NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, December 12, 2009

KABINTI KANGU KA PILI KAMEFIKISHA MIAKA SITA

Ni hako katikati. Kanaitwa Zofa Minza Matondo. Kako shule ya vidudu na mwaka kesho kataanza darasa la kwanza. Ni kamalaika ka Mungu kazuri, kapole, kacheshi, kenye huruma na kanakopenda sana kusoma vitabu!
 
  Keki ilitakiwa iwe na "microphone" ya Hannah Montana. Kazi kweli kweli. 
   Marafiki kadhaa walikuweko kusherehekea na kuimba "Happy Birthday, happy birthday to you Zofa" 

    Best friend naye alikuweko!
      Baada ya maakuli na shamrashamra nyinginezo, ilibidi kuingia katika "Nascar". Hapa dad anahakikisha kuwa hatua zote za kiusalama zimezingatiwa. Happy Birthday Zofa Kija Matondo! (Kosa - jina linapaswa kusomeka Zofa MINZA Matondo)

      21 comments:

      1. Happy birthday mtoto. Uishi many many years. Thanks!

       ReplyDelete
      2. Matondo, hongera zangu kwa Zofa kwa kufikisha miaka sita. Naomba mpigie huu wimbo: www.youtube.com/watch?v=XdakudMZ0J4.Nadhani umechanganya madawa vibaya kwenye jina la kati la Zofa, je ni Minza au Kija?

       Sijui nianze kutoa posa mapema kama wamasaidi, maana pale kwangu kuna timu nzima ya madume, ambapo wasingependa kumkosa mrembo kama huyu.

       ReplyDelete
      3. Mstari wa kwanza aya ya pili nilitaka kumaanisha kama wamasai.

       ReplyDelete
      4. Happy birthday Zofa,kweli ni kamalaika kazuriiii! kana onekana kana sura ya upole na kacheshi kapenda watu,hongera sana shangazi nimefurahi sana kusikia unapenda kusoma,mungu akusaidie uendelee kuwa hivyo hivyo na tabia nzuri.Uendelee kuwa mtoto mzuri kwa baba na mama pia,sawa shangazi?xxxxxx

       ReplyDelete
      5. Mwalimu Prof.Matondo mpe hongera binti na sisi huku Bandari Salama tunampa hongera! Mwambie ndugu zake huku nao wanaendelea vizuri saa hizi mawazo yetu na vichwa vinakunwa ili ipatikane nguo ya sikukuu , ada,kodi ya nyumba na vikolombwezo vingi!!Unamiss vingi huku ikiwa ni pamoja na kutembelewa na ndugu kipindi hiki wasiotoa taarifa wanakuja kuona bahari kwa ajili ya krismas!! Akikua mhadisie asije kosa mengi aloishi babaake!

       ReplyDelete
      6. Hongera kwa siku ya kuzaliwa kutoka kwa shangazi yako Yasinta..

       ReplyDelete
      7. Asanteni sana. Nitafanya kazi ya kumtafsiria Zofa maneno yenu mema. Mashangazi itabidi mjiandae kuwafunda hawa watoto kwani ndiyo kazi yenu mojawapo. Kazi mnayo!

       Bwana Matiya. Asante kwa kusoma vizuri na kuona jinsi nilivyochanganya majina. Ndiyo maana hata Mumyhery nikamchanganya. Jina la kati ni Minza na siyo Kija na kwa hivyo jina kamili ni Zofa Minza Matondo. Kija ni "first born" na ni jina la bibi mzaa baba aliyekuwa ananipenda sana! Pengine ndiyo maana jina hilo limechomoza hata mahali lisipotakiwa.

       Bwana Ntisi - umenifurahisha na kunikumbusha nyumbani pia. Nakumbuka wakati wa sikukuu kule kijijini enzi zile bila kupata kaptula mpya, shati na viatu mambo hayaendi. Mchana tulikuwa tunakwenda mjini Bariadi kutembea na kununua maandazi na MIWA, na jioni ni lazima kuwe na ubwabwa na nyama ya kutosha. Familia nzima, ndugu na majirani wanakusanyika hasa kama siku hiyo kumechinja mbuzi, kondoo au ng'ombe pale nyumbani. Ilikuwa safi sana!

       Hilo la kutembelewa na ndugu wasiotoa taarifa nadhani pia litabadilika muda si mrefu kwani mfumo wetu mzima wa maisha umeanza kubadilika na kuwa wa kizungu. Muda si mrefu itakuwa ni mtu na familia yake tu basi. Nimeshaanza kuiona hali hii pale Dar es salaam ambako watu sasa wameanza kuzaa mtoto mmoja au wawili tu na hawakubali tena kurundikiwa watoto wa kulea na kusomesha hata kama wana uwezo wa kufanya hivyo. Hii pengine itachukua vizazi viwili vitatu hivi; na sina uhakika kama hili ni jambo jema. Kwa hivyo hapa sijui kama nikupe pole au nikupongeze!

       Zofa na dada zake watakwenda nyumbani usukumani muda si mrefu ujao. Ni lazima wajue kwao.

       ReplyDelete
      8. 'ongela' zofa kwa kusogeza umri. nimependa tabia yako ya kupenda 'kubukua'

       ReplyDelete
      9. TOTAL KNOCKOUT - asante kwa kutembelea hapa na kuipenda blogu hii. Hivyo vigari vya "Nascar" vina injini na vinaweza kwenda mpaka maili 25 - 30 kwa saa. Ndiyo maana nahakikisha binti amejifunga mikanda vizuri!

       Mwaipopo - asante. Mi naendelea kutafsiri tu kwani Kiswahili cha hawa mabinti ni cha kurashiarashia tu!

       ReplyDelete
      10. Hongera shangazi yangu Zofa, Mungu akubariki sana katika maisha yako upende kusoma vitabu zaidi na zaidi kwani ndimo utakapopata maarifa yote. Swali je umemeliza vitabu vingapi vya Hannah Montana? na sinema zake je? Nimeipenda keki yako shangazi.

       **Hannah Montana jamani!! Kumbe kaka matondo na wewe yamekukuta haya?

       Halafu wenzetu kwenu winter vipi?

       ReplyDelete
      11. Da Mija - akina Hannah Montana hawaepukiki. Tupo karibu na Disney Orlando (saa moja na nusu kwa gari) na akina Zofa ni lazima waende huko karibu mara mbili kila mwaka. Basi hapa ni Disney tupu na Hannah Montana ndiye ametawala - kuanzia vibaiskeli, wanasesele, vitabu, Nintendo DS n.k. Kazi kweli kweli.

       Hapa Florida Winter huwa siyo kali sana, na kwa kawaida huwa hakuna barafu. Kwa mfano sasa zaidi ya robo tatu ya nchi imefunikwa na barafu lakini hapa Florida bado ni joto. Wakati kama huu watu wengi huondoka sehemu zao za baridi na kuja kupumzika huku. Kwa hivyo utalii hapa ndiyo shughuli kubwa ya kiuchumi. Huko kwenu Netherlands nadhani sasa ni baridi kali sana. Poleni!

       ReplyDelete
      12. aaaaaaaw!! Hehe! Hannah Montana stuff...I am sure she likes High School Musical too...na kama you live near the park then it is so likely kwamba watoto watapenda vitu hivyo, anyway japo I am late but Happy Birthday dada mdogo

       ReplyDelete
      13. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 14, 2009 at 10:32 AM

       Hepi besdei Zofa!

       Halafu nimependa/nimestushwa na maneno ya hiyo fulana ya huyo 'best frendi' imeandikwa "Boys Rule"...duh!

       Wanakuja lini bariadi niwaandalie matobholwa na michembe?....lol

       Kisha tuwachinjie mbuzi tuwatengenezee ma-chibhulanga....lol

       ReplyDelete
      14. Hongera Zofa kwa kutimiza miaka sita. Tabia ya kusoma imenikuna!

       ReplyDelete
      15. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti - hebu usinikumbushe nyumbani. Matobolwa/michembe na chibulanga. We acha tu.

       Fulana ya huyu kijana isikushangaze - mfumo dume bado unatawala dunia nzima. Tena ukiitazama vizuri haijaishia hapo bali inasema: Boys Rule, Girls drool" Upo hapo?

       Hapa tumeshazoea nguo zenye maandishi aina aina. Ungefanyeje kama mwanafunzi wa kike angetinga darasani kwako na kifulana kilichoandikwa "Self Service?" au kibukta kilichoandikwa "Juicy" matakoni. Ungemtoa mkuku au? Tumeshazoea!

       Bwaya - Asante! Nitamwambia Zofa kutokuitelekeza tabia hiyo!

       ReplyDelete
      16. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 15, 2009 at 9:25 AM

       @ Matondo: naweza kukutumia chibulanga kwa posta...lol

       duh! kama hali ni hivo inabidi uwe ngangari a.k.a jidulamabambasi....lol

       ReplyDelete
      17. Hongera kwa kusherekea sikukuu ya kuzaliwa Minza! Mungu aijalie familia yenu mafanikio tele!

       ReplyDelete
      18. AISIFIAYE MVUA.........
       Kwa sasa sina hakika kama mtu akiwa na mwana anayesherehekea umri kama huo nahitaji kutanguliza POLE ama HONGERA? Najua vyote ni vyao lakini kpi cha kwanza?
       Kwa Minza wewe unaombewa as always. Kwa hiyo wala usijali.
       Nianze kwa SHUKRANI kwake Mungu aliyewawezesha wazazi kumlea Minza kwa namna walivyofanya mpaka hapa. Pia kwa kumtunza na kumuongoza. SIFA NA SHUKRANI VIMWENDEE.
       Pili kwa Mama yake. Hawa kinamama nilikuwa nakutana nao barabarani na kuwaona kama "watu wengine wa kawaida" lakini kuna u-kawaida ulio nyuma ya ule tuuonao ambao kwa hakika unahitaji kuthaminiwa.
       Mwisho kwa Baba kwa kutushirikisha hili. Sasa twajua kuwa kuna Da'Minza ambaye anazidi kukua na kuzidi kuwa m'dada mwema atakayekuja kuwa "BALOZI" mwema kwetu.
       SHUKRANI KWA KILA ALIYEWEZESHA MINZA KUWA ALIVYO LEO.
       Amani kwenu

       ReplyDelete
      19. Hongera kwa hayo ya Kuzaliwa...Miaka Sita...ndio hivyo tena. Tunaingia ulimwenguni tayari tuna umri wa karibu robo tatu ya mwaka!

       Mwalimu, angalia ((December 11, 2009 6:08 pm)pale ulipotundika maelezo kuhusu "mama yangu/wangu"; "ng'ombe yangu/wangu", nk.

       Nimeweka maswali mengine mawili hivi yanayohitaji msaada wako!

       ReplyDelete

      JIANDIKISHE HAPA

      Enter your email address:

      Delivered by FeedBurner

      VITAMBULISHO VYETU