NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, December 26, 2009

MNIGERIA AJARIBU KURIPUA NDEGE KULE DETROIT

 • Wakati ulimwengu ukisherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo, abiria mmoja raia wa Naigeria alifanikiwa kuripua "kifaa" fulani katika ndege iliyokuwa inajaribu kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Detroit.
 • Ndege (Airbus 300) ni ya shirika la ndege la Northwest na ilikuwa inatoka Amsterdam Uholanzi kwenda Detroit, Michigan nchini Marekani. Ilikuwa imebeba watu 278. Ndege hiyo iliweza kutua salama
 • "Kama kawaida" Mnigeria huyo ameelezwa kuwa na uhusiano na makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali.
 • Kwa habari zaidi kuhusu habari hii soma hapa. Kama nilivyotegemea, watoa maoni katika tovuti mbalimbali tayari wanashambulia Unigeria na Uafrika wa mshambuliaji. Tazama video hapa au hapa.

6 comments:

 1. Hii ilitisha saana. Maana ni kwamba mlipuko haukwenda sawasawa la sivyo tungekuwa tunazungumza mengine sasa
  Nilishasema na nasema tena. HATUTAWEZA KUSHINDA VITA VYA KUPIGANA NA MTANDAO KWA KUTUMIA JESHI
  Wako nje wanapigana, humu ndani wanajikusanya
  Mungu atusaidie

  ReplyDelete
 2. Mzee wa Changamoto - umesema kweli. Huwezi kushinda vita vya kifikra, kiitikadi na kitamaduni kwa kudondosha mabomu. Sijui kwa nini Wamarekani wanashindwa kuutambua ukweli huu rahisi na wazi!

  ReplyDelete
 3. Ama kweli hapa kazi ipo, nguvu haiwezi kubadili mawazo ya mtu

  ReplyDelete
 4. kuushambulia uafrika na unaieria ndilo tatizo kuu labda. jamaa wanajiona maalumu kuliko matondo msukuma.

  tuone wamarekani wenye nguvu

  ReplyDelete
 5. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 29, 2009 at 11:57 AM

  nyani haoni ngokoye....

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU