NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, December 16, 2009

WATOTO WA KUBAMBIKIWA: NANI WA KULAUMIWA? KUNA UMUHIMU WA KUPIMA DNA?

 • Tatizo la kubambikiana watoto inaonekana ni tatizo la tangu zamani.
 • Kabla ya mapinduzi makubwa katika taaluma ya chembechembe za urithi katika miaka ya hivi karibuni, hakukuwa na njia za kisayansi za kuweza kuwathibitishia akina baba kama kweli watoto “waliowazaa” ni wao. Leo hii inawezekana kuhakikisha kwamba huyo mtoto wako asiyekufanana ni wako kwa asilimia 99.99%
 • Katika gazeti la The Guardian la tarehe 10/4/2009 kulikuwa na habari yenye kichwa kilichosema “DNA proof: 60pc of Male Parents not Biological Fathers”. Habari hii pia iliwekwa katika Blogu ya Jamii. Habari hiyo ilimkariri mkemia mkuu wa serikali Bwana Ernest Mashimba akitoa data kwamba katika vipimo vyote vya DNA ambavyo ofisi yake ilikuwa imevifanya, ilibainika kwamba asilimia 60 ya akina baba hawakuwa wazazi halali wa watoto hao bali walikuwa wamebambikiwa tu. Gazeti la Habari leo katika ukurasa wake wa mbele pia liliandika: Wanaume Wengi Wasingiziwa Watoto: katika kila wawili waliopima, mmoja amebambikiwa
 • Katika maoni mengi yaliyotolewa na wadau katika Blogu ya Jamii (kwa bahati mbaya mengi ni ya kiosha vinywa), akina mama hasa ndiyo walioandamwa na kubebeshwa lawama utafikiri kwamba wanajitundika hizo mimba. Mimi nadhani hili ni tatizo la kijamii ambalo linabidi kutazamwa kwa kina na pande zote zinazohusika. Ni lazima tujue, kwa mfano, sababu hasa zinazowafanya akina mama kutembea nje ya ndoa zao wakati huu ambapo gonjwa la UKIMWI linaangamiza maisha ya watu.
 • Swali jingine la msingi ambalo nilijiuliza baada ya kuisoma habari hii ni hili: kuna ulazima kweli wa kupima DNA ili kuthibitisha kama mtoto ni wako ama la? Sipingi matumizi ya DNA katika kutibu magonjwa au kuamua mizozo ya urithi na mengineyo. Ninachopinga ni matumizi ya “kiushabiki” ya DNA mf. ili kuthibitisha kama mtoto aliyezaliwa ni wako eti kwa sababu tu mtoto huyo anamfanana muuza mkaa wa nyumba ya jirani au Mpemba mwenye meza ya mbogamboga katika genge la pale mtaani kwenu.
 • Katika jamii nyingi za Kiafrika mtoto hakuwa “mali” ya mzazi pekee bali alikuwa mali ya ukoo mzima. Ndiyo maana, baba mzazi alipofariki, wanaukoo wengine walipewa jukumu la kumlea mtoto huyo na kuhakikisha kwamba anakua salama. Kwa hali hiyo, kujua “baba hasa” wa mtoto ni nani halikuwa jambo la muhimu sana. Japo leo hii utandawazi unatusukuma na kututenga na utamaduni wetu, kuna mambo ambayo inabidi tuwe waangalifu nayo, na hili ni mojawapo.

  Je, leo hii ukipima DNA na kugundua kwamba kumbe “babako” aliyekulea, kukusomesha na kukusaidia kwa hali na mali katika maisha yako si “babako mzazi” bali alibambikiwa tu utafanyeje? Utamkana? Utamlaumu nani? Na ukipima DNA na kugundua kwamba hivyo vitoto vyako virembo vimalaika vya Mungu uvipendavyo kikweli umebambikiwa utafanyeje? Utavikana? Utamtaliki mkeo?
 • Hebu tusije tukaiga hii tabia ya kupima DNA bila sababu za msingi kwa vile tu eti tumeona katika Maury Show. Huko watu hufurahi na kurukaruka (kama huyu chini) wanapothibitishwa kwamba si wazazi halali wa watoto waliobambikiwa kwa sababu jamii yao imesimikwa katika ubinafsi; na wanakuwa wameziepuka zile gharama kubwa za “child support” – gharama ambazo wangehangaika nazo mpaka huyo mtoto wa kubambikiwa afikishe miaka 18!

10 comments:

 1. Prof. tafadhali badili rangi ya font uliyotumia katika baadhi ya vifungu kwani rangi ya maandishi imelandana na ya background hivyo haisomeki hadi mtu a-highlight. Senkyu!

  ReplyDelete
 2. Dada Subi - Sasa ni saa sita na dakika 17 usiku. Post hii niliiandika kama siku tatu hivi zilizopita. Nilikuwa namalizia kazi fulani hapa na nilitazama blogu kwa bahati mbaya tu kabla sijaenda kulala. Asante sana kwa kunijulisha. Naona HTML zilikuwa zimeparaganyika sijui kwa nini. Huko Ulaya na Tanzania sasa mnajiandaa kuamka/mmeshaamka. Ngoja sisi huku tulale.

  ReplyDelete
 3. hata mimi najiuliza, ila wahaya zamani kama mke anataka kuolewa mara ya pili, sharti mtoto atakayemzaa kwenye ndoa mpaya, arudishwe kwenye ndoa ya zamani kama proof ya kutokupeleka uzazi wa ukoo ule kwenye kizazi kipya.

  anyway mimi sijui. ila ukigundua mtoto aliyezaa mkeo ni wa Obama au bush ni sherehe sio?

  kuna jamaa alienda kusoma nje, ariporudi akakuta demu wake ana mimba, kazi hiyo. mimi nashindwa kuamua hapa ila si ni mtoto tu. kwani watoto wetu wanafananaje?

  kwa bahati nzuri katika ukoo wangu soote tunafanana kwa hgiyo lazima katoto kanifanane tu kwani tunafanana ile mbaya

  ila matatizo ya mimba unayajua. unamlea wife akiwa na mimba, anatapika unaenda kumwaga, hospitali nk, kumbe unalelea wajanja fualani ehe?

  ReplyDelete
 4. Mmh...mie kama mtoto (big baby lol), aliyenilea ndio huyo huyo at least kuna MALE figure in my life na sio kama after a long time I find out kwamba aliyenilea sio biological father, I won't abandon him but I will be curious and want to know who I share my "DNA" with...ndio wanasema "any man can be a father but it takes someone special to be a dad" :-)

  ReplyDelete
 5. The truth ni kwamba wanaume wengi mkivuka 40 years you stop being good in bed mpaka mule maviagra - ambayo nayo si mazuri kwa health. Mnataka sisi tufanye nini? Tunakwenda kusaka vijana wadogo na tukitundikwa huko kwa vile we still want you to provide then we hide it and pile up on you. It is yo mistake guys so stop it.

  Halafu most of you you don;t treat us well -no mapenzi no nothing. Twaenda nje kupata utamu. Vijana wanakamua na nyie mwatunza. Nani mjanja hapo?

  Mama Pekecha - Kinondoni

  ReplyDelete
 6. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 17, 2009 at 9:01 AM

  @Matondo: sidhani kama kuna uchungu ambao mtu anaweza kupata akijua kama mtoto anomlea si wake....lol Ukisikia uchungu basi huyo si wewe bali ego inayozungumza badala yako....lol

  @annony a.k.a Mama pekecha: hilo unalolisema nalo neno....lol! Lakini unachokisema kuwa hawawi good at sita-kwa-sita at 40z sidhani kama ni kweli la sivo tusingesikia wazee kule mjengoni idodomia wanashobokea videmu viduchu viduchu na kuvisambaratisha....mpaka vingine vinakimbia vikiwa vimeshikilia chupi mkononi/kichwani...lol

  kwa kweli hiyo ni case by case kwamba wababa wakifika 40z hawawezi malavidavi....lol

  Halafu juu ya treatment-two way traffic sweetie! Kama naja home nakuta nyumba ovyoovyo na wakati nakuweka ndani ulikuwa kimotibel na sasa unalingana na wale majamaa wa sumo unatarajia nini? sisemi ndo sababu bali ni mojawapo ya sababu ndo maana nasema ni two way traffic

  ReplyDelete
 7. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!December 17, 2009 at 4:30 PM

  @Kamala: hiyo ni siri yangu ila nilikuwa namtafadhalisha Mama Pekecha lisije kumkuta la kumkuta pindi atakapokubali kumegwa na ova40 akakutana na mitwango atakayoenda kumhadithia mumewe a.k.a switii...lol

  ukitaka kujua muulize BIBI yangu....lol

  ReplyDelete
 8. Chachaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa bibi yako???? mama naniliiiiiii wa kale katoto kangu kapendwa jina kama mwanamapinduzi wa guantanamo?? maweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

  ReplyDelete
 9. Cha kujiuliza wakati tunafikiria moja ya chanzo .

  Wewe kama Mwanaume umewahi kutamani mke wa Mtu wakati unajua ni mke wa mtu?


  Mimi nimewahi kutamani aingawa sikuonja!:-(

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU