NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, December 15, 2009

GAZETI LA KWANZA JAMII SASA KUCHAPISHWA MARA MOJA TU KWA MWEZI!

MABADILIKO KWANZA JAMII

Wapendwa wasomaji wa gazeti hili la KWANZA JAMII,

Baada ya kutafakari kwa kina, Bodi ya Uhariri na Uongozi wa KWANZA JAMII tumefikia uamuzi wa kulifanyia mabadiliko gazeti lenu hili ili tuweze kukidhi mahitaji yenu. Hadi hapo tutakapopata uwezo wa kuwa na rasilimali watu ya kutosha na uwezo wa kifedha kumudu kuchapa kila wiki aina ya makala za kiutambuzi na kielimu mlizo na kiu nazo zaidi, KWANZA JAMII litakuwa likichapa makala hizo mara moja kwa mwezi, hivyo basi, kuanzia toleo hili, KWANZA JAMII litakuwa likitoka mitaani kila Jumanne ya kwanza ya KILA MWEZI, kwa maana ya mara moja kwa mwezi. Tunaahidi KWANZA JAMII litakuwa likitoka likiwa na ubora zaidi ya wa sasa. Vinginevyo, unaweza kuendelea kusoma KWANZA JAMII mtandaoni kila siku na kwa maana hiyo kufuatilia na kuchangia katika mijadala hai. Kwa taarifa kamili soma hapa.

Inavyoonekana mambo hayaendi vyema katika gazeti hilo ambalo lilikuwa likijibidisha sana kuchapisha makala za uchambuzi. Nimeligusia suala hili katika makala yangu itakayochapwa wiki ijayo ambayo kimsingi ni jibu la makala ya Padri Privatus Karugendo.

2 comments:

 1. Tatizo la Bwana Mjengwa ni kutokuwa na washauri au ni kitu gani?
  Kaanzisha Gozi likafa, sasa na hili nalo linarusha rusha miguu kukata roho. Why?
  Naandika kwa uchungu kwa sababu yanayotokea hayapendezi. hakuna anayependa kilichoanzishwa kife.

  Kuna tetesi kwamba upungufu wa wasomaji wa gazeti lake ni kwa sababu ya utaratibu wake wa kuioshea serikali hata psipohitaji miosho. Ajirekebishe tutaanza kulisoma

  ReplyDelete
 2. Mjengwa pia ana mambo ya udini udini na ni wazi kwamba gazeti hilo pengine ni la CCM. Kwa hivyo sie tunaona bora kusoma uhuru na Daily News kuliko kusoma gazeti lisilokuwa na mwelekeo. Kama ni makala basi kuna Raia Mwema ambako kweli mtu ukisoma unaridhika. Au Mwanahalisi. Gazeti kufanikiwa ni lazima kuwa na agenda iliyo wazi na siyo hii ya Mjengwa ya kutumiwa na CCM kwa kujifichaficha.

  Nashanggaa mpaka leo ni kwa nini kwa mfano gazeti hilo haliandiki habari/picha za vijijini wakati Mjengwa ana blogu ambayo inahusika sana na mambo ya vijijini? Amepoteza nafasi nzuri sana kwa kuwa gazeti la kwanza kuandika habari za kijijini.

  Halafu website ya gazeti hilo ni ya kitoto. Imekaa kama vile blogu na mtu ukienda pale unaona makala moja moja tu. Halafu unakwenda kwenye tovuti za Raia Mwema, Habari Leo na mengineyo. Unaona matoleo mazima ya magazeti. Hata ukiliona gazeti mtaani basi unatamani ulinunue.

  Haya ndiyo matatizo makubwa ya Mjengwa. Kama ana washauri basi mshaurini otherwise atachoka tu kuanzisha magazeti halafu yanakufa!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU