NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, January 14, 2010

NIMEANZA KUWAZA NA KUWAZUA - INAWEZEKANA AIKA M. ALIKUWA NA POINTI!

Siku ya Ijumaa tarehe 14, 2009 nilitundika katika blogu hii mada iliyosema UTAFITI: WATU WEUSI NDIYO WANAONGOZA KWA UNENE. Mada hiyo ilichemka sana na iliishia kuwa na maoni mengi. Kati ya watoa maoni waliochemka sana na kung'ang'ania msimamo wao pamoja na kushambuliwa kulia na kushoto ni mdau mmoja aliyejiita Aika M. Yeye alianza maoni yake hivi:

"Watu weusi wamelaaniwa. Popote pale utakakowapeleka iwe ni Afrika, Ulaya, US, Jamaika, Haiti all ni the same. Incompetence, laziness, dirty and poverty. Halafu tukiambiwa kwamba we are a cursed race tunalalamika. I wish I were not black becauese it is a shame. Nikipata mzungu wa kunioa au siku nikienda nje, I will never come back to Africa again"

Aika M. aliendelea

"Don't blame everything on the white man - allover the world. Mzungu ndiye anatulazimisha tuwe mafisadi? Mzungu ndiye anatulazimisha tuwe lazy? Kwa nini hatuwezi kuwa na transparent society? Kwa nini hatuwezi kuwa na viongozi wanaojali watu wao? Kwa nini tusiwe na responsible leaders? Ni kwa sababu ya mzungu? I don't think so. Ndiyo maana mimi naamini kwamba something is inherently wrong with blacks!...mtu mweusi ni masikini, mchafu, mvivu, maneno mengi, mpenda kufanyiwa vitu na ombaomba POPOTE DUNIANI.."

Nimekuwa nikiangalia taswira za kutoka Haiti tangu nchi hiyo ikumbwe na tetemeko kubwa la ardhi - taswira zinazoonyesha umasikini wa kutisha. Na kama kawaida, watu wanaohusika ni weusi. Inaonekana kama vile umasikini na mtu mweusi ni vitu vinavyokwenda pamoja duniani kote. Ndipo nilipoyakumbuka maoni haya ya Aika M - maoni ambayo sikukubaliana nayo na bado sikubaliani nayo. Japo ni hivi, nimeanza kufikiria, inawezekana Aika M alikuwa na pointi!

**********************************************
Data muhimu za Haiti

Idadi ya watu: 9, 035, 536
Makabila
: Mulatto na wazungu: 5%, Weusi 95%
Dini
: Waprotestanti 16%, Wakatoliki 80%, nyinginezo 4%
Zaidi ya nusu ya wakazi wanaamini pia katika "vudu"
Wanaojua kusoma na kuandika
: 52.9%
Wanaoishi katika umasikini
: 80%
GDP per capital
: $1,300
Ajira
: zaidi ya robo tatu hawana ajira za kuaminika.

7 comments:

 1. Data zaidi
  Zaidi ya nusu ya wakazi ni under 18
  Inasikitisha kwa kweli na INAUMA PIA
  Wanahitaji msaada JAPO WA MAOMBI

  Bado nakubaliana kutokubaliana na sehemu ya maoni ya Da Aika M

  ReplyDelete
 2. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!January 15, 2010 at 9:02 AM

  @Matondo: ni hilo tu ama kuna jingine linalokufanya ukubaliane na AIKA ze kwini?

  tujuze

  ReplyDelete
 3. Mzee wa Changamoto - Asante kwa nyongeza ya data. Inakuwaje zaidi ya nusu ya wakazi inakuwa na umri chini ya miaka 18? Pengine watu wanazaliana sana na halafu wanakufa mapema. Tunaweza pia kuongeza - uharibifu mkubwa wa mazingira. Jana kulikuwa na kipindi katika BBC na kilikuwa kinadai kwamba pengine Haiti ndiyo mfano nambari wani wa uharibifu mbaya kabisa wa mazingiwa. Watu wamekata mito yote na kubakiza asilimia 2 tu. Maji taka na maji ya kunywa vimechanganyikana na .....

  Ng'wanambiti - sina sababu nyingine. Mwanzoni hata mimi niliyachukulia maoni haya ya Aika kama maoni ya kichokozi tu na kichwa ngumu. Ninachokisema hapa ni kwamba pengine tunapaswa kuyafikiria vizuri. Aika alikuwa anauliza ni kwa nini sasa imefikia hatua kwamba mtu mweusi (popote pale duniani) ni synonymous na neno umasikini? Umasikini huu unasababishwa na nini? Ni kwa sababu ya kutawaliwa na wazungu na kuendelea kubanwa katika mifumo ya kinyonyaji katika viwango vyote? Ni kwa sababu ya ufisadi na viongozi wasiojali matakwa ya umma? Ni kwa nini? Mtu ungeweza kufikiri kwamba nchi kama Haiti, kulingana na Jiografia yake, ingeweza kuwa tofauti kidogo.

  Sikubaliani na Aika lakini inabidi, kama watu weusi tuanze kufikiria kwa kina kuhusu sababu hasa zinazotufanya watu weusi kuwa hivi na hatua ambazo tunatakiwa kuzifanya. Tazama hapa, kwa mfano: http://matondo.blogspot.com/2009/11/kwa-ufisadi-kama-huu-afrika-tutaendelea.html

  ReplyDelete
 4. Siamini kama nitakubaliana moja kwa moja na Aika. Lakini haimaanishi kuwa napingana ama kumpinga kwa kila kitu. Kuna uzembe unaokera na kuuma. Tunajiharibia saana na hasa hii DIVIDE AND RULE iliyopo kwetu inatuua. Tanzania ndio kabisaaaaa
  Yaani maisha ya kitu kidogo yanatumaliza. Viongozi ...SORRY. WATAWALA wanahongwa na kusaini mikataba hewa kisha nao wanakwenda na kuwapuuzisha walio na uwezo wa kuongea huko vijijini na kuwapa kitu kidogo kisha wanaushawishi umma ukubaliane na "maendeleo" yao ambayo ni hatari kwa jamii.
  Hivi kuna mtu mwenye akili timamu asiyejua athari za tetemeko likitokea Dar? Majengo ambayo yalisemwa yamepinda na kusemwa yamejengwa kinyume na taratibu za kiusalama leo hii yanatumika. Hakuna barabara na sijui ukitokea mzozo tutasaidiana vipi? Foleni sasa hivi imefikia hatua mbaya na ni karaha kusafiri kwa gari kuliko kwa miguu. Hakuna maegesho bali kinachoongezeka ni 'vikwangua anga' tusivyohitaji kwani haviendani na ukuaji wa miundombinu yetu.
  Mifumo ya majitaka iliyokuwepo wakati Dar ina watu laki kadhaa ndio inayotumika kwa mamilioni leo hii na hakuna anayehoji. Unadhani hawajui?
  Hakuna anayejali maslahi ya nchi
  Ndio maana nami nimeandika kuwa HAITI SIO HAITI. Ni kioo kinachonionesha Tanzania siku zijazo (http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/01/niangaliapo-haiti-naiona-tanzania.html). Ama kwa ujumla wake http://changamotoyetu.blogspot.com/search/label/Tanzania%20yangu
  Nasikitika kusema hili kwani ikitokea yaliyotokea Haiti, kwetu yaweza kuwa aibu zaidi. Nasema sasa ili baadae tukubaliane kuwa TULIKWISHAONYWA (WE WERE WARNED)

  ReplyDelete
 5. Kinachohuzunisha zaidi ni ukweli kwamba Wanajiolojia na Wanasiesimolojia walikuwa wamewaonya viongozi wa Haiti miaka miwili iliyopita kwamba kulingana na data walizokuwa nazo kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa nchi hiyo kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi. Inavyoonekana, hakuna maandalizi yo yote yaliyofanyika.

  Tanzania pia tupo katika bonde la ufa ambapo misingi ya mabara inaachana. Tuombe sana tetemeko kubwa la aina hii lisije kutokea. Likitokea, hatutakuwa tofauti na Haiti!

  ReplyDelete
 6. Aika M (now studying in Sweden)January 21, 2010 at 9:53 PM

  Hi guys, this is Aika M. I was away...I am happy that you are now beginning to see my point of view. I cannot even manage to look at what is happenging in Haiti. It is more than sad, but hey we are blacks and that is what we do the best!!!

  ReplyDelete
 7. Aika wape hao...! Waonyeshe na hayo ya Ivory Coast! Mzungu pale ndio anang'ang'ania uraisi?????

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU