NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, December 1, 2009

WATU 25 WENYE "AKILI SANA" KATIKA MWONGO HUU

(1) Larry Page and Sergey Brin (Waanzilishi wa Google hapo juu)
(2) Steve Jobs - Mwanzilishi-mwenza wa Apple (Iphone, Ipod...)
(3) Steven Chu - Waziri wa Nishati wa Marekani, Mshindi wa Tuzo ya Nobel (1997) katika Fizikia.
(4) Hillary Clinton - Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
(5) Muhammad Yunus (Bangladeshi) - Mkurugenzi wa Grameen Bank na mshindi wa Tuzo ya Nobel (2006)
 • Mwafrika pekee katika orodha hii ni Kwame Anthony Appiah - mzaliwa wa Ghana ambaye ameshika nafasi ya 13. Kwa sasa ni Profesa wa Falsafa katika Chuo Kikuu cha Princeton.
 • Manmohan Singh - Waziri Mkuu wa India ameshika nafasi ya 11. Tazama orodha kamili hapa. Bofya kwenye kisanduku cha "View all" chini kushoto.

Orodha hii imeandaliwa na Wamarekani na hatuambiwi ni vigezo gani vilivyotumika. Kama tungeandaa orodha ya watu 10 wenye "akili sana" nchini Tanzania kwa miongo sita iliyopita (yaani tangu tupate uhuru), orodha hiyo ingekuwaje? Vigezo?

5 comments:

 1. Namba moja atakuwa Mwalimu Nyerere - kigezo - alijitahidi kuboresha maisha ya wananchi wake bila KUWAIBIA. Japo alishindwa lakini alijaribu sana. Ni mwanafalsafa ambaye watu wanamwandikia PhDs na Masters nyingi tu katika vyuo vikuu...That is the only one I can name.

  ReplyDelete
 2. ni prof Matondo, mzee wa changamoto, Mbelle, mtktf Kitururu, Chacha wambura na hata MIMI! na hayati Munga tehenan.

  unajua ulimwengu huchagua watu wachache na kuwatukuza, je aliyeandaa orodha hiyo kajiweka mwenyewe? bila shaka hapana, hajui labda ni akili nyingi kufikiria juu ya akili?

  ReplyDelete
 3. Kamala, Chacha Wambura aka Ng,wanambiti yuko wapi siku hizi? Sijamsikia siku nyingi. Mwambie namtafuta!

  ReplyDelete
 4. Ningepewa fursa ya kuchagua watu 10 walio wapuuzi zaidi katika nchi yangu, ingekuwa rahisi sana kuliko ya kuchagua wale wenye akili.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU