NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, December 1, 2009

ATI, KWA NINI ULIAMUA KUANZISHA BLOGU?

  • Nimeiona hii katuni ikanifikirisha. Kila mmoja wetu ana sababu yake ya kuanzisha blogu: kuelimisha, kuburudisha, kutangaza biashara, kubadilishana mawazo, kutahadharisha, kukosoa, kupongeza, kujipatia umaarufu, kuipigania jamii, kuhakiki, kushambulia, kujiongezea kipato, kukomoa, kueneza mawazo kombozi (hata kama siyo), kutapanya mitazamo na mitindo bora ya maisha (hata kama siyo), ku....Ati, ni kwa nini wewe uliamua kuanzisha blogu? Ungali umemakinikia lengo lako la awali au umeshapogoka, ukalitelekeza lengo lako kuu na kufuata "mkumbo" ili pengine kuweza kuvutia wasomaji katika blogu yako?. Sina nia mbaya na msije mkanielewa vibaya Ni hii katuni tu imenifikirisha! Samahani!

2 comments:

  1. Wacha nilale ntalijibu kesho maana nilikuwa nimeanza kuandika juu ya hili
    Blessings

    ReplyDelete
  2. Ulale unono. Tunasubiri mtazamo wako kuhusu hili.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU