NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, June 30, 2009

WAMAREKANI WANAJIANDAA KUONDOKA IRAK - JE, WAMESHINDA VITA?

Pamoja na kuongezeka kwa mashambulizi ya mabomu ya kujitoa mhanga kwa wiki za karibuni, majeshi ya Marekani leo yanaanza kuondoka katika miji mingi ya Irak na kuwaachia wanajeshi wa Irak ulinzi wa miji hiyo. Haya ni maandalizi ya mwanzo kwa majeshi hayo kuondoka kabisa katika nchi hiyo kama alivyoahidi rais Obama katika kampeni zake wakati wa uchaguzi. Lakini je, wameshinda vita hivyo? Je, wamepata walichokuwa wamekifuata huko, ambacho wachambuzi wengi wanaamini ni mafuta? Baada ya kupoteza wanajeshi wao zaidi ya elfu nne (tazama hapa) na fedha zaidi ya dola trillioni tatu (huku uchumi wao ukianguka), pamoja na kujivunjia heshima duniani kote (ingawa hawajali) , nini wamepata katika kampeni yao ya Irak?

Ni ajabu jinsi kiongozi mmoja mwenye mawazo na msimamo uliopogoka anavyoweza kuiingiza nchi katika hatihati isiyo ya lazima.

JE, WAGOGO WATAFAIDIKA NA UBUYU WAO?

Baada ya utajiri wake kunyonywa na wageni kwa muda mrefu, Afrika sasa inakabiliwa na ukoloni mpya - ukoloni wa kibayolojia na kiikolojia. Makampuni ya madawa na vyakula ya nchi za Kimagharibi sasa yanakimbilia kujimilikisha (kwa kuchukua hati miliki) mimea ya Kiafrika ambayo ina manufaa ya kitiba na kilishe. Mfano ni Hoodia - mmea kutoka jangwa la Kalahari na ambao unasaidia kuzima hamu ya kujisikia njaa. Inavyoonekana mbuyu (Adansonia Digitata kwa jina la kisayansi) nao utachukuliwa hivi karibuni. Nasi Waafrika kama kawaida yetu tumekaa tu tunaangalia. Katika makala haya ninauliza: kama ubuyu utaanza kuuzwa kama zao la Kibiashara kimataifa, Wagogo ambao ni wenyeji wa Dodoma ambako mibuyu mingi inapatikana (na Waafrika kwa ujumla) wataambulia cho chote? Inabidi wataalamu wa biashara na sheria za Kimataifa waliangalie suala hili la makampuni ya Kimagharibi kujimilikisha mimea yetu na kuhakikisha kwamba Waafrika hawaachwi kwenye mataa tena kama ilivyotokea katika madini na rasilimali nyinginezo za bara lao tajiri. (Makala imechapishwa katika gazeti la Kwanza Jamii la Leo nami naitundika hapa kama ilivyo)
====================================================
Wagogo Watafaidikaje na Biashara ya Ubuyu?
Na Dkt. Masangu Matondo Nzuzullima

Afrika kwa hakika ni bara la ajabu. Kwa upande mmoja, ni bara tajiri pengine kuliko mabara mengine yote ulimwenguni. Kwa upande wa pili, Afrika pia ni bara masikini pengine kuliko mabara mengine yote. Hali hii kanganyifu wazungu huwa wanaiita “paradox” Ati, inawezekanaje uwe tajiri nambari wani na wakati huo huo uwe masikini nambari wani? Hili linawezekana tu kama umewaachia watu wengine wakunyonye na wautumie utajiri wao kwa faida yao; na kukuacha wewe ukiwa huna kitu. Ndivyo Afrika inavyofanya, au tuseme inavyokubali ifanyiwe.

Pamoja na utajiri wake wa maliasili (madini, mapori, wanyama wa kila aina, watu, bahari, maziwa, mito, ardhi n.k.) Afrika bado ni masikini kwa sababu utajiri wake hauusaidii umma wake wa wakulima na wafanyakazi katika kuleta maendeleo ya kweli. Kwa mtazamo mmoja utajiri huu umegeuka kuwa kama “laana” kwa bara la Afrika kwani ndiyo hasa ulikuwa chanzo cha Afrika kutawaliwa. Wakati wa biashara ya utumwa Waafrika wenyewe waligeuzwa bidhaa wakauzwa mnadani kwenda kuzalisha malighafi zilizohitajika Ulaya. Malighafi hizi ndizo zilizochochea mapinduzi ya viwanda na hatimaye ukingunge wa nchi za Ulaya katika sayansi, teknolojia, uchumi na utamaduni. Wakati wa ukoloni, Afrika iliingizwa rasmi katika mfumo wa uchumi tegemezi ambamo ilijikuta (kama asemavyo Walter Rodney katika kitabu chake cha How Europe Underdeveloped Africa) ikizalisha isichokifaidi na ikifaidi isichokizalisha. Kuanzia hapo Afrika ilipoteza rasmi umiliki wa malighafi zake ambazo uzalishaji wake sasa ulidhibitiwa na mabwana kutoka Ulaya. Hata bei za malighafi za Afrika zikawa zinapangiwa Ulaya bila kujali hali halisi ilivyo Afrika kwenyewe. Malighafi hizo zilizalishwa na kuuzwa kwa bei ya chini sana lakini zilipofikishwa Ulaya na kubadilishwa kuwa bidhaa, bidhaa hizo hizo zilirudishwa Afrika na kuuzwa kwa bei ya juu sana. Kwa hali hiyo mabepari wa Ulaya waliweza kujitajirisha huku Waafrika ambao hasa ndiyo wenye mali ghafi wakiendelea kusikinika.

Baada ya uhuru mabepari wa Kimagharibi walihakikisha kwamba wanaweka tabaka lao la vibwanyenye kushika hatamu katika nchi nyingi za Kiafrika, tabaka ambalo lilihakikisha kwamba mfumo huu tegemezi wa kiuchumi waliouanzisha unadumishwa na kuimarishwa. Viongozi “vichwangumu” ambao walisitasita kufuata mfumo wa kibepari na hivyo kugoma kuwa vibwanyenye wa wakubwa wa Ulaya ama walipinduliwa au waliuawa. Hiki ndicho kilichowapata akina Kwame Nkrumah wa Ghana, Patrice Lumumba wa Kongo na wengineo. Mfumo huu wa “aliyenacho ataongezewa na yule ambaye hana hata kile kidogo alichonacho atanyang’anywa” ndiyo umetawala duniani na baada ya miaka 60 ya uhuru, hali haijabadilika na utajiri wa Afrika bado unazinufaisha nchi za Kimagharibi (pamoja na tabaka dogo la watawala “viranja” katika nchi nyingi za Kiafrika). Kama unabisha nenda pale mgodi wa almasi wa Mwadui ukaangalie almasi zinazozalishwa pale. Halafu ukitoka nje ya geti la mgodi angalia maisha ya Wasukuma katika vijiji vinavyouzunguka mgodi huo wanavyoishi. Utabakia kujiuliza, almasi yote ile inayochimbwa pale inamsaidia nani? Nilipata bahati ya kutembelea mgodi huo mwaka 1995 na nilipotoka nje ya mgodi ule machozi yalinidondoka baada ya kuona hali za wenyeji ambao almasi zile zinafukuliwa kutoka katika ardhi yao wenyewe – ardhi ya mababu zao! Haya ni makala ya siku nyingine. Sasa tuendelee na mada yetu ya wagogo na ubuyu wao.

Baada ya kupora utajiri wa Afrika kwa muda mrefu, makampuni ya Kimagharibi na hasa yale yanayotengeneza madawa na hata vyakula sasa yanakimbilia kujimilikisha mimea yenye asili ya Afrika ambayo ina manufaa kitiba na kilishe. Ukoloni huu mpya wa kibayolojia na kiikolojia umeyafanya makampuni haya kuanza kuchukua hati miliki za mimea hii ambayo Waafrika wamekuwa wakiitumia kama tiba ya maradhi mbalimbali na chakula kwa muda mrefu. Mfano mzuri ni huu mmea wa Hoodia ambao Wasan - wenyeji wa jangwa la Kalahari kule Namibia wamekuwa wakiutumia kwa muda mrefu kama kizuia njaa. Kampuni moja la Uingereza liitwalo Phytopharm ndilo limejimilikisha hati miliki ya mmea huu na sasa mmea wa Hoodia umegeuzwa zao la kibiashara na mashamba makubwa yamefunguliwa kule Afrika Kusini na jangwani katika jimbo la Arizona kule Marekani. Vidonge vya kupunguza hamu ya chakula (na hivyo kusaidia kupunguza uzito) vinavyotokana na mmea huu (Hoodia diet pills) sasa vinauzwa na kununuliwa sana hapa Marekani. Chupa moja ndogo inauzwa kwa dola 39.95 za Kimarekani. Mwafrika hapa, kama kawaida yake, amepigwa chenga ya mwili na utajiri wake unafaidiwa na watu wengine. Japo Wasan walikwenda mahakamani kudai haki yao, walifikia makubaliano ya muda mwaka 2002 ambapo iliamriwa kwamba walitakiwa walipwe asilimia 8 ya faida yote ambayo kampuni la Phytopharm lilikuwa limepata mpaka wakati ule; na kuanzia hapo wangeendelea kupata asilimia sita (6%) ya mapato yote yanayotokana na mmea wa Hoodia. Hata hapa mtu unaweza kujiuliza: ni nani anayehakikisha kwamba kweli hata hiyo asilimia 6% waliyotengewa wanaipata?

Mmea wa Mbuyu (Adansonia Digitata kwa jina la Kisayansi) inaonekana nao utakumbwa na mkasa kama wa Hoodia (yaani kumilikiwa na makampuni ya Kimagharibi) muda si mrefu ujao. Kwa karne nyingi mmea huu umekuwa ukitumiwa katika sehemu nyingi za Afrika kwa matibabu na shughuli nyingine mbalimbali. Karibu kila sehemu ya mmea huu ina faida – sehemu ya mti hutumiwa kutengenezea kamba na nyavu za kuvulia samaki, majani hutumiwa kulishia wanyama kama mbuzi, kondoo na ng’ombe; shina lake kubwa linaweza kutumiwa kama makazi kwa binadamu, matunda yake ni chakula na tiba. Kule Gambia kwa mfano, inaaminika kwamba mbuyu unatibu malaria, ugumba, pumu, maumivu ya kichwa, meno na magonjwa mengine.

Makampuni ya madawa pamoja na vyakula ya nchi za Kimagharibi yanaunyemelea mmea huu wa mbuyu na kuna imani kwamba siku moja pengine unaweza kuwa ndiyo chanzo kimoja kikuu cha madawa na chakula. Imeshathibitishwa kisayansi kwamba ule unga mweupe katika matunda ya mbuyu una faida lukuki: Una antioksidanti (antioxidants), potasi (potassium) na fosforasi kwa wingi, vitamini C mara sita zaidi ya juisi ya machungwa na kalisi (calcium) mara mbili zaidi ya ile inayopatikana katika maziwa ya ng’ombe. Majani yake yana madini ya chuma, potasi, maginesi (magnesium), manganizi (manganese), fosforasi na molybdenum kwa wingi sana. Mbegu zake pia zina protini ya kutosha. Kwa uchambuzi wa kisayansi kuhusu madini yaliyomo katika mbuyu pamoja na bidhaa mbalimbali zinazotokana na mbuyu soma makala ifuatayo (pdf)

Kutokana na faida zake hizi, (linaripoti gazeti la New York Times la tarehe 26/5/2009) bidhaa zinazotokana na mbuyu zimeruhusiwa kuingizwa sokoni katika nchi za Jumuia ya Ulaya kuanzia mwaka jana na shirika la viwango la madawa na vyakula la Marekani (Food and Drug Administration) linategemewa kutoa ruhusa mwaka huu kwa bidhaa hizo kuingizwa na kuanza kutumiwa hapa Marekani. Sehemu ya ndani ya tunda la mbuyu itauzwa kama kiungo muhimu katika “smoothies” na “cereal bars”. Tayari kikopo kidogo cha jamu iliyotengenezwa kutokana na mbuyu kinauzwa kwa dola 11 za Kimarekani kule Uingereza. Kulingana na tathmini ya Natural Resources Institute ya Uingereza, biashara ya kimataifa ya ubuyu inaweza kuzalisha dola za Kimarekani zaidi ya bilioni moja (sawa na shilingi za Kitanzania 1,300,000,000,000) kwa mwaka pamoja na kutoa ajira kwa familia za Kiafrika zipatazo milioni mbili na nusu.

Niliposoma makala haya kutoka gazeti la New York Times na kuona faida na mategemeo makubwa ya kibiashara ya mmea huu wa mbuyu niliwakumbuka marafiki zangu Wagogo kutoka Dodoma ambako kama sikosei ndiko kuna mibuyu mingi kuliko sehemu nyingine hapa Tanzania. Kama mmea huu utaanza kuzalishwa kibiashara natumaini kwamba Tanzania haitabaki nyuma na kwamba wazalishaji wa zao hili watawezeshwa ili hatimaye waweze kufaidika na kuuona uhalisi wa sera ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Kama Kahawa ilivyoweza kuwanufaisha wenyeji wa mikoa ya Kilimanjaro, Kagera na Mbeya, bila shaka zao hili la Ubuyu pia litaweza kuwanufaisha wenyeji wa mkoa wa Dodoma na kwingineko linakopatikana. Nchi za Kiafrika ni lazima ziamke na kupambana na ukoloni huu mpya wa kibayolojia na kiikolojia; na kuhakikisha kwamba mimea hii yenye faida kubwa (kama hoodia na mbuyu) ambayo ni mali ya watu wake ambao wamekuwa wakiitumia kwa muda mrefu kama tiba (ambazo wazungu hao hao waliziita sehemu ya utamaduni wa kishenzi) inalindwa na kubakia mali ya Waafrika. Hata kama ikianza kutumiwa kibiashara kama ilivyotokea kwa Hoodia na pengine mbuyu (Adanjsonia Digitata), basi uandaliwe utaratibu ambao utahakikisha kwamba marafiki zangu Wagogo wanafaidika na ubuyu wao. Vinginevyo, baada ya kumiliki almasi, dhahabu, tanzanite na utajiri mwingine wa bara letu, walafi hawa wa Kimagharibi kamwe hawatosheki na kama wakiweza wataweza kumiliki kila kitu kilicho chetu. Ni lazima tuwaambie kwamba Hoodia, Mbuyu na Mwarobaini ni vyetu na sisi ndiyo tunastahili hiyo hati miliki.

Monday, June 29, 2009

SIMU ZA MKONONI TANZANIA KUSAJILIWA KUANZIA JULAI MOSI

Inaonekana sasa ile tabia ya kumiliki namba za simu hovyo hovyo itapungua kama siyo kwisha kabisa. Hii itasaidia pia kuweza kumfuatilia mmiliki wa simu mathalani simu yake inapotumiwa vibaya mfano katika shughuli za kihalifu. Huu ni utaratibu mzuri kama kweli utatekelezwa kwa dhati!

Saturday, June 27, 2009

Friday, June 26, 2009

THRILLER - NA MAREHEMU MICHAEL JACKSON

Kijana huyu mweusi alikuwa na kipaji cha pekee; na kama angetaka angeweza kuwa (Mmarekani) Mweusi mashuhuri kuliko wote duniani. Ninakumbuka mara yangu ya kwanza kuiona video yake ya Thriller nilikuwa kidato cha kwanza, na mpaka sasa imebakia kuwa moja kati ya kazi bora kabisa za kisanii. Kazi hii ilikibainisha kipaji chake kisichopimika kwa njia ya kipekee.

Lakini kama kawaida yetu sote tuliozaliwa, hatimaye safari yake hapa duniani imefikia kikomo (Michael Jackson 1958 - 2009). Hebu basi na apumzike kwa amani. Hapa chini ni video yake ya Thriller pamoja na mashairi yake.


video

Thriller lyrics

Songwriters: Temperton, Rod;

It's close to midnight and something evil's lurking in the dark
Under the moonlight, you see a sight that almost stops your heart
You try to scream but terror takes the sound before you make it
You start to freeze as horror looks you right between the eyes
You're paralyzed

'Cause this is thriller, thriller night
And no one's gonna save you from the beast about strike
You know it's thriller, thriller night
You're fighting for your life inside a killer, thriller tonight

You hear the door slam and realize there's nowhere left to run
You feel the cold hand and wonder if you'll ever see the sun
You close your eyes and hope that this is just imagination, girl!
But all the while you hear the creature creeping up behind
You're out of time

'Cause this is thriller, thriller night
There ain't no second chance against the thing with forty eyes, girl
Thriller, thriller night
You're fighting for your life inside a killer, thriller tonight

Night creatures calling, the dead start to walk in their masquerade
There's no escaping the jaws of the alien this time
(They're open wide)This is the end of your life
They're out to get you, there's demons closing in on every side

They will possess you unless you change that number on your dial
Now is the time for you and
I to cuddle close together, yeah
All through the night I'll save you from the terror on the screen
I'll make you see

That this is thriller, thriller night
'Cause I can thrill you more than any ghost would ever dare try
Thriller, thriller nightSo let me hold you tight and share a
Killer, diller, chiller, thriller here tonight

Cause this is thriller, thriller night
Girl, I can thrill you more than any ghost would ever dare try
Thriller, thriller nightSo let me hold you tight and share a killer, thriller, ow!

(I'm gonna thrill ya tonight)
Darkness falls across the land
The midnight hour is close at hand
Creatures crawl in search of blood
To terrorize y'alls neighborhood

I'm gonna thrill ya tonight, ooh baby
I'm gonna thrill ya tonight, oh darlin
'Thriller night, baby, ooh!

The foulest stench is in the air
The funk of forty thousand years
And grizzly ghouls from every tomb
Are closing in to seal your doom

And though you fight to stay alive
Your body starts to shiver
For no mere mortal can resist
The evil of the thriller

Thursday, June 25, 2009

"ARE MEN WIRED TO CHEAT?"

Hii ilikuwa ni mojawapo ya mada kuu katika kipindi cha "Science of Sex" kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Discovery Channel hivi karibuni. Swali hili limezuka tena hapa Marekani baada ya Mark Sanford - Gavana wa jimbo la South Carolina mwenye mke na watoto wanne "kupotea" kwa siku kadhaa huku familia yake na watu katika jimbo lake wakiwa hawajui aliko. Baadaye wafanyakazi katika ofisi yake walidai kwamba Gavana alikuwa amekwenda kuteleza katika barafu katika milima ya Appalachians.
  • Jana gavana mwenyewe akaibuka na kukiri kwamba hakuwa akiteleza milimani bali alikuwa ametimkia Buerno Aires Argentina kwa nyumba yake ndogo. Sanford ndiye alikuwa mwenyekiti wa chama cha magavana wa chama cha Republican (mpaka jana alipojiuzulu wadhifa huo) na alikuwa anategemewa kugombea uraisi mwaka 1012 dhidi ya Obama. Kama kawaida ya Republican gavana huyu pia alikuwa ni mpigania familia, mpinzani mkali wa mambo ya kishoga, usagaji, mapenzi nje (na kabla) ya ndoa na kila kitu kinachotishia uhai wa familia kama taasisi ya kijamii.
  • Swali ambalo watu wengi wanajiuliza ni hili: Kwa nini mtu mashuhuri kama mwanasiasa huyu mtegemewa anaamua kuwa na nyumba ndogo wakati akijua kabisa kwamba maisha yake ya kisiasa, umashuhuri, madaraka, pesa, heshima na kila kitu alichopigania katika maisha yake kitakwenda na maji?
  • Katika kipindi cha Discovery Channel wanasayansi waliofanya utafiti wa kina walifikia hitimisho kwamba binadamu ni mnyama na tukitaka kufahamu jambo hili ni lazima tuangalie wanyama wengine wanavyoishi. Kwa kifupi sana ni kwamba inavyoonekana kila mnyama wa kiume analo lengo kuu moja kimaumbile - kusambaza "genes" zake kwa wingi kwa kadri inavyowezekana kabla hajafa; na tabia ya wanaume kuwa na nyumba ndogo na wapenzi wengi inawezekana ni kutaka kutimiza jukumu hili la kimaumbile. 
  • Hitimisho? Si jambo la kushangaza mwanaume akiwa na nyumba ndogo au kuwa na wapenzi wengi na kwa kawaida, walihitimisha wanasayansi hawa, tamaduni nyingi zinaruhusu jambo hili na ni shida kidogo kwa mwanaume kuridhika na mwenzi mmoja tu kimapenzi katika maisha yake yote. Kufanya hivyo kunamfanya ajione kama "failure" katika mashindano ya kimaumbile ya kusambaza "genes" zake kwa wanawake wengi kwa kadri inavyowezekana. Kuna mnyama mmoja tu ambaye ndiye amethibitika kwa asilimia 100 kuwa na mwenzi mmoja tu katika maisha yake yote - mnyoo fulani unaoishi katika matamvua (gills) ya samaki!
  • Hata hivyo, walionya wataalamu hawa, utafiti wao usitumiwe kama kisingizio na wanaume kuwa na nyumba ndogo. Walisema kwamba, kinyume na wanyama wengine, binadamu anao uwezo wa kuishinda hulka hii ya kimaumbile, na katika jamii ambazo hazikubaliani na mfumo wa wanaume kuwa na wanawake au wapenzi wengi, mwanaume anategemewa kuwa na mwenzi mmoja tu.
Kwa habari zaidi, soma makala hapa chini.
======================================


Are we wired to cheat on our mates?
Biologists say we should not be too surprised by spouses who have affairs

By Mike Celizic, March. 19, 2008

For one species of flatworm that lives in the gills of freshwater fish, monogamy is the rule. But for humans and every other living creature, biologists believe nature prefers that man and beast have multiple sexual partners.

With that in mind, some biologists say we shouldn’t be too surprised when public figures like former New York Gov. Eliot Spitzer and others get caught cheating on their mates.

We may just be wired that way.

“Nature wants one thing, and what it wants are babies,” Jeffrey Kluger, TIME magazine’s science editor, told TODAY’s Meredith Vieira on Wednesday. “It also wants lots of them and it wants variety, because the greater the genetic variety, the greater the likelihood that the babies are going to survive to adulthood and do well. So even when we’ve had children, we have some very primal software that keeps telling us, ‘Look around.’ ”

Once upon a time, biologists thought that there were a number of animals — eagles, geese and beavers among them — that remained monogamous throughout their lives. But DNA testing has shown that even the animals that look like the models of fidelity are getting out at night for a little extra on the side. And, according to a report filed by TODAY’s Natalie Morales, the list of officially monogamous creatures is down to one — that freshwater flatworm that physically attaches itself to a mate for life.

“Men will look for women who look like they’re young and fecund,” Kluger added. “And women look for men who look like they’re good providers, which is why rich and powerful men do well.”

Even in human societies, Americans are relatively unique in their expectation of lifelong fidelity, said University of Texas psychologist and author David Buss.

“Historically, most cultures are polygynous, meaning men are legally entitled to take multiple wives, and so mating with many women is very common across cultures and perfectly acceptable in many cultures,” he said from Austin, Texas. “Our culture is somewhat unique in that we have presumptive monogamy or legal monogamy — men are only supposed to have one woman.”

Vieira wondered whether we haven’t evolved beyond our biological impulses, and both men agreed that humans do have the ability to override their genetic and biological programming. And, studies show, most people do, with 65 percent of men and 75 percent of women claiming that they have never cheated on their spouses.

“If you look at marriages, in fact, more than half of them — in America anyway — do remain monogamous,” Buss said. “I think it’s important to keep in mind that although we do have these biological impulses to stray, we also have inhibitions against straying, for example, reputational damage. When people get caught straying, they incur reputational damage, and we are very concerned about our social reputations.”

The conflict between desire and morality was famously defined by former President Jimmy Carter, who told Playboy that he felt “lust” in his heart, and was roundly criticized for admitting even that.

But, Buss said, Carter was making an important point. “It’s a reflection of reality,” he said. “I think it’s also important to keep in mind that both men and women experience lust in their hearts. They feel attractions to others.”

Both scientists agreed that while women do cheat, men are more likely to.

“There are two reasons for that,” Kluger said. “First of all, men simply can breed more. Men biologically can conceive a child every day if they wanted to. So we’re trip-wired for that kind of thing.”

Above the rules?

The way society is structured also adds to a male’s incentive to cheat. “We still live in a patriarchal society, which means men are more commonly in positions of power,” Kluger went on. “Positions of power tend to validate the belief that you’re above the rules. You and I don’t get a motorcade when we go places. We don’t get a flying wedge on the sidewalk. So if you’re entitled to the sidewalk and you’re entitled to the street, why aren’t you entitled to that beautiful woman on your communications staff?”

Buss said that although the urge to cheat is universal, people with certain personality traits are more likely to stray than others.



“Our studies find two in particular,” said Buss in addressing those traits. “One is impulsivity or lack of conscientiousness. But the most important personality characteristic is narcissism. Men who are high on the narcissism personality characteristic are more likely to cheat than men who are lower. They put their own needs and their own urges before those of their families.”

Both agreed that “biology made me do it” isn’t an excuse for infidelity.

“We have to be realistic about our human nature. We have these impulses to stray,” said Buss. “But we also have inhibitions against straying and the ability to choose whether or not we do.”

Makala hii inapatikana HAPA.


Wednesday, June 24, 2009

MVULANA ALIYETAKA BAISIKELI KUTOKA KWA MUNGU

...na Mungu "alipokawia" kumpa hiyo baisikeli, alibadilisha mikakati. Mwanzoni nimecheka lakini nilipotafakari vizuri niliona kuna ujumbe muhimu kumhusu Mungu na jinsi anavyogawa mibaraka na misamaha yake kwa sisi waja wake. Naogopa kutafsiri nisije nikaharibu uhondo!
=== ==== === === ===
A priest was asking a young boy about his views on religion.

"Well, priest," the boy said.
"I used to pray for a bike, then I realized God doesn't work that way."

The priest nodded with approval. "What else, my child?"

"Well, priest," the boy continued

"Instead of praying for a bike, I stole one and decided to pray for forgiveness instead."

Tuesday, June 23, 2009

JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINARUDI TENA RASMI !!!

Nimeyaona haya makala katika gazeti la Habari Leo la leo (Juni 23, 2009) na inavyoonekana Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linarudi tena rasmi. Lengo la uamuzi huu, kama alivyofafanua Waziri Mkuu, ni "kujenga jamii ya vijana watakaoshiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali vijijini na mijini, ulinzi wa taifa, na kuonyesha mfano katika kujitegemea". Swali ni kwamba - jeshi hili ni kweli litatimiza lengo lake kuu sawasawa? Je, lengo hili kuu linaendana na mazingira ya sasa ambayo yanamzunguka kijana wa Kitanzania? Tunaposema vijana wetu wawe "mfano katika kujitegemea" tunamaanisha nini? Ati, siasa yetu ya Ujamaa na kujitegemea bado iko hai?

Mimi sina ugomvi na JKT. Nilikata mwaka mzima pale Makutupora JKT, Dodoma (Operesheni Miaka 30 ya Uhuru); na kusema kweli nilipenda uzoefu na mafunzo niliyoyapata pale. Hata kama ningekuwa na mtoto wa kiume ningehakikisha kwamba anakwenda JKT - na hasa hawa vijana wa kizazi cha dot.com. Kupiga kwata, kumwagilia maji nusu eka ya bustani, kupalilia mizabibu, kuchunga ng'ombe, kukata kuni, kufyatua matofali na kuyachoma, kujenga nyumba, kukesha usiku katika lindo na mengineyo pengine yatawarudisha kidogo katika mambo halisi katika jamii yetu na kuwakumbusha kwamba haya ndiyo maisha halisi wanayoishi Watanzania wengi kule vijijini.

Ni lazima niseme pia kwamba sikupenda waliyokuwa wakitendewa mabinti - hasa katika ile miezi mitatu ya mwanzo wakati mambo bado yako moto moto; na ningekuwa na wasiwasi sana kama ningekuwa na binti ambaye angetakiwa aende JKT. Kutokana na uwazi uliosababishwa na vyombo vya habari, pamoja na mwamko mzima katika jamii naamini pengine mambo sasa yameshabadilika - na kwamba sasa hii itakuwa ni JKT mpya na ya kizazi kipya - itakayoendeshwa kwa uwazi, kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya!

Makala ya gazeti ni kutoka blogu ya Kennedy

Monday, June 22, 2009

WATU WAPUNGUE MISAFARA YA VIONGOZI - JK

Baada ya mjadala mkali uliozuka baada ya makala ya Profesa Mbele kuhusu safari za nje za Rais Kikwete (bofya hapa), nimefurahi kuona kwamba Rais mwenyewe ameagiza idadi ya watu katika safari hizo ipunguzwe. Mimi nadhani hii ni hatua nzuri kwani itasaidia kupunguza gharama za safari hizo ambazo naamini zinafanyika kwa maslahi ya taifa na si vinginevyo. Soma makala hapa chini.

JK Aagiza Watu Wapungue Misafara ya Viongozi

Imeandikwa na Oscar Mbuza, Dodoma
(Gazeti la Habari Leo, Juni 19 2009)

Rais Jakaya Kikwete ameagiza kupunguzwa kwa idadi ya watu katika msafara wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu katika safari za nje ya nchi ili kupunguza gharama. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliliambia Bunge jana kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kuonekana kuwa Sh bilioni nane zilizotengwa mwaka jana kwa kazi hiyo ya safari hazitoshi.

Alisema hatua hiyo inafanya mamlaka husika kuanza kuangalia namna nzuri ya kuandaa watendaji wanaopaswa kufuatana na Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Alisema utaratibu unaotumika katika kuchagua nani afuatane na viongozi wa juu wanaposafiri unazingatia vigezo mbalimbali kama vile wapambe wa viongozi, maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao hawana budi kufuatana na viongozi kwa mujibu wa itifaki.

Alisema pia wapo viongozi wanaoteuliwa kujiunga na misafara hiyo kutokana na kusudio na madhumuni ya safari ambapo uteuzi hufanywa na ofisi za viongozi hao kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa upande wa Zanzibar na Ofisi ya Spika kwa upande wa wabunge.

Alisema katika uteuzi huo, vigezo vya jinsia, uwakilishi kutoka pande zote mbili za Muungano na wa kambi ya Upinzani huzingatiwa. Alisema kila wakati viongozi wakuu wanaposafiri nje ya nchi, waandishi wa habari wamekuwa wakijumuishwa katika misafara hiyo na inapotokea kuwa viongozi wamekaribishwa kutembelea nchi jirani, basi wakuu wa mikoa inayopakana na nchi hizo huteuliwa kufuatana na viongozi.

Alisema kwa kuzingatia vigezo hivyo, makundi ya viongozi yanayofuatana na viongozi wakuu wa nchi ni mawaziri wa pande zote za Muungano, wabunge na watendaji wa idara mbalimbali za Serikali kutegemeana na madhumuni ya ziara. Waziri Membe alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Zulekha Yunus Haji (CCM), aliyetaka kujua ni utaratibu gani unaotumika kuchagua viongozi wanaofuatana na Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu katika ziara nje ya nchi.

Friday, June 19, 2009

HIKI CHOO NIMEKIPENDA

Hebu tazama ubunifu huu wa Mwafrika - choo safi kabisa (tena inavyoonekana ni cha "kisasa") ndani ya mbuyu. Hapa hakuna haja ya kiyoyozi wala kipasha joto bali necha ndiyo inatawala.

Mbuyu umekuwa ukitumiwa kama makazi na makabila mengi yanayoishi sehemu kame ambako ndiko hasa mmea huu unastawi vizuri mf. Watindiga na Wafulani. Kuweka choo cha kisasa ndaniye ni kupanua tu matumizi yake ya tangu zamani ingawa si ajabu watu wanaotetea mazingira wakadai kwamba kitendo kama hiki cha kuugeuza mbuyu kuwa choo si kitendo cha kujivunia kwani kinahatarisha maisha yake.

DEGE (BOEING 777) LATUA SALAMA BAADA YA RUBANI KUFARIKI LIKIWA ANGANI

Dege la shirika la ndege la Continental aina ya Boeing 777 likiwa na abiria 247 likisafiri kutoka Brussels kwenda Newark, New Jersey Marekani limetua salama baada ya rubani wake mwenye umri wa miaka 60 kufariki ghafla dege likiwa angani tena juu ya bahari ya Atlantiki. Baada ya rubani huyo kufariki tangazo lilitolewa kama kulikuwa na daktari miongoni mwa abiria na abiria kadhaa walikwenda katika chumba cha marubani. Rubani wa ziada ambaye kwa kawaida huwa anaambatana na marubani wengine katika safari ndefu kama hii alikwenda na kuchukua nafasi ya rubani aliyefariki. Mpaka dege linatua Newark abiria wengi hawakujua kilichokuwa kinaendelea. Kwa habari zaidi bofya hapa.

Tarehe 29 Machi, 2009 rubani wa ndege ya shirika la ndege la Precision liyokuwa inaruka kutokea Mwanza kwenda Kilimanjaro (KIA) alipoteza fahamu baada ya ndege kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza. Inavyoonekana kulikuwa na msukosuko mkubwa kwenye ndege baada ya tukio hili. Tembelea hapa kusoma maelezo ya abiria mmoja (anayejitambua) aliyekuwa katika ndege hiyo. Kwa watu kama mimi ambao hatujitambui sawasawa na ambao tunaogopa kusafiri kwa ndege sijui hii ingekuwa na athari gani kwetu kisaikolojia. Kamala, tunahitaji msaada wako hapa!

Tuesday, June 16, 2009

ATI, ZE UTAMU IMETUFUNDISHA NINI???

Makala hii imetoka katika gazeti la Kwanza Jamii la leo (16/6/2009). Naiweka hapa kama ilivyo.

ZE UTAMU IMETUFUNDISHA NINI?

Na Dkt. Masangu Matondo Nzuzullima

Alhamisi tarehe 23/4/2009 rafiki yangu mmoja kutoka Dar es salaam alinitumia barua pepe ya kushangaza. Alikuwa analalamika kuhusu tovuti moja iliyokuwa ikiitwa Ze Utamu. Alisema kwamba tovuti hiyo mashuhuri sana ilikuwa ni tovuti ya hatari na ilikuwa imesababisha madhara makubwa katika jamii. Katika barua pepe hiyo alisema kwamba watu Dar es salaam walikuwa hawalali kwani hawakujua kama kesho yake wangejikuta wametamuishwa (kutundikwa katika Ze utamu) ama la. Kwa ujumla mambo hayakuwa shwari. Aliendelea kushangaa ni kwa nini serikali ilikuwa imeiachia tovuti kama hiyo kuendelea kuchafua amani na utangamano wa wanajamii.

Siku hiyo hiyo, gazeti la Majira lilikuwa na makala yenye kichwa cha habari "Waendesha mtandao Ze Utamu wasakwa, Ni baada ya kuwadhalilisha viongozi". Habari hizi pacha zilinitatanisha na kuniachia maswali mengi. Je, hii Ze Utamu ilikuwa ni tovuti ya aina gani na ilikuwa inaandika habari zipi mpaka kulisukuma jeshi la polisi kuacha shughuli zake muhimu za ulinzi wa raia na kuanza kuwasaka wamiliki wake? Niliikumbuka Jambo Forum ambayo nayo katika kilele chake ilileta kizaazaa mpaka wamiliki wake wakakamatwa na jeshi la polisi. Bila kupoteza muda nilikimbilia kwenye google na baada ya sekunde chache tu niliweza kuipata hiyo Ze Utamu. Nilichokiona kilinishangaza kwani sikujua kama Tanzania tulikuwa tumepiga hatua kubwa namna ile katika uhuru wa vyombo vya habari. Japo mitandao ya udaku imezoeleka sana katika nchi za Magharibi ambako kusema kweli hakuna mtu anayeshangazwa nayo tena, Ze Utamu kidogo ilikuwa tofauti. Hata huku kwa wazungu, sijawahi kuona mtandao ambao lengo lake ni kutukanana na kuchafuliana majina na hadhi. Kinyume na mitandao iliyotangulia kama vile Jambo Forum ambayo ilijikita zaidi kushambulia tabaka fulani la watu katika jamii, Ze Utamu yeye alikuwa hachagui tabaka la mtu wala nafasi na hadhi yake katika jamii – si matajiri, si masikini, si wanawake, si wanaume, si wazee, si vijana, si viongozi, si waongozwaji, si mafisadi, si wasafi – kila mtu alikuwa sawa mbele yake. Kinyume na nchi za Kimagharibi, mitandao na magazeti ya udaku huwa hayatiliwi maanani sana na wasomaji; na mara nyingi hakuna anayejihangaisha na kutaka kuthibitisha habari yanayoziandika. Gazeti la udaku la Globe kwa mfano limekuwa likiandika mara kwa mara habari zinazodai kwamba Obama ni shoga na kwamba aliwahi kuwa na mpenzi mwanamme wakati akiwa bado seneta (tazama hapa). Kila mtu anajua kwamba habari hizi ni za uwongo na hakuna anayezijali wala kuzitilia maanani hapa Marekani. Hii ndiyo tofauti kubwa na nyumbani ambako watu bado wanadhani kwamba kila kitu kinachoandikwa katika magazeti au katika mtandao basi ni cha ukweli. Kama hili lingeeleweka, tovuti kama Ze Utamu isingeweza kuwa mashuhuri na kufikia hatua ya kuwanyima watu usingizi.

Ze Utamu ilikuwa nini?

Kimsingi, inavyoonekana Ze Utamu ilikuwa ni tovuti ambayo (kama walivyodai waendeshaji wake) ilikuwa na lengo la kurekebisha tabia za wanajamii wote bila kujali nafasi zao. Lengo lake kuu lilikuwa ni kupambana na ufisadi - ukiwemo ule wa ngono - na matendo yote machafu yaliyoonekana kukiuka maadili ya jamii yanayotendwa na mtu ye yote katika jamii bila kujali tabaka lake.

Kama tovuti hii ingemakinikia lengo lake hili, kwa hakika ingekuwa chombo makini na cha muhimu sana ambacho kingetoa mchango mkubwa katika kutetea maadili ya jamii ya Kitanzania wakati huu ambapo utandawazi unameza kila kitu kilicho chetu tena kwa kasi ya kutisha. Mitandao na magazeti ya aina hii wakati mwingine yamechangia kuibua kashfa nzito nzito za viongozi katika sehemu mbalimbali duniani. Kwa mfano, John Edwards - mgombea mwenza wa uraisi wa Marekani mwaka 2004 na mgombea uraisi mwaka 2008 kupitia chama cha Democrat alikumbwa na kashfa ya ngono ambayo iliibuliwa kwa mara ya kwanza na mtandao wa gazeti la udaku la National Enquirer. Mwaka juzi waziri mmoja kule Afrika ya Magharibi ilibidi ajiuzulu baada ya picha zake za ngono kuwekwa katika mtandao wa kurekebisha tabia kama Ze Utamu. Mifano hii inaonyesha kwamba mitandao kama hii inaweza kuwa na mchango fulani chanya katika jamii japo kusema kweli faida zake zinakinzwa na uhasi na migongano ambayo mitandao hii inaweza kusababisha katika jamii kama yetu ambako watu bado wanafikiri kwamba kila kitu kinachoandikwa katika mitandao au magazeti ni cha kweli.

Hata hivyo, Ze Utamu ilikuwa imeshalitelekeza jukumu la kurekebisha tabia za wanajamii, na badala yake iligeuka kuwa chuo kikuu cha matusi, majungu, fitina, udaku na husuda. Kama mtu ulimtongoza akakukataa, kama mtu ana maisha mazuri kukuzidi, kama mwenzio alikuzidi kete na kumchukua binti au mvulana uliyekuwa ukimtaka kwa muda mrefu, kama mtu anapendwa na watu kuliko wewe, kama .....basi ulichotakiwa kufanya ni kuitafuta picha yake (hata bila picha ni sawa tu) na kuituma kwa Ze Utamu. Fomyula ilikuwa rahisi sana: sema kwamba ni fisadi (wa ngono), anatembea na watu wengi kwa kujirahisi (unaweza kutaja majina machache), ana UKIMWI na anausambaza tena kwa makusudi, anachukua waume/wake za watu, anapenda vya bure (mteremko), anajiona sana kumbe hana lolote n.k. Halafu waombe "wadau" wamwage data. Na kweli data zingemwagwa na mara nyingi yalikuwa ni matusi ya kutisha ambayo yangeweza kukufanya ufiche uso wako kwa soni. Mara moja moja wadau wangeweza kusimama kidete na kumtetea huyo aliyetamuishwa wakidai kuwa kaonewa, ni mwanajamii makini asiye na ubaya na mtu n.k. Sifa moja ya Ze Utamu hata hivyo ilikuwa ni kwamba mtu ukishatamuishwa basi ulikuwa huachiwi hata utetewe/ujitetee vipi.

Kwa vile hakuna utafiti ambao umekwishafanywa na wanasosholojia au wanasaikolojia kujua hasa madhara ya kutamuishwa katika mitandao ya aina hii si ajabu mtandao huu tayari ulikuwa umeshaleta misukosuko ya kifamilia na kisaikolojia kwa wale ambao walishatamuishwa. Kutokana na matusi mazito yanayoporomoshwa hapo, bila kujali nafasi na tabaka la mtu aliyetamuishwa, watu wengi walianza kuhoji ulikokwenda undugu, umoja, amani, upendo na Utanzania wetu ambao Mwalimu Nyerere alituachia. Wengine walihoji ni kwa nini serikali ilikuwa imeufumbia macho mtandao wa aina hii kwa karibu miaka miwili mizima. Swali la msingi ambalo linaweza kuulizwa hapa ni hili: tumefikaje katika hatua hii ya kutamuishana – sisi Watanzania na Utanzania wetu? Jibu ni rahisi sana - UTANDAWAZI!

Utandawazi na Lengo Lake

Utandawazi ni joka la mdimu lenye vichwa vingi angamizi – vichwa vyenye kazi tofauti tofauti ambavyo lengo lake kuu la jumla hasa ni kuuangamiza utamaduni wetu na hivyo kutufanya tujidharau, tujidogoshe, tusijitambue na hatimaye tuweze kuendelea kutawalika, kunyonyeka na kudhulumika kirahisi zaidi. Ni lazima ikumbukwe kwamba tapo la utandawazi tunalolishuhudia kwa sasa ni mojawapo tu ya matapo mengi ya utandawazi yaliyotangulia, matapo ambayo yalitukutanisha na wageni kutoka Ulaya na kwingineko. Mahusiano yetu na ulimwengu wa wageni hawa kutoka nje tangu mwanzo yamekuwa ya kihasama, kiunyonyaji na dhuluma – kuanzia enzi za biashara ya utumwa mpaka wakati huu tulio nao. Uzalendo, utu na Uafrika wetu ulikunguwazwa na kufishwa wakati wa biashara ya utumwa “tulipokubali” kugeuzwa bidhaa na kuuzwa kama nyanya au vitunguu sokoni. Ni wakati huu ambapo tulipondwapondwa kisaikolojia na kuaminishwa kwamba tulikuwa binadamu wa tabaka la chini ambao kamwe tusingeweza kuwekwa katika daraja moja na “mabwana” kutoka Ulaya na Uarabuni. Vita hivi vya kisaikolojia vilivyopiganwa kwa ujanja sana kupitia dini, sera za lugha na elimu dhidi yetu vilipiganwa kwa nguvu zaidi na “mabwana” wakati wa ukoloni. Ni wakati huu ambapo bara letu liliitwa bara la giza na tamaduni zetu zilizotukuza, kutulea huku zikishabihiana vyema na mazingira yetu ya asili zilibatizwa kuwa za kishenzi na kinyama. Ukoloni ulitazamwa na hata kutambulishwa kama mkakati wa “kutustaarabisha” na kututoa katika giza nene la kuabudu dini za “kishenzi”, kuongea lugha za kishamba na kukumbatia tamaduni zetu za kiwango cha chini. Lugha zetu ambazo kupitia kwazo fikra zetu na mtazamo wetu pamoja na nafasi yetu katika dunia hii vimefinyangwa ziliitwa duni, zikadumazwa na kunyimwa nafasi za matumizi katika sekta rasmi. Matokeo yake lugha zetu ambazo ndizo zinaamua sisi ni nani, nafasi yetu ni ipi katika ulimwengu huu na tunahusianaje na wengine katika mazingira yetu zilinyimwa “meno” na tangu hapo zimebakia kuwa lugha zisizo na mwelekeo wala matumaini. Kulingana na Ngugi wa Thiong’o, ukoloni na utumwa wetu wa kisaikolojia ulikamilika pale tulipokubali lugha zetu kuvishwa sanda na kutengwa na ulimwengu na mazingira yetu. Kuanzia hapo, tulikoma kuwa sisi na kuanzia wakati ule, sisi si sisi tena, hatujijui na hatujui kwamba hatujijui kuwa sisi ndisi. Tumekuwa watumwa wa fikra!

Japo kupatikana kwa uhuru wa bendera kuliwasha moto wa matumaini katika mioyo ya Waafrika, sasa ni wazi kwamba matumaini hayo yalikuwa yametiwa mubaalagha na ahadi za “kuutafuta kwanza uhuru wa kisiasa na uhuru mwingine ungefuata” tulizopewa na akina Kwame Nkrumah wetu zimeshindwa kutekelezeka. Lakini utumwa mbaya kabisa ni ule utumwa wa kisaikolojia - utumwa wa kimawazo uliomdogosha Mwafrika na kumfanya ajione kuwa yeye ni binadamu wa daraja la pili na utamaduni wake kuwa wa kizamani, usioendana na wakati na wa kishenzi. Mkakati mama ulioanzishwa na watawala wetu wakati wa biashara ya utumwa na kuendelezwa (wakati mwingine kwa nguvu) wakati wa ukoloni bado unaimarika siku hadi siku na bado umejikita barabara katika fikra zetu. Na baada ya miaka sitini ya uhuru bado tunaamini kwamba utamaduni wetu na hata lugha zetu ni za kishamba na hazifai kutumiwa katika sekta rasmi kama elimu na vyombo vya habari. Matokeo yake lugha zetu za jadi zimegeuka kuwa lugha za kuonewa haya na kizazi kipya hakitaki tena kuzizungumza. Ati bila lugha na utamaduni wetu wenyewe, sisi ni/tumekuwa/tutakuwa nani?

Kutokana na kutawaliwa kwetu kitamaduni, leo tunakazana sana kuiga utamaduni wa “mabwana” zetu wazungu. Kinashosikitisha zaidi ni ukweli kwamba mara nyingi uigaji wetu umegeuka kuwa mashindano ya kujidharau na tunaiga mpaka kuwazidi hao tunaojaribu kuwaiga. Mifano ni mingi kuthibitisha dai hili (mfano mashindano ya urembo yaliyozagaa kila mkoa, wilaya, mji, tarafa, kata, vitongoji na muda si mrefu pengine yataingia katika familia). Naona hata katika Ze Utamu tulifuata ruwaza (pattern) ile ile – kuiga mpaka kuwazidi tunaojaribu kuwaiga. Nadhani hata wazungu, pamoja na uhuru wao wa habari usio na kikomo, wanayo heshima kidogo kwa viongozi wao na hawawezi kuwa na tovuti mashuhuri ya kizushi ambayo inaweka picha za uongo (zilizofanyiwa photoshop) za viongozi wao wakiwa uchi na watu kuanza kuporomosha matusi mazito. Pamoja na kuishi Marekani kwa karibu miaka 10 sasa jambo hili lilinishangaza na kunisikitisha. Hata kama tovuti za aina hiyo zingekuwepo (au zipo), wenzetu hawa, kinyume na sisi ambao tunaparamia na kuiga mambo kwa pupa, wanajua kwamba huu ni upuuzi tu na hakuna mtu anauyetilia maanani.

“Kiinimacho” cha usawa, Undugu na Umoja

Swali kubwa nililojiuliza baada ya kuiona Ze Utamu ni hili: Moyo wa upendo, umoja, usawa, undugu na mshikamano ambao muasisi wa taifa letu Mwalimu Nyerere alijitahidi sana kuupandikiza mioyoni mwetu ulikuwa wapi? Chuki, uhasama na hasira ya “wadau” katika Ze Utamu ilikuwa ya kutisha na ilikuwa ni vigumu kuamini kwamba hawa walikuwa ni Watanzania waliobahatika kuwa na kiongozi mwanafalsafa, msomi na mwenye welewa mpana aliyepigana kufa na kupona kuangamiza ukabila, matabaka na kuhakikisha kwamba kila mtoto anapatiwa nafasi sawa ya elimu ambayo ndiyo mkakati mama wa ukombozi katika jamii. Je, upendo, usawa, amani, undugu na mshikamano vilivyokuwa vikihubiriwa sana miaka michache tu iliyopita vilikuwa vya kweli au vilikuwa kiinimacho tu kwa Watanzania? Hasira hii ya “wadau” – ambayo ilionekana waziwazi hasa kama mtu aliyetamuishwa alikuwa ni kiongozi, “fisadi” au mtu mashuhuri katika jamii – imetoka wapi? Inawezekana usawa, undugu na umoja vilivyokuwa vikihubiriwa sana vilikuwa ni viinimacho tu? Ati, hali halisi ikoje katika jamii? Ahadi zile za MwanaTANU na baadaye mwanaCCM bado zina ukweli wo wote? Ni kweli kwamba binadamu wote ni sawa au (kama wanyama wanavyogundua katika riwaya mashuhuri ya George Orwell ya Shamba la Wanyama) binadamu wote ni sawa lakini binadamu wengine ni sawa zaidi ya wengine?

Ze Utamu Imetufundisha nini? Tufanye nini?

Mbali na kuionyesha vyema tabia yetu tatanishi na ya kijinga ya kuiga mambo hadi kuwazidi hao tunaojaribu kuwaiga (na hivyo kuthibitisha zaidi utumwa wetu wa kisaikolojia na kitamaduni), Ze Utamu imetufundisha kwamba mambo si shwari katika jamii yetu na watu wana hasira; na kwamba upendo, amani, umoja na mshikamano uliokuwa ukihubiriwa sana ama vilikuwa ni kiinimacho tu au watu wameshtushwa na mfumuko wa matabaka na sasa wamechoka. Niliangalia maoni yaliyokuwa yakiwekwa na “wadau” baada ya mtu mashuhuri, kiongozi au “fisadi” kutamuishwa na niliweza kuiona hasira ya watu ikiwaka moto. Pengine matabaka ambayo tumeyaachia kufumuka kwa kasi ya risasi - ambapo tumewaruhusu watu wachache wajikusanyie “vijisenti” vyote na kuwaacha walio wengi wakiwa hawana kitu yameshatia sumu katika mioyo ya Watanzania na hasira kali inafukuta mumo kwa mumo kama volkeno iliyolala. Tusije tukaiachia volkeno hii iendelee kufukuta mumo kwa mumo kwani siku itakayoripuka Tanzania yetu itakuwa matatani.

Ze Utamu pia imetuonyesha tabia nyingine ambayo tunayo sisi Watanzania. Tunapenda sana kuongea na kupiga porojo na Mswahili hata kama hana hoja au mchango wa maana katika mjadala ni lazima achangie. Tazama kwa mfano mada mbalimbali makini katika blogu mashuhuri ya michuzi na utaona ninachokisema. Hata kama mada iliyoanzishwa ni nzuri, yenye manufaa na inayotaka mjadala hasa na hoja komavu, badala ya kutoa hoja na kujadili kwa heshima na hatimaye kukubali kutokubaliana kiungwana utakuta mara nyingi watu wataanza kubeza, kudharau na kumponda mtoa mada. Mfano mmoja ni mada ya hivi karibuni ya Profesa Mbele kuhusu safari za nje za Raisi Kikwete. Profesa Mbele kama vile Mtanzania ye yote anayo haki ya kutoa maoni yake na kwa vile hii ni topiki ya muhimu basi mtu ungetegemea hoja madhubuti za kuunga mkono ama kupinga. Badala yake hoja hutaziona na mahali pake ni mashambulizi na mengine ni yale wenyewe wanaita “ad hominem” Tabia hii inayokera na ambayo inaashiria uzembe wa kufikiri, kutafakari mambo kwa kina, kujenga hoja madhubuti na kuzitetea, kwa kiasi fulani inaakisi yale yaliyokuwa yakitokea kwenye Ze Utamu – kushambuliana na kudhalilishana. Kwa sisi Watanzania, tabia hii inatatanisha kwani kutokana na malezi yetu na falsafa yetu ya kitaifa tungetegemewa kuwa watu wenye upendo na masikilizano. Kuna chuki mioyoni mwetu na sijui kiini chake hasa ni nini!

Ninapoandika makala haya Ze Utamu haipo tena. Tusije basi tukakaa kitako, tukabweteka na kukenua meno tukidhani kwamba tumeshinda vita. Vita ndiyo tu kwanza vimeanza kwani inawezekana kabisa Ze Utamu wengine na pengine wabaya zaidi watazaliwa. Kwa vile sisi tunaiga kuzidi hao tuwaigao, tusubiri siku vipindi kama Jerry Springer, Maury na Cheaters vitakapofika kwetu. Sijui vitakuwa na sura gani. Tusije tukasahau kwamba adui yetu hasa ni utandawazi na hao “mabwana” zetu wanaotamani kututawala katika nyanja zote za maisha yetu milele na milele. 

Tufanyeje basi ili kuuokoa Utanzania, Uafrika na utu wetu? Kusema kweli si jambo rahisi na hakuna njia ya mkato. Kutokomeza utumwa wa kisaikolojia na kasumba ya kujidharau sisi pamoja na utamaduni wetu, kasumba iliyopandikizwa akilini mwetu kijanja kwa karne nyingi, kasumba inayotufanya tujione kuwa binadamu wa daraja la pili si kazi rahisi. Inabidi tuwe na mkakati mama wa kufufua utamaduni wetu na mahali pazuri pa kuanzia ni katika lugha zetu za kienyeji kwani kama asemavyo Ngugi wa Thiong’o katika kitabu chake cha Decolonizing the Mind, lugha zetu ndizo nguzo hasa za utamaduni wetu na hatuwezi kuwa huru bila kuziheshimu lugha zetu na hivyo kuulinda utamaduni wetu. Wakati sasa umefika wa kuandaa sera makini inayotekelezeka kuhusu uhimizaji na uboreshaji wa lugha zetu - sera ambayo itazipa nafasi lugha zetu za kienyeji kutumika katika sekta rasmi kila inapowezekana. Mfumo wetu wa elimu urekebishwe na elimu tunayowapa vijana wetu ihusiane na mazingira yao. Ni lazima pia tupunguze tofauti za kitabaka kati ya wenye “vijisenti” na masikini walio wengi wanaoshindia mlo mmoja. Afya na mustakabali wa taifa letu unategemea ni kwa jinsi gani tutakavyofanikiwa katika kupunguza pengo kati ya matabaka haya kinzani. Si budi pia tuangalie upya dhana nzima ya maendeleo. Ati, tunaposema maendeleo tunamaanisha nini hasa? Ni lazima tuvumbue dhana mpya ya maendeleo – dhana yetu wenyewe kulingana na mazingira yetu. Yote kwa yote tukumbuke kwamba hivi ni vita vya kisaikolojia. Tukiweza kuwaaminisha vijana wetu kwamba kuongea Kisukuma, Kihaya au Kichaga kwa ufasaha ni jambo la kujivunia, kwamba siyo lazima kuvaa mitepesho kuashiria usasa, kwamba siyo lazima kujikondesha mpaka mbavu zichomoze kuwa mrembo, kwamba rangi nyeusi haina tofauti na rangi zingine na kamwe Mwafrika siyo kiumbe wa daraja la pili basi tutakuwa tumeanza kupiga hatua (japo za kitoto) katika safari yetu ndefu na ngumu ya kujitafuta na kujifahamu upya sisi ni nani na nafasi yetu katika dunia hii ya sasa ni ipi. Kizazi hiki cha dot com ni lazima kiandaliwe mkakati wa kuanza kukirudisha katika kiini cha Uafrika na Utanzania wake.

Waswahili wana msemo unaosema kwamba zimwi likujualo halikuli likakumaliza. Utandawazi ni zimwi lisilotujua – zimwi lililotuparura vibaya sana wakati wa utumwa, likafinyangafinyanga fikra zetu wakati wa ukoloni na sasa, baada ya miaka zaidi ya sitini ya uhuru, linatishia kuumeza kabisa utamaduni na usisi wetu. Kila siku tunapoamka ni lazima tujisaili: Utandawazi ambalo ni zimwi lisilotujua, linaweza kweli kutula lisitumalize? Je, tufanye nini?


Friday, June 12, 2009

MAGAZETI YA UDAKU - OBAMA NI SHOGA!!!

  • Magazeti ya udaku likiwemo hili la Globe yamekuwa yakiandika, tena kama habari kuu katika ukurasa wa mbele kabisa, kwamba Obama ni/alikuwa shoga. Mwanaume mmoja aitwaye Larry Sinclair amekuwa akidai kwamba alikuwa mpenzi wa Obama kwa miaka mingi wakati ule akiwa bado seneta kule jimbo la Illinois; na kwamba walikuwa wanatumia madawa ya kulevya pamoja. Kashfa hizi zilianza zamani wakati Obama bado akiwa mgombea wa uraisi na bado zinaendelea. Larry Sinclair amekuwa akidai kwamba yeye pamoja na mwanaume mwingine shoga aliyekuwa mwimbishaji wa kwaya katika kanisa la zamani la Obama kule Chicago (huyu aliuawa mwaka 2007) waliwahi kuwa na uhusiano wa kishoga na Obama. Hata hivyo alipopewa "polygraph test" ili kuweza kujua kama alikuwa anasema ukweli ama la kuhusu kashfa hizi, alishindwa na matokeo yalionyesha kwamba alikuwa anadanganya.
  • Nyumbani sisi bado tunafikiri kwamba kila kitu kinachoandikwa katika gazeti au kuwekwa mtandaoni ni cha kweli lakini hawa wenzetu wanajua kwamba huu ni udaku na hakuna mtu ambaye anajali. Ndiyo maana Obama aliweza kushinda uraisi pamoja na magazeti haya kuandika udaku wote huu. Siku tutakapoweza kung'amua kwamba mambo mengi yanayosemwa katika magazeti (hasa haya ya udaku yaliyofumuka kila kona ili kuishibisha kiu ya utandawazi) ama si ya kweli au hayajathibitishwa basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa. Nimeandika makala ndefu yenye kichwa "Ze Utamu Imetufundisha Nini?" kuhusu jambo hili na makala hiyo itatoka katika gazeti la Kwanza Jamii la Jumanne tarehe 16/6/2009. Nitaiweka hapa baadaye kidogo.
  • Ishu hii bado inaendelea. Bofya hapa kuona jinsi hawa jamaa wa Globe walivyoishikia bango.

Tuesday, June 9, 2009

MKAKATI SAFI WA KUVIMALIZA VITA VYA IRAQ HARAKA

Pengine hili ndilo suluhisho bora kabisa ambalo nimeshawahi kuliona kuhusu jinsi ya kuvimaliza vita vya Iraq haraka.
========================================
"Why are we still in Iraq? We could end this war tomorrow, it's simple. We build a Wal-Mart, McDonald's, and Krispy Kreme in every village in Iraq. A Starbucks on every corner, and a Hummer dealership in the middle of town. I say it is time we fight evil with evil. How long can you stay angry when you start every day with a hot, frothy latte and freshly glazed Krispy Kreme, driving a Hummer to your job at Walmart? Life is good. It wouldn't be long before they are just as fat and lazy as Americans"
Rand Harken (Mwanakomedi/Mchekeshaji? wa Marekani)

Monday, June 8, 2009

NYUMBA YA KULALA WAGENI YENYE MASHARTI "MAGUMU"

Kama nyumba zote za kulala wageni zingekuwa na masharti "magumu" kama haya, (ambayo Mjengwa amesema kwamba yanakubalika hata Vatican) na zikayatekeleza, pengine zingeweza kutoa mchango chanya katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Picha ni kutoka blogu ya Mjengwa.

Wednesday, June 3, 2009

UJIRANI GANI HUU??? - WAZUNGU KWELI KIBOKO

Naona huyu mzee haamini kama kweli jirani yake anaweza kumfanyia hivi. Lakini kwa wazungu hili si jambo la ajabu. Sisi Waafrika tunayo namna yetu ya kutatua ugomvi na misukosuko - ikiwemo kupigana vijembe kwa kutumia lugha ya mafumbo kupitia kwenye kanga, nyimbo, umbea na kwingineko. Yote kwa yote mnaweza kupigana vijembe na mwishowe mkaanza tena kuombana chumvi na unga pamoja na kuazimana kanga na vipodozi. Ubinafsi wa hawa wenzetu umepindukia kimo - kila mtu na lwake na mkikosana kidogo tu usije ukashangaa akakufanyia kama huyu babu alivyofanyiwa. Na hapo huwezi kumfanya lolote kwani hiyo "decoration" ipo katika yadi yake na ukivuka hilo geti la mbao tayari unakuwa umeingilia himaya yake. Kazi kwelikweli. Halafu eti ndiyo tumekazana kuwaiga hawa jamaa pamoja na tabia zao.

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

BLOGU ZA BURUDANI NA UREMBO