NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, December 3, 2009

ARE MEN WIRED TO CHEAT? - SASA NI ZAMU YA TIGER WOODS!!!

 • Tiger Woods - mwanamichezo tajiri kuliko wote duniani na anayeheshimiwa sana kutokana na maisha yake ya faragha, kujali familia, utayarifu wake wa kusaidia masikini, upendo na msimamo wake usiotetereka, moyo wa kishujaa wa kushindana; na kutokubali kushindwa hatimaye naye ameangukia katika mtego ambao umeshawaangusha watu wengi "mashuhuri/macelebrity" hapa Marekani - kutembea nje ya ndoa.

 • Tangu apatwe na ajali ya gari ya kutatanisha nje ya nyumba yake tetesi zilianza kuzagaa kwamba kilichomletea majeraha usoni si ajali ya gari bali ni mkong'oto kutoka kwa mkewe.

 • Muda si muda zikaibuka tetesi kwamba Tiger ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja anayekaa New York. Mwanamke huyo alikana shutuma hizo lakini mwingine akaibuka na kudai kwamba kweli yeye ni nyumba ndogo ya Tiger, na amekusanya barua pepe na "text messages" alizokuwa akitumiwa na Tiger. Ujumbe mmoja kutoka kwa Tiger unasema "I will wear you out...when was the last time you got (***?). Mwingine unasema "Send me something very naughty...Go to the bathroom and take (a picture)." Soma habari zote hapa na hapa.
 • Watu walikuwa wanachukulia habari hizi kuwa ni udaku tu lakini maelezo ya Tiger mwenyewe ambayo ameyaweka katika tovuti yake yamethibitisha kwamba baadhi ya tuhuma hizi ni za kweli na hii imezua sokomoko kweli.
 • Swali ambalo watu wengi wanajiuliza ni hili: Kwa nini mtu mashuhuri na anayeheshimika kama Tiger aamue kutembea nje ya ndoa wakati akijua kabisa kwamba jambo hili litajulikana na kumharibia kila kitu? Ni lazima kutembea nje ya ndoa?
 • Kwangu mimi swali hili ni la kipuuzi kwani "macelebrity" hawa ni watu tu wa kawaida tu, tena wanaowindwa na kila mwanamke kwa sababu wanaonwa kama njia rahisi ya kujipatia utajiri na umaarufu. Kama akina "baba askofu" - watu ambao wameandaliwa na kufundwa kwa miaka mingi kuyashinda majaribu ya aina hii - wanaanguka katika majaribu haya, sembuse hawa "macelebrity?"
 • Zamani kidogo niliweka katika blogu hii utafiti wa kisayansi ulioonyesha kwamba kutembea nje ya ndoa kwa wanaume siyo jambo la kushangaza kwani binadamu ni mnyama na wanyama wote wana hulka hii (SOMA HAPA). Wanasayansi wanasema kwamba kuna mnyama mmoja tu ambaye ndiye amethibitika kwa asilimia 100 kuwa na mwenzi mmoja tu katika maisha yake yote - mnyoo fulani unaoishi katika matamvua (gills) ya samaki. Sijui kama akina Yasinta, Koero na Mwanamke wa Shoka wanakubaliana na matokeo ya utafiti huu. Kazi ipo!

2 comments:

 1. Men are no more wired to cheat than women are.

  ReplyDelete
 2. HAKUNA MWANADAMU MWENYE AKILI TIMAMU ANAYEWEZA KUUNGA MKONO ALICHOFANYA Tiger. Ila najua wapo ambao wanaweza kutopendelea namna ambavyo habari nzima imekuwa ikiripotiwa. Nami ni mmoja wao
  Nitakuwa upande wa KUWASAIDIA KINAMAMA katika hili.
  Umeshawahi kujiunguza kidole kisha ukakiweka kwenye maji baridi ama barafu? UNAPATA NAFUU YA UCHUNGU.
  Ndilo nionalo kwa wanawake kuhusu suala la wanaume ku-cheat. Nilisoma kwenye blog moja ya Dadangu kuwa wastani ni mwanaume mmoja kwa wanawake kama wanne. Nikajiuliza ni nani wa kulaumiwa? Ina maana katika wanaume 10 wanaolala nje ya uaminifu wao, kuna wanawake 40 wafanyao hivyo. Sasa kwanini tuweke lawama zote kwa wanaume? Wanawake wanataka usawa lakini inapokuja kwenye suala kama hili wanajiweka pembeni na kusema "mwanaume ndiye aliyemfuata".
  Ndio mfano wa kidole na moto. Kama wanawake wanafuatilia usawa, basi wajue gharama zake.
  Hii kama Tiger alikuwa na wanawake 2 ama 4, ni wangapi kati yao hawakujua kuwa ana mtoto? Leo hii anajitokeza mwanamke kwenye Tv kusema kuwa alikuwa na uhusiano na Tiger na bado watu wanamuacha na kuendelea kumshambulia Tiger. Ni kipi ambacho Tiger amefanya kimakosa ambacho mwanamke huyo hakufanya?
  Nadhani ulimwengu uache kumuangalia mwanakmke kama mdhaifu kiasi hicho. Ni hao hao wanawake "wanaowatega" wanaume kuweza kuwapata. Kama juhudi zitawekezwa kuwafanya wanawake waseme HAPANA, basi wanaume hawatakuwa na pa kwenda na watakuwa waaminifu (kama hawatapendana wenyewe), na hapo tutaweza kuwa na lawama za kweli.
  Tiger na mwanamke / wanawake hao wamefanya kosa la aina sawa na sidhani ni kwanini wamtumie huyo mwanamke kum-crash Tiger (ambaye sijawahi kuwa shabiki wake hata chembe kutokana na baadhi ya kauli zake nilizosikia kuhusu uAfrika)
  Basi tujaribu kuweka lawama kwa msisitizo huu tuuonao kwa huyo Dada tuone ni wangapi wataweza kujitokeza kufanya na kusema haya yasemwayo na kutendwa.
  Blessings

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU