NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 18, 2010

BARAFU IMEUA MICHIKICHI YANGU!

 • Nilipolalamika kuhusu jimbo lenye hali ya hewa ya kitropiki la Florida kukumbwa na barafu (ambayo ni nadra sana), Mzee wa Changamoto alicheka na kusema kwamba hakuona barafu katika picha nilizoweka. Alidhani kwamba nilikuwa nimekosea na kuweka picha zisizohusiana na mada husika.
 • Ukweli ni kwamba barafu hiyo imeleta kizaazaa kikubwa hapa Florida hasa kwa wakulima wa mboga mboga. Kwa kiasi kikubwa, Marekani hupata kiasi kikubwa cha mboga na matunda kutoka jimbo la Florida hasa katika kipindi hiki cha baridi. Kutokana na barafu hii kuharibu kiasi kikubwa cha mboga na matunda, inategemewa kwamba bei za mboga na matunda zitapanda nchi nzima kwa miezi michache ijayo.
 • Kwangu mimi barafu hii imeua kabisa miti yangu sita ya michikichi ambayo nilikuwa nimepanda. Hii ni pamoja na kila kitu katika bustani yangu. Sasa inabidi kuanza upya na safari hii kila mti na ua la kudumu nitakalolipanda ni lazima nihakikishe kwamba linaweza kuvumilia baridi kali.
 • My wife wangu anatoka sehemu zenye migomba na hapa nilijitahidi nikampandia vimigomba-andunje vinne. Vilitakiwa kutoa vindizi mwaka huu lakini kama unavyoweza kuona navyo vimepigwa dafrau na barafu. Inabidi nianze upya!

3 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!January 19, 2010 at 10:57 AM

  pole Dakt. Hivi hiyo michikichi inatoa matunda au ni urembo? na hiyo migomba kadhalika?

  kwa kuwa unahitaji matunda itabidi upande mingine ambayo nayo yawezekana ikapigwa na barafu nyingine mwakani (samahani miye sina ukoo na ng'wanaMALUNDI!)

  vumilia tu baba :-(

  ReplyDelete
 2. Hii michikichi ni kwa ajili ya mapambo tu. Ikikua huwa inapendeza sana. Tatizo ni kwamba inakua polepole sana. Sasa hii yangu iko nyang'anyang'a na sijui kama itafufuka au ndiyo kwisha kazi.

  Unafahamu hata mambo ya Ng'wanamalundi? Huyo ndiye "Yesu" wetu kwani naye alikuwa mkali wa miujiza...ingawa hakudai kuwa mkombozi!

  ReplyDelete
 3. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!January 20, 2010 at 9:34 AM

  Masangu, hivi karibuni ntatembelea pale ambapo Ng'wanamalundi alifia. Nasimuliwa kuwa mmojawapo wa wasaidizi wake (yawezekana alipewa mlungula)alichukua kinyesi cha Ng'wanamalundi akakiweka mahali ambapo mzee Ng'wanamalundi alikuwa anakaa. Mzee Ng'wanamalundi alipokuja na kukuta kinyesi akanyosha kidole chake akikielekeza kwenye kinyesi na kusema 'nani huyu alojisaidia hapa kwenye kiti changu?' The moment alipokinyooshea kile kinyesi kidole alipooza kuanzia miguuni mpaka kiunoni na akamaka "mmnimaliza" na ndo ikawa ugonjwa ulomuua! :-(

  Kama Yesu asingeuawa na wayahudi kwa kusalitiwa na Yuda Iskariote pengine angekuwa hai mpaka leo na kama Ng'wanamalundi asingesalitiwa na mmoja wa wasaidizi wake pengine tungekuwa naye leo....lol

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU