NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, December 15, 2009

ATI: UNAONA "OPTICAL ILLUSION" YO YOTE KATIKA PICHA HII?

 • Jamani. Nimeambiwa eti kuna "optical illusion" kali katika picha hii. Nimeichunguza kwa karibu dakika mbili nzima lakini sijaona kitu kingine kipya mbali na kile nikionacho. Kama kuna anayeona cho chote basi atwambie. Isije ikawa kama kule kwa Kamala ambako tulifumba macho weee bila kuona cho chote.

10 comments:

 1. ha ha ha hah ha ha hah, kaazi kweli kweli.
  Huyo dada aliyeshika camera, mkono wake wa kulia kwenye kikunjo cha kiwiko imetengeneza taswira ya matako kwa yule dada aliyesimama kuleeee na shati lake la drafti za pinki na nyeupe. Nadhani nimetumia sekunde 30 tu na picha hii ndo kwanza naiona leo, atakayeona zaidi ya ahapo atufahamishe. LOL ha ha ha hah!

  ReplyDelete
 2. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 15, 2009 at 12:03 PM

  duh!

  ReplyDelete
 3. Dada Subi - Aisee! Kweli wewe una "macho makali". Hata mimi sasa naweza kuona. Hii kweli ni duh! kama alivyosema Ng'wanambiti!

  ReplyDelete
 4. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 16, 2009 at 7:33 AM

  sasa naona kama 'tako' lina g-string ya kiaina, ama!...lol

  ReplyDelete
 5. matondo umeona? hivi ile kozi ya meditatation ya kuona vitu kwa kutumia jicho la rohoni ulifikia wapi?

  ReplyDelete
 6. Kamala - sikuona cho chote. Nilifumba macho nikawa naona nyoka wa kule Usukumani (nina phobia nao) basi nikaghairi. Pengine yahitaji mafunzo. Niliomba sana watu wakiona cho chote waseme lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza na kusema ameona kitu.

  ReplyDelete
 7. kweli uliona Nyoka? yaweza kuwa sehem ya wrong meditation kwamba umeenda upande mwingine. tafuta vitabu vya meditatio usome na kuelewa vinapatikana sana marekani. kimoja wapo ni the science of meditation cha torkom Saraydarian, tafuta you the healer cha Jose silver na vinginevyo. hii ni sayansi ya ajabu na nzuri na muhimu pia

  ReplyDelete
 8. Kamala. Nitavitafuta vitabu.

  Hapana sikuona nyoka bali nilikuwa natania tu. Niliona rangi zinaingiliana tu bila mpango.

  Sayansi ya meditation hapa ina mvuvumko sana na sasa imeingia katika tiba. Si ajabu tena daktari hapa kukushauri ufanye meditation pamoja na yoga. Ukiangalia channel ya Discovery Health mara nyingi utawasikia watu ambao walikuwa na magonjwa yasiyotibika na walikuwa wamepewa muda mfupi tu wa kuishi na madaktari wao. Walipoanza kufanya meditation walipata amani, utulivu na ujasiri wa kukikabili kifo. Hali zao zilibadilika na kinga yao ya mwili iliimarika. Matokeo yake wengi wao bado wanaishi - kitendo ambacho kinawashangaza madaktari.

  ReplyDelete
 9. ni meditation. hata ukimwi unatibika. kwa ufupi hakuna lisilowezekana katika meditation. hata yesu Kristo alimeditate ndo akapata nguvu zoote za kimaumbile, hakuna gumu katika hili. meditation inakukpa Hekima Ipitayo uelewa woote.

  nakupamoyo Prof. twende kazi. zile rangi ilibidi uendelee kuwa ntulive na kurelax, ungeona tu

  ReplyDelete
 10. yap nimeoiona!!kule nyuma kuna dada tako linaonekana ila sio tako ni mkono wa mpiga picha!!
  Challenging, i liked it.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU