NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, January 22, 2010

NI KWELI AU NI KAULI MBIU YENYE OMBWE?

 • Kama asemavyo mhusika mmojawapo katika tamthiliya mashuhuri ya Tartuffe (Mnafiki) iliyoandikwa na Moliere, sote tunajua kwamba njia kati ya azimio na kitendo ni ndefu. Hayo maneno kwenye picha (ambayo naamini ni kibwagizo cha chama kimojawapo cha siasa) ni dhamira ya kweli watakayoitekeleza au ni kauli mbiu tu yenye ombwe watakayoitelekeza? Kuna lolote ambalo wamelifanya kutuaminisha kwamba wataitekeleza kauli mbiu yao hii kwa vitendo wakiingia madarakani au ni yale yale ya "Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa?"

5 comments:

 1. Sina uhakika LAkini kwa mtazamo wangu bado hatuna vyama vya upinzani vyenye nia thabiti na upinzani wetu bado hauna nguvu za kutosha

  ReplyDelete
 2. hata CCM ilianza hivi, pia siasa ni kudanganyana kwa hiyo lazima utumie madhaifu (yawe ya kweli au feki) ya mshindani wako ili upate nachokihitaji, ukiishapata basi unafurahia na kuanza kutunga uongo mwingine mwingine!

  ReplyDelete
 3. Nawasiwasi aliyepewa tenda ya kuandika hayo maneno yenyewe aweza kuwa FISADI.:-(

  Lakini labda turudie moyo chanya na kuamini kuwa angalau hatakama kwa vitendo hawatendi, ILA angalau wanasema ,- kitu ambacho Watanzania tumebarikiwa.:-(

  ReplyDelete
 4. Salaam aleikum Prof Nzuzullima na wana-blogu, kwanza kabisa nikiri kuwa mimi ni mgeni katika globu ya prof Matondo. Hoja: Waswahili husema 'mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni'. Hii ni kaulimbiu ya Chadema na hatuna budi kukubali kuwa wamekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi (ufisadi kwa maana ya kleptocracy - kansa inayotafuna taifa wakati wanajamii wanacheka). Mapambano dhidi ya ufisadi ambayo yameshika kasi katika kipindi cha takriban miaka miwili iliyopita yalizinduliwa rasmi na kuongozwa na Chadema - pale MwembeYanga, Temeke, tarehe 15 Sept 2007 ambapo orodha ya kwanza ya mafisadi ilianikwa hadharani (na hadi sasa bado iko katika tovuti/wavuti wa CHADEMA) ikiwa na maelezo fafanuzi. Yafuatayo ni majina katika orodha hiyo na matokeo hadi sasa:
  Hyt Daudi Balali (alitoroka na kwa bahati mbaya kufia ughaibuni); Mhe Anderea Chenge (mzee wa vijisenti alilazimishwa kuachia ngazi ya uwaziri); Mhe. Basil Mramba (yuko mbele ya pilato); Mhe Gray Mgonja (mbele ya pilato); Mhe Patrick Rutabanzibwa (sijui yuko wapi); Mhe Nimrod Mkono (huyo bado anapeta); Mhe. Nazir Karamagi (alilazimishwa kuachia ngazi ya uwaziri); Mhe Rostam Azziz (anaendelea kupika majungu); Mhe Edward Lowassa (alilazimishwa kuachia uwaziri mkuu); Mhe Ben Mkapa ( leo hii akialikwa katika hafla za hadhara anajiuliza mara mbili na mara nyingi anakacha kwa kusafiri nje); Mhe Jakaya Kikwete (anaendelea kuhangaika kuyakingia kifua mafisadi, sitashangaa akiondoka nayo). Kama si MwembeYanga sijui kasi mpya ya ufisadi ingekuwa imelifikisha wapi taifa? Jamani MNYONGE MNYONGENI...
  bwenge

  ReplyDelete
 5. Prof. Bwenge. Umetoa data nzuri na hoja yako imejengeka vizuri. Sikujua kama Chadema wameshafanya yote haya. Kama ni hivi basi wanastahili kuhongereshwa!

  Mjadala niliokuwa najaribu kuuibua ni ule uliojengwa katika uzoefu kwamba mara nyingi watu - hata wawe wakereketwa na wapigania haki namna gani - wanapokifikia kilele cha madaraka hugeuka na kutenda yale yale ya watangulizi wao. Siku mpya itapambazuka kama siku moja (na naamini siku hiyo itafika) chama cha upinzani kitachukua madaraka na kutenda yale kinayoyapigania. Hili la mwisho ndilo nina wasiwasi nalo!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU