jamaa wasiojua kitu walete mabilioni yao.

  ReplyDelete
 3. We subiri usikie kuwa nchi fulani imemuwekea vikwazo Musharraf kwa "kuiibia" na hutashangaa kusikia viongozi wa Afrika wakiwa wa kwanza kutekeleza vikwazo hivyo hata kama hawahusiki nalo.
  Wanasikia "wakubwa" wanalosema
  Tutafika tuuu

  ReplyDelete
 4. Msharraf alitumia kichwa badala ya tumbo. Watawala wetu-si viongozi- au sema hata wezi wetu-wanatumia utumbo kufikiri badala ya ubongo. Wamejaa upogo na ufisi kiasi cha kutisha.
  Wanatuuza, kutuchuuza na kutotoa sadaka wakiwamo hata wao. Baada ya kustaafu-kama Mkapa, Muluzi, Chiluba na Moi wanaishi kwa kujificha kama bundi huku wakitegemea kukingia vifua na wezi wenzao waliowarithi kwenye mchezo mzima mchafu wa ujambazi wa kutumia ikulu na wake zao na waramba viatu wao bila kusahau watoto wao.
  Nkwazi Mhango
  Zaidi unaweza kuliona hili kwenye kitabu changu kipya cha SAA YA UKOMBOZI ambacho kimo mitaani.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU