NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, January 7, 2010

HILI NI TUNDA GANI?

 • Tunda hili linapatikana sana katika mikoa ya kanda ya Ziwa (hasa Usukumani na Unyamwezini), mikoa ya kati na sehemu zingine kame kame.
 • Tulizoea kulila wakati ule tukiwa wadogo wakati tunachunga ng'ombe. Mpaka leo nikienda nyumbani huwa naenda porini kulitafuta kama ni wakati wa majira yake. Picha ya huyu bwana mdogo imenikumbusha maisha mazuri ya utoto kijijini miaka ileee! Nimekumbuka!
(...Sikumbuki picha hii niliipata wapi!). Mwenye picha ameshajitokeza. Ni Meshack Maganga wa http://magangam.blogspot.com. Samahani mkuu!!!

14 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!January 7, 2010 at 11:29 AM

  jamani hata mie siujui mti huu labda mnitonye nami pia... :-(

  ReplyDelete
 2. hizo ni gumbalo au?

  ReplyDelete
 3. no si ngumbalo ni yale yanakuwa kama makamasi nimeyasahau jina

  ReplyDelete
 4. kumbukumbu za zamani ni nzuri ajabu tunda si lifahamu

  ReplyDelete
 5. Yanafanana na matunda kule kwetu kusini yanaitwa masuku hsa ubapa wa majani yako.

  ReplyDelete
 6. See my vintage picture blogs:
  http://mynewoldpictures.blogspot.com
  http://mypetarts.blogspot.com
  http://mynaturepictures-benmil.blogspot.com

  ReplyDelete
 7. Du umenikumbusha mbali sana. Haya bwana tunayala sana Singida na yapo kwa wingi sana hasa maeneo ya vijijini. Yanajulikana kama manthong'o kwa kinyaturu, ama matogo kwa kinyaturu cha kimjini.

  Yana utomvu mzuri ili kuupata inabidi utafune kwa muda (kama muwa) na kinachobaki kinatemwa. Matamu sana, yana sukari nzuri ya asili.

  Nakumbuka stori inayofutana na matunda haya...du basi bwana tuishie hapa!

  ReplyDelete
 8. Kule Ndala-Nzega(Tabora) matunda hayo, kwa kinyamwezi cha huko, huitwa ´nohboh´ au ukitamka kwa kinyamwezi-swahili ni ´ntobo´

  Kuna hata kijiji au kata katika wilaya ya Nzega chaitwa Itobo, nafikiri ni kwa sababu ya tunda hilo- sina hakika lakini!

  Asante, unimekumbusha mbali pia,sikuchuga ng´ombe lakini matunda niliyala wakati tulipokwenda porini-vichakani kutafuta kuni

  ReplyDelete
 9. Haa .hii picha uliipata vkwenye blog yangu .ni picha yangu hasa nilipiga picha hii huko Iringa
  http://magangam.blogspot.com

  ReplyDelete
 10. Kule Usukumani (Unyatuzu) tunda hili huitwa NHOBO na kama alivyosema Bwaya inabidi uwe na meno ya uhakika kulila na kulifaudu sawasawa. Likikomaa huwa linapasuka. Inabidi ulitafune sana na likianza kulainika linatoa maji matamu yanayonatanata. Basi unatafuna mpaka hayo maji yanaisha, unatema ganda na kuchukua jingine. Basi unatafuna wee mpaka meno yakuume!

  Bwana Maganga, kule Iringa tunda hili linaitwaje?

  ReplyDelete
 11. hili tunda si mchezo lina sukari ya asili(fructose) ila likikauka linakuwa na tumanyoya tudogo tudogo kama upupu kitu ambacho ni usumbufu kwenye kulila

  ReplyDelete
 12. Matunda haya yapo mengi mkoani iringa na inasadikiwa yanasaidia sana kutia nguvu viungo kama magoti na viwiko vya mikono

  ReplyDelete
 13. Matunda haya yapo mengi mkoani iringa na inasadikiwa yanasaidia sana kutia nguvu viungo kama magoti na viwiko vya mikono

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU