NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, January 21, 2010

MIUJIZA KUTOKA HAITI: MTOTO WA MIAKA MITANO AKUTWA AKIWA HAI BAADA YA SIKU NANE

 • Kama nilivyowahi kugusia hapa, kweli kama siku zako hazijafika hazijafika tu. Mtoto wa miaka mitano amepatikana leo kule Haiti akiwa hai SIKU NANE tangu nchi hiyo ikumbwe na tetemeko kubwa la ardhi. Mama yake alifariki katika tetemeko hilo na baba yake hajulikani aliko. Haijajulikana kama mtoto huyo alikuwa na njia ya kujipatia chakula na maji katika kipindi alichokuwa chini ya kifusi. Madaktari wamesema hana mifupa iliyovunjika ingawa alikuwa ana upungufu mkubwa wa maji mwilini. Miujiza kama hii huwa inatia moyo na kuleta matumaini katika nyakati za giza kama zinazoikumba Haiti kwa sasa. Tazama video hapa na kwa habari kamili zaidi tembelea hapa.
KWINGINEKO
 • Serikali ya Haiti imesema kwamba mpaka sasa maiti 72,000 wameshapatikana. Mashirika mbalimbali yanakadiria kwamba pengine watu wapatao 200,000 wameangamia katika tetemeko hilo.
 • Matetemeko mengine matatu katika miaka 100 iliyopita ndiyo yaliangamiza watu wengi zaidi kuliko hili la Haiti:
1920 - China - liliua watu 200,000 au zaidi
1976 - China - liliua watu 225,000
2004 - lilisababisha sunami katika nchi mbalimbali za Asia na kuua watu zaidi ya 300,000.

2 comments:

 1. Yes, huma spirit can be very enduring. I hope this boy will grow up, be seccessful and tell his story to the world. God bless.........

  ReplyDelete
 2. EDWARD ALEX MKWELELEJanuary 21, 2010 at 11:15 PM

  HAYA NI MAMBO YA MUNGU KUYAZUWIA HAYAWEZEKANI, LAKINI NINA SWALI, TUNAWEZA KUTABIRI HALI YA HEWA, I MEAN WEATHER NOT CLIMATE AS THERE IS DIFFERENCE BETWEEN WEATHER AND CLIMATE, WEATHER NI HALI YA MABADILIKO YA HALI YA DUNIA YA KILA SIKU WAKATI CLIMATE NI MABADILIKO YA MUDA MREFU INAWEZA KUCHUKUWA HADI MIAKA 30, AND HERE COMES GLOBAL WARMING. LAKINI HAPA NATAKA KUULIZIA WEATHER. WATABIRI WANAWEZA KUSEMA KESHO SAA KADHAA KUTAKUWA NA SNOW KALI SO JAMANI MUJIANDAE, SO HIVI HAKUNA UWEZEKANO WA KUTABIRI TETEMEKO WATU WAKAJIANDAA KUTOKA NJE NA KUKAA MAHALA PEUPE

  NI MIMI TENA
  EDWARD ALEX MKWELELE
  edwardmkwelele@yahoo.co.uk

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU