NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, December 14, 2009

TOVUTI MPYA YA HABARI, MUZIKI, KAMUSI, MAFUNZO YA KOMPYUTA NA MENGINEYO

Pole na shuguli za kutupasha habari mbali mbali zinazotokea ndani na nje ya Tanzania.

Naomba nafasi katika blog yako ili niwajulishe ndugu zangu watanzania kwamba nimetengeneza website www.rusumo.com ambapo wataweza kusikiliza nyimbo mbali mbali za Tanzania kama vile taarab,segere,dance,bongo flava,gospel na nyimbo za kigeni kama vile raggae,za kihindi,pop na nyengine nyingi tu.

Pia kuna dictionary ya kisasa kabisa ambayo ina lugha zote za Ulaya na baadhi ya lugha za Asia,katika dictionary hii baada ya kupata tafsiri ya neno pia unaweza kuona picha za neno hilo kwa kubofya upande wa pili wa Ukurasa.

Kadhalika wadau wataweza kuona hali ya hewa na wakati wa sehem mbali mbali za dunia.
Karibuni sana wadau, ni mimi

MSAFIRI ISMAIL RUSUMO.
www.rusumo.com

2 comments:

 1. This guy seems to be uncivilized. See the message below that I copied from his website (when you click the music section). Is Michuzi supposed to accept his announcement? It is his blog and he can decide whatever he wants. Yes we know that Michuzi is bullshit, religiously biased and a dangerous government SHUSHUSHU (that is why he travels a lot) but I think the reaction of this guy is also too much! I am staying away from his website!
  *******************************

  Special message to Issa Michuzi

  Nimekutumia kama mara kumi ujumbe ambao ungeuweka katika blog unayoiita ya jamii ili watanzania wenzangu na watu wote wa Africa ya Mashariki wajue kuwepo kwa website hii, Nimefanya hivyo kwa kujua kwamba ni blog ya jamii na kwa vile na mie ni sehemu ya jamii na lengo langu ni kuwanufaisha wanajamii wote.

  Kumbuka hunibanii mimi isipokuwa wanajamii wote ambao wangependa kufaidika na mambo niliyoyaandaa. Sasa nimeamini kwamba Tanzania inashindwa kupata maendeleo kutokana na kuwepo watu kama nyie akina Michuzi, wenye roho za Korosho,yakhe umenikera kiasi kwamba ningekuwa karibu yako ningekupiga kibao. Mwanamme mzima kazi kulialia tu "Blog ya jamii yapigwa vita"; Nani akupige vita wewe? Mie lengo langu ni kutaka kushare elim aliyonijaaliwa M/Mungu na wanajamii wote, hasa ya watu wa Africa ya mashariki. Nakushauri usiite glob yako glob ya jamii wakati wewe ni mmoja wa wasiopenda maendeleo ya jamii.

  ReplyDelete
 2. Anony hapo juu. Sidhani kama shutuma za Bwana Msafiri kwa Michuzi hapo juu zinahalalika. Kila mwanablogu anajua jinsi ilivyo kazi ngumu kuendesha blogu. Sasa fikiria kama unaendesha blogu kama ya Michuzi ambayo inatembelewa na watu karibu 20,000 kwa siku. Unafikiri ni barua-pepe ngapi anazopata kila siku? Unafikiri zote anazijibu au kuzishughulikia? Katika hali kama hii ni rahisi sana kwa baadhi ya barua pepe kuponyoka.

  Nijuavyo mimi Michuzi anatuunga mkono sana sisi wanablogu wengine na ndiyo maana wengi wetu tulipitia kwake tulipoanzisha hizi blogu naye bila wasiwasi alitutangazia; na leo hii tupo tunasonga mbele.

  Ni lazima pia tukumbuke kwamba hii ni blogu yake na ana uhuru wa kuamua nini cha kubandika pale na nini cha kuacha. Kama hakupenda kuliweka tangazo la tovuti ya Bwana Msafiri huo ni uamuzi wake. Kwa hivyo sidhani kama Bwana Msafiri alikuwa na haki ya kusema hayo aliyoyasema!

  Hayo mengine uliyoyataja hayahusiani na mambo ya blogu wala suala ulilolianzisha!

  Tuvumiliane, tupendane, tuheshimiane...kwani lengo letu ni moja. Tutafika!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU