NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, January 15, 2010

HATA FLORIDA KUMBE KUNA BARAFU!!!

 • Kwa mara ya kwanza tangu nihamie hapa Florida, sijawahi kupambana na baridi ya aina hii. Mpaka tumeweza kurashiwarashiwa na barafu na rekodi za baridi za miaka na miaka zimevunjwa. Mimi sijawahi kuishi sehemu ya baridi na hii ndiyo mara ya kwanza kupambana na baridi ya kweli kweli. Najua Mzee wa Changamoto pengine atacheka tu, lakini mimi hata sikujua la kufanya baada ya kukuta gari limefunikwa na unga wa barafu!
 • Unaweza kuona "yard" yote imeota mvi. Maua na miti yote pia nyang'anyang'a! Kuna hatari ya kulazimika kupanda majani na maua mapya mwaka huu.

 • Mabinti walikuwa na wakati mgumu asubuhi wakati wa kwenda shule. Hapa ilikuwa ni baada ya zaidi ya dakika ishirini nzima za kupasha gari moto na kujaribu ku-defrost hiyo barafu. Hapa nilikuwa ninakaribia kuishiwa mbinu wakati mabinti wakizidi kuchelewa kwenda shule. Kazi kwelikweli!

4 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!January 15, 2010 at 9:12 AM

  poleni! yaweza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa a.k.a climate change/global warming iko upenuni mwa eneo lenyu.

  ni makoti kwa kwenda mbele....lol Heri muje upumzike bAriadi japo kuna vumbi :-(

  ReplyDelete
 2. Ha ha ha ha ha!! kazi kwelikweli kwa hiyo itabidi turudi nyumbani kwa hali hiyo. maana naona sasa kila sehemu ni maunga tu inawezekana ni kweli asemavyo Chacha Wanbura ni mabadiliko ya hali ya hewa.

  ReplyDelete
 3. hongereni, Bukoba ni mvua na upepo mkali kiana, hali ya hewa ni tammu kupitia puani!

  ReplyDelete
 4. Nahisi post yenyewe ina maoni yangu. Niliposoma heading kuwa kuna barafu nikasema wacha niiangalie. Kisha nikaona picha nikaanza kufungua email nimwamndikie "mwandishi" kuwa katumia picha zisizo kwenye post hii. Lakini baadae nikaenda kuchukua DARUBINI nikaangalia vema kisha nikaona "vumbi la barafu". Lol
  Well!! Mimi nilipolia na ile barafu yetu iliyofikia karibu futi tatu na ambayo bado haijamalizika kuyeyuka mtaani, rafiki yangu wa Canada akasema hayo ndio maisha yao kwa miezi 4 -6 kwa mwaka na yeye anafanya OVERNIGHT DELIVERY.
  Nikanyamaza maana nilihisi nimetekenya sanamu nikitaraji icheke.
  Nikajiona nisiyejua makubwa, sasa nakutana na hii.
  Hahahahaaaaaaaaaaa
  Karibu baridini familia ya Mwl Matondo
  Poleni na hongereni kwa uzoefu huu mpya

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU