NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, January 22, 2010

MHESHIMIWA PINDA ALIPOTEMBELEA "ALMA MATER" YAKE - PUGU SECONDARY SCHOOL

 • Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika Bweni la Mapinduzi One, alilolala wakati akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu kwenye miaka ya 60. Mheshimiwa Pinda alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo, Januari 21, 2010. (Picha na maelezo ni kutoka kwa Father Kidevu)
**********************************
 • Picha hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu imenifikirisha. Sina uhakika kama hii ndiyo "Pugu Secondary" aliyoiacha. Sina uhakika kama hili ndilo Bweni la Mapinduzi One alimolala wakati akisoma hapa. Sijui hapa Mheshimiwa anawaza nini baada ya kuona bweni lake alipendalo likiwa katika hali hii. Uso wake unaonyesha huzuni!

3 comments:

 1. Hii inaonyesha wazi vile Watanzania hatuna utamaduni wa ukarabati. Ni aibu kuona mambo badala ya kusonga yanarudi nyuma. yaani shule ilikuwa nzuri enzi za ukoloni kuliko ilivyo sasa. Huo ni mfano tu wa shule moja. Tembelea shule nyingine nyingi za serikali, ufananishe zamani na sasa. utatamani kulia

  ReplyDelete
 2. Matondo, umenikumbusha mbali, bweni aliloishi Pinda yaani mapinduzi one ndilo bweni nililoishi mimi wakati nilipojiunga na sekondari ya Pugu kwa masoma ya A' level mwaka 1989/1991.

  ReplyDelete
 3. Godwin. Usipoziba ufa, utajenga ukuta. Hata sijui ni kwa nini tuna hii methali katika lugha yetu. Pengne hatujui maana yake! Utakuta kashimo kadogo kanajitokeza barabarani, hakuna anayejali. Ukikaona kashimo kale kale baada ya mwezi mmoja utakuta kamegeuka dimbwi na huo ndio mwanzo wa barabara kuharibika. Hii ni nzuri kwani inaonyesha kwa ubayana sana tatizo letu mojawapo kuu - kutojali!

  Ukiliangalia hili bweni la Mapinduzi One unashangaa. Hata kuweka "Ceiling Board" mpya tu haiwezekani? Kuna kawaida ya maeneo wanayotembelea wakubwa kupambwa kabla ya ziara zao. Naona Mhishimiwa pengine aliwashutukiza hawa kwani hawakuwa na muda hata wa kuweka ceiling board mpya!

  Bwana Malkiory, itakubidi umtafute Mheshimiwa Pinda ili mpange mkakati wa kuweza "kulifufua" bweni lenu la Mapinduzi One!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU