NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 18, 2010

LUGHA ZA MITAANI, KISHENG NA "MUHADHARA"

 • Nilipousikia wimbo huu kwa mara ya kwanza nilishangazwa na jinsi neno muhadhara lilivyotumika. Baadaye nikaambiwa kwamba hili ni neno la Kisheng na kule Kenya linatumika kumaanisha shida kubwa, janga au maafa.
 • Kisheng kimevutia watafiti wengi wa Isimu Jamii kutokana na ubunifu unaojitokeza katika uundaji na mpangilio wake wa maneno. Mpaka sasa imeshindikana kujua hasa Kisheng ni nini kwani si rahisi kukipambanua na kukipa sifa za moja kwa moja. Mpaka sasa bado haijajulikana kama ni lahaja ya Kiswahili, lugha ya mseto, lugha ya mitaani, pijini au Creole.

4 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!January 19, 2010 at 10:32 AM

  hata mie huwa naiongea sana hiyo sheng hasa nikiwa huko kimatembezi ama kikazi kwa kuwa nimikaa Nairobi a.k.a nairobari wakati nasomea upadre ulonishinda!

  ama kwa hakika ukinisikia naongea na mkenya utadhani nami ni mkalee (kalenjini) ama mkeyuu (kikuyu) wa huko.

  nadhani nyie wataalamu mnatakiwa mtutoholee na mtujulishe sheng ni kitu gani.

  na mwisho, WADHANI Tanzania HATUNA LUGHA INAYOFANANA NA SHENG YA KENYA? YAWEZEKANA IKO KILA PAHALA, UGANDA, RWANDA, BURUNDI NA HATA DRC :-(

  Mtafiti basi mtujuze :-)

  ReplyDelete
 2. Kumbe unaongea Kisheng! Basi nikiwa na maswali nitakuwa nakuuliza. Ninaandika makala inayoitwa "Minimality Effects in Sheng and Swahili" na usishangae nikikuomba ufafanuzi wa baadhi ya maneno.

  Inavyoonekana kuna lugha zenye sifa kama za Kisheng katika miji mingi ya Kiafrika - Lusaka, Accra, Afrika Kusini na hakuna sababu kwa nini isiwepo Uganda, Rwanda, DRC na kwingineko. Kisheng (cha Kenya) kinavutia zaidi kwa sababu ya wingi wa lugha zinazochangia maneno na ubunifu wa hali ya juu katika uundaji na mpangilio wake wa maneno. Pia kina Historia ndefu zaidi - pengine kuanzia miaka ya 60 kinyume na "Kisheng" cha miji mingine ambacho kimsingi kimeibuka hivi karibuni kama tokeo la makali ya utandawazi...

  ReplyDelete
 3. Mzee ipo powa sana yani maana hata mimi inanikumbusha mbali sana kaka Matondo,kuna jamaa yangu nilikuwa nae mitaa ya Armağan City na alinipa story kama hiyo,nadhani msanii alicopy kwa huyo jamaa maana kilichobadilika ni idadi ya pesa tuu maana jamaa alitumiwa 100,000 na msanii katumiwa 80,000....

  ReplyDelete
 4. Bwana Bwaxb. Pengine hiki ni kisa jumuishi huko Kenya. Niliupenda ujumbe uliomo ingawa sina uhakika kama kijana kweli asiye na kipato (wala mjomba aliyeko USA) ataweza kuvishinda vishawishi vya mama sweet. Walokole wa kweli pengine...

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU