NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, January 25, 2010

SHUTTLE ZINAUZWA - WAJASIRIAMALI MPO?

 • Inasemekana kuwa shuttle hizi ndizo mashine tata na za kiwango cha juu zaidi zilizowahi kuundwa na binadamu na ni kielelezo bayana cha kilele cha mafanikio ya kisayansi yaliyofikiwa na Wamarekani katika milenia iliyopita.
 • Ziliundwa sita tu - Enterprise, Columbia, Discovery, Challenger, Atlantis na Endeavour. Challenger iliripuka mwaka 1986 wakati ikijaribu kuruka na Columbia iliteketea mwaka 2003 katika angala la Texas wakati ikielekea kutua kule Kennedy Space Center jimboni Florida. Mpaka sasa ni tatu ndizo bado zinaendelea kupiga mzigo wa kwenda na kurudi katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za juu (Discoverry, Atlantis na Endeavour)
 • Shuttle hizi zimepangiwa kustaafishwa mwaka huu (2010) na tayari NASA inazipiga bei. Bei ya awali ilikuwa dola milioni 42 kwa kila shuttle na sasa bei imepunguzwa na kuwa dola milioni 28.8. Inaaminika kwamba shuttle hizi zitakuwa kivutio kikubwa cha utalii huko mbeleni.
 • Hakuna kweli liTanzania angalau limoja lenye pesa (hata kama ni lifisadi sawa tu) likanunua shuttle mojawapo na kututoa kimasomaso kwa kusaidia kuimarisha sekta yetu ya utalii huko mbele? Tukiongezea shuttle mojawapo na mabaki ya ile rada yetu ya bei mbaya, (+ K'njaro, Serengeti, Ngorongoro na Z'bar yetu) bila shaka tutawika sana katika sekta ya utalii huko mbele.
 • Itazame Atlantis hapa ikitua. Nimepanga kwenda kushuhudia kutua kwa shuttle hizi zitakapofanya safari zake za mwisho mwisho!


3 comments:

 1. Samahani Bwana Matondo mie nataka kujua nini kinachozifanya hizi shuttle kuwa za kiwango cha juu na tata kaitka vitu vilivyowahi kuundwa na binadamu?...Ahsante Abraham

  ReplyDelete
 2. Bwana Abraham: Tazama hapa:

  http://spaceflight.nasa.gov/shuttle/upgrades/upgrades5.html

  Au soma hii karatasi hapa:

  http://spaceflight.nasa.gov/spacenews/factsheets/pdfs/21stCenturyShuttle.pdf

  Inawezekana pia ikawa ni Wamarekani tu wanajisifia kuhusu shuttle zao hizi. Wanasayansi wanajua lakini kwa mbumbumbu kama mimi, hii inatosha kuniaminisha kwamba kweli pengine hizi shuttle ndizo mashine tata kabisa. Wewe unaonaje?

  ReplyDelete
 3. Ningetamani saana kwenda kuziona. Niko naitembelea ile iliyopaki hapa Museum (http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/05/changamotos-day-out.html) lakini nafuatilia saaana shughuli zao. Hii kitu inatisha na ukisikia maandalizi yao (kama nilivyohojiana na Astronaut Dr Thomas hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/05/kutoka-shamba.html) unaweza kuwaza mara mbili kama unaweza mruhusu nduguyo yeyote kwenda huko.
  Ni UTATA zaidi ya UTATA

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU